SoC04 Kupambana na Changamoto za Vijana Kupata Mikopo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Alexis Mbunda

New Member
Joined
Jan 10, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Kupambana na Changamoto za Vijana Kupata Mikopo.

Ningependa kuanza na swali inawezekanaje kijana alietoka kukopeshwa na serikali miezi michache iliyopita milion za pesa awe "hakopesheki" ilhali alikopeshwa bila ya kua na uhakika wa kupato cha kurudisha mkopo huo? Sasa kwanini kusiwe kuna bodi ya mikopo kwa vijana ambapo (ndio kuna changamoto ya uelewa wa biashara na usimamizi) watapeleka taarifa zao kama bodi ya mikopo ambapo zitakua na mawazo ya biashara watakaofuzu watapatiwa mikopo yao yenye riba nafuu na ambao hawatafaulu wataendelea kujifunza zaidi ili waweze kukidhi vigezo, hii itasaidia vijana kutenga mda kwenye kujifunza ujuzi wa biashara, andiko mradi na kutengeneza mtazamo kwamba kila kitu kipo ni wao tu kua na wazo hivyo wataacha kuilaumu serikali (kama serikali itafanya jukumu lake kwa kua imeshindwa kutoa ajira ila vijana wakijiajiri wataendelea kutoa ajira kwa vijana wengine pia)
Pili kuwa na usimamizi madhubuti mfano, baadhi ya maafisa mikopo hua wanaomba rushwa katika hio hio mikopo ambayo wanatoa sasa mtu akipata mkopo aje alipe riba atoe ba rushwa anakua bado hajasaidika.

Serikali inaweza kufuatilia taarifa za wanufaika wa mikopo kwa Kutumia vitambulisho vya taifa, kujua mtu yupo wapi sehemu alipo ili iwe rahisi kuaminika na kumtafuta pale anapodaiwa pia inaweza kuboresha ufuatiliaji wa vitambulisho hivyo kwa kuhamasisha matumizi ya vitambulisho hivyo katika sehemu za muhimuj ambapo kila mtu analazimika kutumia au kupita katika sehemu hizo mfano, ofisi za serikali, benki, na checkpoint za barabarani ili kufahamu kitambulisho fulani kinapatikana sana maeneo fulani.

Chanzo cha Changamoto

Changamoto ya vijana kupata mikopo ni kikwazo kikubwa katika maendeleo yao kiuchumi. Vijana wanakabiliwa na vikwazo vingi katika kupata ufikiaji wa fedha kwa sababu ya ukosefu wa historia ya mikopo, uzoefu wa biashara, na dhamana. Changamoto ya vijana wengi masikini lengo la mkopo ni kutatua matatizo yao na sio kufanya biashara izalishe ulipe mkopo ndo maana lazima kurudisha mkopo inakua changamoto kubwa au utakopa sehemu nyingine kulipa mkopo so maisha yako yatakuwa ni mkopo tu, inakua ni shughuli ya kuhamisha deni tu.

Changamoto Zinazowakabili Vijana

Kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana kinasababisha kushindwa kwa vijana kutimiza vigezo vya kupata mikopo kutoka kwa taasisi za kifedha. Aidha, kutokuwa na elimu ya kifedha na ufahamu mdogo wa jinsi ya kutumia mikopo ni changamoto nyingine inayowakabili. Benki na microfinance zinatoa mikopo ya riba nafuu lakini ni kwa watu wenye sifa (wanaokopesheka) na wakopeshaji wasio rasmi (kausha damu) wanatumia hiyo fursa ya vijana kutokukopesheka kupata faida zaidi na zaidi sababu wanajua vijana hawana vigezo yani hawakopesheki na wana shida inabidi warudi kwenye taasisi zisizo rasmi ndio hizo kausha damu ambapo ni kubwa sana kulingana na aina ya mkopo, ambapo mwisho wa siku mkopo huo hautamsaidia kijana.

Njia za Kutatua Changamoto

Kurasimisha taasisi binafsi.
Taasisi binafsi zinaojihusisha na utoaji wa mikopo hususani mikopo ya mitandaoni imekua kimbilio la vijana wengi kwa kua ni mikopo ambayo hahihitaji dhamana licha ya kua na riba kubwa na kiwango cha mkopo kua kidogo ndiyo imekua kimbilio kwa kua vijana wengi hawana uwezo wa kuweka dhamana (kukopesheka). Taasisi hizo kwa kua sio rasmi zinachukua taarifa binafsi za watu na kutumia kama dhamana ikiwemo kutumia taarifa hizo kudhalilisha walengwa au kutumia taarifa za uongo kwa walengwa mitandaoni, hivyo sio msaada sana kwa vijana bali imekua ni changamoto kwa kua vijana wengi. Hivyo kama taasisi hizi zipo kwa ajili ya kuwasaidia vijana zikirasimishwa, kuwa na utaratibu sahihi wa kutumia taarifa hizo na kuwa na riba nafuu, suala hili litakua msaada na kupunguza wimbi la vijana kutokukopesheka.

