Kuongezewa Mshahara

Kuongezewa Mshahara

Spartacus boy

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2020
Posts
1,727
Reaction score
3,464
Habarini wanajukwaa,

Mimi ni mhitimu wa chuo kikuu kwa elimu ya ngazi ya degree kwa mwaka 2021.

Mwaka 2022 nilibahatika kupata kazi katika kampuni moja ya BINAFSI ambapo nilipita kihalali katika nafasi moja ya kazi ilokuwa inahitaji watu sabini na kitu hivi.

Katika tangazo lao la kazi, kampuni iliainisha sifa za elimu ni kidato cha nne hadi degree. Ili kutafuta fursa nami niingie niliamua kuomba lakini shida ni ilikuwa vyeti.

Yaani mkononi nilikuwa na cheti tu cha form six. Cha chuo sikuwa nacho na hapo kumbukeni nilikuwa nishagraduate bila hata "kimeo" kimoja ila shida ni kuwa sikuweza kwenda kukifata kwa muda huo kutokana na uchumi kwani hata mahafali sikubahatika kufanya.

Mungu si Athuman niliapply hivyo hivyo nikapata kazi . Na uzuri walichanganya watu wa elimu mbalimbali .

Shida ni kiwango cha Mshahara (haimaanishi hakikidhi) ila ni kwamba tunalipwa kutokana na elimu yako.

Mwaka jana niliomba ruhusa kazini nikafuata vyeti vyangu vya chuo na nikavipata.

Nikarudi kazini kuonana na HR (kipindi hicho alikuwepo huyu msaidizi) akanambia ya kuwa muda wa probation bado haujaisha (miezi sita) so nikaongee na manager wangu yeye ndo ataandika " ripoti" juu ya utendaji kazi wangu. Na mimi nikafanya hivyo.

Manager akanambia ya kuwa yeye atajaribu kuongea na HR aone nini atanisaidia.

Imepita si muda manager huyu wa sasa kahamishwa kituo cha kazi. Kabadili mwingine na pia katika kampuni kaja HR mkuu wa tawi kitaifa (ni mwanaume).

Nilivyomface huyu manager mpya kasema niende kwa HR msaidizi (kumbuka huyu ndo alinambia niende chini kwa manager kwanza).

Sasa mimi nataka niende moja kwa moja kwa HR Mkuu.

Msaada kwenu wakuu kama mshawahi kukutana na hii:
1. Je nikienda kwa HR Mkuu nitakuwa nimekosea?

2. Ni vitu vipi au technic zipi za kutumia ili nimshawishi aniongezee mshahara?

3. Msaada wenu positive nipo tayari kuupokea.
 
Kwanza tuulize, iyo course uliyosomea inahitajika hapo ofisini kwenu? Unaweza kuta wao hawahitaji Diploma wala Degree katika wafanyakazi wake wanahitaji tu muhitimu wa form 4 au 6 ndio maana wakakuchukua mara ya kwanza.

Pili, je wananafasi ya iyo ngazi unayotaka kupandishwa? Na je majukumu yako yatabaki ayo ayo au yatabadirika?

Na mwisho itakua budget yao. Jumlisha huruma wa HRs.

Sema nini, give a try. Kikubwa tumia busara sana baada ya kusoma mchezo. Jua jinsi ya kumuingia uyo mkuu HR. Atakusaidia ata kwa mawazo nini cha kufanya.
 
Ahsante mkuu
 
Majukumu yanabaki vile vile
 
Habarini wanajukwaa,

Mimi ni mhitimu wa chuo kikuu kwa elimu ya ngazi ya degree kwa mwaka 2021.

Mwaka 2022 nilibahatika kupata kazi katika kampuni moja ya BINAFSI ambapo nilipita kihalali katika nafasi moja ya kazi ilokuwa inahitaji watu sabini na kitu hivi.

Katika tangazo lao la kazi, kampuni iliainisha sifa za elimu ni kidato cha nne hadi degree. Ili kutafuta fursa nami niingie niliamua kuomba lakini shida ni ilikuwa vyeti.

Yaani mkononi nilikuwa na cheti tu cha form six. Cha chuo sikuwa nacho na hapo kumbukeni nilikuwa nishagraduate bila hata "kimeo" kimoja ila shida ni kuwa sikuweza kwenda kukifata kwa muda huo kutokana na uchumi kwani hata mahafali sikubahatika kufanya.

Mungu si Athuman niliapply hivyo hivyo nikapata kazi . Na uzuri walichanganya watu wa elimu mbalimbali .

Shida ni kiwango cha Mshahara (haimaanishi hakikidhi) ila ni kwamba tunalipwa kutokana na elimu yako.

Mwaka jana niliomba ruhusa kazini nikafuata vyeti vyangu vya chuo na nikavipata.

Nikarudi kazini kuonana na HR (kipindi hicho alikuwepo huyu msaidizi) akanambia ya kuwa muda wa probation bado haujaisha (miezi sita) so nikaongee na manager wangu yeye ndo ataandika " ripoti" juu ya utendaji kazi wangu. Na mimi nikafanya hivyo.

