Kupanda ghafla kwa bei ya nyanya na mbogamboga iwe funzo kwetu

Zanzibar kitunguu kg 1 ni tsh 6000 Nyanya nazo bei juu kama ujuavyo ndugu zetu hawa hata kulima ni mtihan.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kifaa kinapatikana wapi hicho? na kwa chini ni jiko au napo ni kama juu?
 
Holla,

Dunia inaenda inabadilika na mambo yanayoizunguka yanaenda yanabadilika...

Wenyewe sikuhizi wanasema penye Udhia ndipo penye Rupia, ukiona kuna changamoto vaa miwani tizama bila kupiga kope utaona fursa....

Sitaki kwenda kinyume na mada tajwa ila ilisemwa mabadiliko hayana budi kuja na saa ingine yanakukuta hujajiandaa kukabili hayo mabadiliko maana maisha lazima yaendelee tumbo halielewi bei hazibembelezeki sokoni... Na usiombe kipindi cha namna hii uwe na mgonjwa, maana chakula ni sehemu ya tiba.

Changamoto hii ya mfumuko wa bei za vyakula na mboga mboga, suluhisho kadhaa zimetajwa huko juu moja ni watu wenye maeneo kujaribu kuwa na bustani za mboga mboga pia kipindi zipo bei rahisi wazihifadhi ili zitumike hadi kipindi zimeadimika.

Yote hii imeletwa na kadhia ya mvua miundombinu imeharibika mazao hayafiki kwa walaji hatimaye bei kupanda, hii pia ni kwa mazao makuu kama mchele maharage na mahindi....

Mbadala wa vyakula hivi ni nini ili tumbo liendelee kuchakata chakula?
Kuacha kula mchuzi na kachumbari, badala yake kula mboga ambazo hazihitaji kuungwa na nyanya mfano maharage na jamii yake.
Laah ukiamua kupika njegere au dagaa unaziunga na karanga bila kuweka nyanya kabisa.
Mboga za majani unaunga na nazi, nyama unakula ya kuchemsha mchuzi unaunga pembeni usio na nyanya mradi uweke nazi au karanga.

Wapenda kula kama mie hatukosi mbadala wa mapishi baadhi ya mahitaji yakiadimika au kupanda bei hadi hapo hali itaporudi kuwa sawa.

Kasinde.
 
Huwezi amini baada ya huu uzi naenda kutengeneza matuta ,2 ya mboga mboga.
Hadi jioni yatakua tayari
 
Huwezi amini baada ya huu uzi naenda kutengeneza matuta ,2 ya mboga mboga.
Hadi jioni yatakua tayari
Mimi ninamatuta matatu ya viazi lishe
Bustani ya matembere na Bamia
Kuna majani ya kunde hadi nyumba nzima yamewakifu nawaambiaga waniandalie supu ya majani ya kunde niibugie kila siku.

Vyote vimeanza kuphase out, njiandaa kuwa na more advanced yenye hadi herbal plants.
 


Aahahahahahahhaaaa looh ngoja nikunong'oneze fursa ukusanye njuruku....

Hapo kwenye supu ya majani ya kunde sababu wewe unainywa kila siku, Anza kuitangaza kuwa inaongeza nguvu za kiume na wewe ni shahidi, Anza kuuza mafungu ya majani ya kunde fungu 500 baadhi ya washkaji unaofanyanao kazi unawaandalia na kuwauzia supu iliyopo tayari, paki kwenye vikopo wanapasha wanakunywa.

Kumbuka hata wanaume wenye ndoa japo wake zao wanaweza andaa hiyo supu nyumbani hawatapenda mkewe au mpenziwe ajue kuwa anakula vyakula vinavyomfanya mtarimbo ukae wima kipindi chote cha mtanange. Hivyo watataka uwauzie wanywe warudi nyumbani wakafanye yao....

Kazi kwako ongeza matuta ya majani ya kunde, Ila kiukweli umetisha, supu ya majani ya kunde laaah!!!!!!, umewaza nini aahahahahahahahahahahaaaaaa.
 
Mkeo, housegirl, ndugu unaoishi nao, watoto wako au wewe mwenyewe badala ya kufanya jogging gym, au barabarani, au kuangalia movies kuhudumia bustani ya nyumbani hata nusu saa ni zoezi tosha Kwa wenye Muda.
Wanaishi ilala na kariakoo nyanya watapanda wapi
 
Huwezi amini baada ya huu uzi naenda kutengeneza matuta ,2 ya mboga mboga.
Hadi jioni yatakua tayari
Utapanda na kuvuna overnight..?
Wapi nimesema hivyo?
Nilimaanisha kuandaa matuta ndo itakua tayari
 
Kwakweli bei ya nyanya na vitunguu inatisha, uzuri carrots bei yake ni bwelele, pia waweza nunua carrots kama mbadala wa nyanya, unatia nyanya zako 2 unakuna carrot yako moja unapata mchuzi murua kabisa.
 
Hahaha
Nilijibunia tu hata sijui inaongeza nini.
Nilikuwa naokoa yasipotee bure maana wote wameyachoka.
 
Kwakweli bei ya nyanya na vitunguu inatisha, uzuri carrots bei yake ni bwelele, pia waweza nunua carrots kama mbadala wa nyanya, unatia nyanya zako 2 unakuna carrot yako moja unapata mchuzi murua kabisa.
Ubunifu murua kbs
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…