Bei ya nyanya iko juu. Mtaani kwetu wameacha kabisa kuuza.
Wakina mama wapika mihogo nimeona sehemu wanatumia matango kama nyanya Ktk kachumbari.
Leo nimeshangaa pia eti bamia moja inauzwa 100 mtaani.
Vitunguu na mbogamboga poa ziko juu.
Sababu
Nimefuatilia sababu wanasema mvua zilizozidi ndio chanzo.
Utatuzi wa kudumu na ushauri
Ule utamaduni wa kupanda maua majumbani ubadilishwe Kwa kupanda mbogamboga.
Mfano ukipanda kaeneo kadogo matembere yatastawi hata ukimwagilia maji ya sabuni.
Panda mbogamboga, nyanya, Vitunguu, karoti Ktk makopo.
Hii itasaidia kupunguza gharama ndogondogo zinazoepukika.
Mkeo, housegirl, ndugu unaoishi nao, watoto wako au wewe mwenyewe badala ya kufanya jogging gym, au barabarani, au kuangalia movies kuhudumia bustani ya nyumbani hata nusu saa ni zoezi tosha Kwa wenye Muda.