Manager akanambia ya kuwa yeye atajaribu kuongea na HR aone nini atanisaidia.

Imepita si muda manager huyu wa sasa kahamishwa kituo cha kazi. Kabadili mwingine na pia katika kampuni kaja HR mkuu wa tawi kitaifa (ni mwanaume).

Nilivyomface huyu manager mpya kasema niende kwa HR msaidizi (kumbuka huyu ndo alinambia niende chini kwa manager kwanza).

Sasa mimi nataka niende moja kwa moja kwa HR Mkuu.

Msaada kwenu wakuu kama mshawahi kukutana na hii:
1. Je nikienda kwa HR Mkuu nitakuwa nimekosea?

2. Ni vitu vipi au technic zipi za kutumia ili nimshawishi aniongezee mshahara?

3. Msaada wenu positive nipo tayari kuupokea.
Maliza Probation Period Kwnza usitafute Report Mbovu kazini
 
Upo ktk nafasi ambayo mtu wa form4, 6, certificate, diploma au degree anaweza kuifanya... Kwahio hiyo sio professional.
Nakushauri fanya kazi kwa bidii maarifa na weledi (usifanye kazi kujionyesha) hivyo utendaji kazi wako ndio utakao kubeba... Wao ndio wataona umuhimu wa kukupa nafasi itakayohitaji vyeti vya chuo na kukuongeza mshahara...
Kwasasa usilazimishe uongezewe mshahara bali waandikie barua kuwajulisha umosemea fani fulani upo tayari kuitumikia nafasi fulani watakapohitaji mtu...
MDOGO WANGU NYONGEZA YA MSHAHARA SIO JAMBO RAHISI
 
Ilishakwisha mkuu
Tatizo linakuja Kwenye Ajira!
Ajira yako Inasoma kama nani?
Maana kwa Cheti gani?

Nimeuliza Probation nikiwa namaanisha kuwa Baada ya probation Inabdi ukitumikie Cheo Hicho kwa mwaka Mmoja na Upewe mkataba wa Ajira wa mwaka mmoja..

Na baada ya Hapo Inabidi Waangalie Taratibu sasa za Promotion!
NA hapo Ndo utapeleka Vyeti vya Bachelor..

Kosa ulilifanya mwanzoni kabisa kupeleka Cheti cha Form six
Wazungu wanasema
"Mess up in a contract, and you're stuck with the deal."

Au
"Contracts are binding, so mistakes can't be ignored."

Hapo HR wanashindwa kukwambia ukweli ni kwmba ni mpaka Mwaka mmoja uishe ndo wakufanyie Promotion..

Labda wakuajiri upya
 
Mkuu cheti nilichokuwa nacho mkononi ni kilikuwa cha form six. Cha chuo sikuwa nacho kwa sababu ya uchumi . Maana chuo nimesoma km 900 toka mkoa naoishi.
So ilikuwa ni kitu kigumu kuandika katika cv yangu kuwa nija degree ilhali kiambatanisho cha hiyo degree( cheti sina mkononi) kwa wakati huo.
 
Nimekuelewa na ndo maana nimessma sometimes Mistakes inaweza kuleta matatizo
 
Mkuu cheti nilichokuwa nacho mkononi ni kilikuwa cha form six. Cha chuo sikuwa nacho kwa sababu ya uchumi . Maana chuo nimesoma km 900 toka mkoa naoishi.
So ilikuwa ni kitu kigumu kuandika katika cv yangu kuwa nija degree ilhali kiambatanisho cha hiyo degree( cheti sina mkononi) kwa wakati huo.
Sasa una4c nn? Akat wee uliweka cha 4m 6? Subiri utaratibu mwingne, usikurupukee.
 
Hapo kama kuna wa degree ambae mnafanya kazi sawa (Majukum sawa ila mnalpwa tofaut kwakuw yeye ana bachelor)
Muandikie barua yako ya ku update taarfa zako za kitaaluma na kuomba kufanyiwa recati au kupandishwa cheo kutokan na kanuni za kiutumish apo kazn kwenu🐼. KiLa la heri msomi
 
Mkuu cheti nilichokuwa nacho mkononi ni kilikuwa cha form six. Cha chuo sikuwa nacho kwa sababu ya uchumi . Maana chuo nimesoma km 900 toka mkoa naoishi.
So ilikuwa ni kitu kigumu kuandika katika cv yangu kuwa nija degree ilhali kiambatanisho cha hiyo degree( cheti sina mkononi) kwa wakati huo.
Ulitakiwa kuandika kwenye CV yako kuwa una degee haikuzuii hata mama cheti usingeweka. Basi vema utumikie nafasi hiyo angalau mwaka mmoja wakati wa promotion ndio upeleke au kaongee na HR uelezee scenario.

Mbona husemi ni aina gani ya kazi unafanya na umesomea programme gani kwenye shahada yako
 
Back
Top Bottom