Lakini pia kuruhusu jamii za kimataifa na sekta binafsi kuwekeza katika hilo sanjari na kutoa elimu ya mikopo kwa vijana katika ngazi za chini zaidi mfano wengi huona ni bora kukopa katika program za mitandaoni ambazo zinatoa mikopo ya riba kubwa sana ndani ya muda mfupi, kutokana na ukosefu wa elimu na uelewa mdogo wa mikopo walengwa hawahesabu riba wala hawaangalii undani wa taarifa wanazotoa kama dhamana ya kupata mikopo hiyo, mfano mkopo ndani ya wiki moja mtu atatakiwa kulipa riba ya 50% na kuendelea kadri deni linavyozidi, huu ni unyonyaji wa hali ya juu inayochangiwa na umaskini na ukosefu wa elimu, mtu haangalii athari sababu ya shida inayomkabili, hapa ndio inatakiwa usimamizi wa serikali kwa ajili ya kuzikabili hizi taasisi ambazo zinasaidia kutoa mikopo lakini zina riba ya juu sana.

Njia zingine zinazoweza kutumika.

Vikundi vya akiba na kukopa.
Vicoba ni njia mbadala inayoweza kumkomboa kijana na kuwezesha kupata mkopo hivyo serikali na wadau mbalimbali wanaweza kuwekeza na kutoa fedha katika halmashauri ambapo vijana wanaweza kupata mikopo kwa kusajili vikundi na kurejesha fedha hiyo ya mkopo kama kikundi, kasha kuendelea na kikundi kwa kuwaingiza wanachama wapya.

Elimu ya Kifedha kwa Vijana: Vijana wenyewe wanaweza kuwekeza katika mipango ya elimu ya kifedha ili kuwajengea uwezo wa kuelewa mchakato wa kupata na kutumia mikopo ipasavyo, hata kabla hajapata mkopo kua na wazo bora tu na uelewa ni hatua mojawapo katika uelekeo sahihi.

Kuwezesha Ujasiriamali wa Vijana: Kutoa mafunzo na rasilimali kwa vijana ili waweze kuanzisha biashara zao na kujenga historia ya biashara inayoweza kusaidia katika kupata mikopo.

Kuendeleza Programu za Mikopo Maalum: Kuanzisha programu za mikopo maalum ambazo zinalenga mahitaji na uwezo wa vijana, ikiwa ni pamoja na masharti nafuu ya kulipa na viwango vya riba vya chini.

Kuwekeza katika Teknolojia ya Kifedha: Kukuza matumizi ya teknolojia ya kifedha ili kufanya huduma za kifedha ziweze kupatikana kwa urahisi zaidi na vijana.

Kushirikisha Sekta Binafsi na Mashirika ya Kijamii: Kufanya kazi na sekta binafsi na mashirika ya kijamii ili kubuni programu za mikopo zinazolingana na mahitaji ya vijana na kutoa msaada wa kifedha.

Kupunguza Urasimu: Kupunguza urasimu katika taratibu za kupata mikopo ili kufanya mchakato wa kupata mikopo uwe rahisi na wa haraka kwa vijana.

Kupitia njia hizi na mbinu nyingine za kujenga uwezo, serikali, taasisi za kifedha, na wadau wengine wanaweza kusaidia kupunguza changamoto za vijana kupata mikopo na kuwawezesha kufikia ndoto zao za kujenga uchumi imara na endelevu.

Inaweza ikawa inaonekana kama serikali imepiga hatua kukabiliana na hio changamoto ya mikopo kwa vijana lakini hapana haijawasaidia hata kidogo sababu viongozi wengi wa serikali kuanzia ngazi ya juu hadi afisa mikopo ngazi ya halmashauri nao wanaona ni sehemu ya kujipatia kipato, kwa mfano afisa mikopo kutaka sehemu ndogo ya mkopo atakaokuidhinishia hivyo ni changamoto kwa kua ni mkopo wa biashara itakua ngumu kupata faida, riba na kiasi ulichopunguza kumpa afisa mikopo.

Suluhisho la kumsaidia kijana wa hali ya chini kupata mkopo sio uwepo wa taasisi za mikopo ya haraka mitandaoni bali kuhamasisha uwepo wa kampuni hizo kwa wingi na zifuate utaratibu ramsi, Dawa ya mikopo isiyo rasmi inayowaumiza vijana na wannchi wengi wa hali ya chini ni kuondoa umasikini, kutoa elimu na kurasimisha taasisi hizo za mikopo sababu zinampa mlengwa uwezo wa kukubaliana na taasisi riba za mkopo na taratibu rafiki za urejeshaji, ila tukiwa na jamii masikini na isiyo na elimu walengwa watakuwa hawana nguvu wala uelewa wa kukubaliana na kuangalia mikopo iliyo nafuu kwao hivyo watakopeshwa kwa riba kubwa ambayo sio rafiki kwao kwa kua hawajui kiwango gani cha riba kitakua rafiki kwao ili kupata faida.
 
Upvote 3
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…