Spartacus boy
JF-Expert Member
- Sep 22, 2020
- 1,727
- 3,464
Habarini wanajukwaa,
Mimi ni mhitimu wa chuo kikuu kwa elimu ya ngazi ya degree kwa mwaka 2021.
Mwaka 2022 nilibahatika kupata kazi katika kampuni moja ya BINAFSI ambapo nilipita kihalali katika nafasi moja ya kazi ilokuwa inahitaji watu sabini na kitu hivi.
Katika tangazo lao la kazi, kampuni iliainisha sifa za elimu ni kidato cha nne hadi degree. Ili kutafuta fursa nami niingie niliamua kuomba lakini shida ni ilikuwa vyeti.
Yaani mkononi nilikuwa na cheti tu cha form six. Cha chuo sikuwa nacho na hapo kumbukeni nilikuwa nishagraduate bila hata "kimeo" kimoja ila shida ni kuwa sikuweza kwenda kukifata kwa muda huo kutokana na uchumi kwani hata mahafali sikubahatika kufanya.
Mungu si Athuman niliapply hivyo hivyo nikapata kazi . Na uzuri walichanganya watu wa elimu mbalimbali .
Shida ni kiwango cha Mshahara (haimaanishi hakikidhi) ila ni kwamba tunalipwa kutokana na elimu yako.
Mwaka jana niliomba ruhusa kazini nikafuata vyeti vyangu vya chuo na nikavipata.
Nikarudi kazini kuonana na HR (kipindi hicho alikuwepo huyu msaidizi) akanambia ya kuwa muda wa probation bado haujaisha (miezi sita) so nikaongee na manager wangu yeye ndo ataandika " ripoti" juu ya utendaji kazi wangu. Na mimi nikafanya hivyo.
Manager akanambia ya kuwa yeye atajaribu kuongea na HR aone nini atanisaidia.
Imepita si muda manager huyu wa sasa kahamishwa kituo cha kazi. Kabadili mwingine na pia katika kampuni kaja HR mkuu wa tawi kitaifa (ni mwanaume).
Nilivyomface huyu manager mpya kasema niende kwa HR msaidizi (kumbuka huyu ndo alinambia niende chini kwa manager kwanza).
Sasa mimi nataka niende moja kwa moja kwa HR Mkuu.
Msaada kwenu wakuu kama mshawahi kukutana na hii:
1. Je nikienda kwa HR Mkuu nitakuwa nimekosea?
2. Ni vitu vipi au technic zipi za kutumia ili nimshawishi aniongezee mshahara?
3. Msaada wenu positive nipo tayari kuupokea.