Kupanda ghafla kwa bei ya nyanya na mbogamboga iwe funzo kwetu

Kupanda ghafla kwa bei ya nyanya na mbogamboga iwe funzo kwetu

Holla,

Dunia inaenda inabadilika na mambo yanayoizunguka yanaenda yanabadilika...

Wenyewe sikuhizi wanasema penye Udhia ndipo penye Rupia, ukiona kuna changamoto vaa miwani tizama bila kupiga kope utaona fursa....hivi ukikosa kupikia nyanya muda mrefu si kuna upungufu wa vitamin utapata

Sitaki kwenda kinyume na mada tajwa ila ilisemwa mabadiliko hayana budi kuja na saa ingine yanakukuta hujajiandaa kukabili hayo mabadiliko maana maisha lazima yaendelee tumbo halielewi bei hazibembelezeki sokoni... Na usiombe kipindi cha namna hii uwe na mgonjwa, maana chakula ni sehemu ya tiba.

Changamoto hii ya mfumuko wa bei za vyakula na mboga mboga, suluhisho kadhaa zimetajwa huko juu moja ni watu wenye maeneo kujaribu kuwa na bustani za mboga mboga pia kipindi zipo bei rahisi wazihifadhi ili zitumike hadi kipindi zimeadimika.

Yote hii imeletwa na kadhia ya mvua miundombinu imeharibika mazao hayafiki kwa walaji hatimaye bei kupanda, hii pia ni kwa mazao makuu kama mchele maharage na mahindi....

Mbadala wa vyakula hivi ni nini ili tumbo liendelee kuchakata chakula?
Kuacha kula mchuzi na kachumbari, badala yake kula mboga ambazo hazihitaji kuungwa na nyanya mfano maharage na jamii yake.
Laah ukiamua kupika njegere au dagaa unaziunga na karanga bila kuweka nyanya kabisa.
Mboga za majani unaunga na nazi, nyama unakula ya kuchemsha mchuzi unaunga pembeni usio na nyanya mradi uweke nazi au karanga.

Wapenda kula kama mie hatukosi mbadala wa mapishi baadhi ya mahitaji yakiadimika au kupanda bei hadi hapo hali itaporudi kuwa sawa.

Kasinde.
 
Get readyyyyy


Sent from my iPhone using Tapatalk

Yeeey....

We go for the weekend...

We go for the weekend...

We = Kasie and Rogie.... Wuuuhuuuuuu

Am reeady you know am ready....
To go there.... to go there...
Forever...heey Mr. Man....

Come and pick me at 5 O'Clock..

K Matata.
 
View attachment 1348747
Hicho ni kikaushio cha kutumia mwanga wa jua. Nyanya inakatwa slices na kupangwa kwenye tray halafu inawekwa kwenye kikaushio kama hicho. Nanunua kipindi creti ni elfu 5, naanika kama creti 3 napata ndoo nzima ya nyanya kavu. Mwaka mzima hakuna kununua nyanya.
Mkuu nisaidie Naweza kupata wapi Hicho kifaa
Ikiwezekana Naomba mawasiliano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwezi amini baada ya huu uzi naenda kutengeneza matuta ,2 ya mboga mboga.
Hadi jioni yatakua tayari

Wapi nimesema hivyo?
Nilimaanisha kuandaa matuta ndo itakua tayari

Kama lengo ni kukimbizana na soko, hadi uje kuvuna bei itakuwa hii..?
 
Kifaa kinapatikana wapi hicho? na kwa chini ni jiko au napo ni kama juu?
Viko vya aina nyingi na Mimi siwezi kufika sehemu zote. Siwezi kufanya urasimu nakupa design ya kawaida kwa matumizi ya nyumbani. Tafuta plastic sheet Kama ya greenhouse, Jenga mstatiri kama hapo kwenye picha, tengeneza tray zenye plastic net kama za screen house halafu funika huo mstatiri. Chini kabisa kuwekwe plastic sheet nyeusi. Mstatiri uliofunikwa uwekewe madirisha madogo yaliyozibwa na screen net kuzuia wadudu na kupitisha mvuke.
 
View attachment 1348747
Hicho ni kikaushio cha kutumia mwanga wa jua. Nyanya inakatwa slices na kupangwa kwenye tray halafu inawekwa kwenye kikaushio kama hicho. Nanunua kipindi creti ni elfu 5, naanika kama creti 3 napata ndoo nzima ya nyanya kavu. Mwaka mzima hakuna kununua nyanya.
Hii nimeipenda,nahitaji elimu zaidi.
 
Kwa kuongezea pia unaweza kukausha mbogamboga kipindi cha mavuno na kuweka kwenye container ukatumia kwa mwaka. Waweza kukausha nyanya, vitunguu, tangawizi, tembele, majani ya kunde, n.k
Mkuu umenikumbusha huo mtambo wa kukaishia ninao na unatumia mkaa kidogo sana, tatizo kile kipima joto cha mercury kimevunjika sababu inabidi kikae ndani.
Ningepata kile haya mabadiliko ya bei yasingeniathiri mfukoni. Kariakoo wanauza digital
 
Mkuu umenikumbusha huo mtambo wa kukaishia ninao na unatumia mkaa kidogo sana, tatizo kile kipima joto cha mercury kimevunjika sababu inabidi kikae ndani.
Ningepata kile haya mabadiliko ya bei yasingeniathiri mfukoni. Kariakoo wanauza digital
Vya digital viko mtaa gani na ni bei gani ndugu.
 
Vya digital viko mtaa gani na ni bei gani ndugu.
Vipo vingi yale maduka ukifika pale round about shule ya uhuru uwe unaenda mnazi mmoja hamia upande wa kulia tembea upande huo kuna yale maduka unaingia ndani kama mall ndogo hivi. Ni maduka yanauza vifaa vya hospitali ukienda mall moja ukiulizia tu vifaa vya hospital utayapata yote. Yangu mimi walisema ni 15,000/= hawakuwa nayo. Za digital bei itakuwa chini sababu ziko aina nyingi.
 
Daah sawa mkuu,na taste yake itaendelea kua vile vile chief?

Maana mimi ndizi mbivu zikikaa kwny friji siku 3 tu,taste yake naona imepotea tayari.

dodge


Huko unaenda mbali..nyanya ilokaushwa kwa jua mie ilinishinda taste yake!mbaya mno mdomoni..sipatii picha hayo maaple!
 
Bei ya nyanya iko juu. Mtaani kwetu wameacha kabisa kuuza.

Wakina mama wapika mihogo nimeona sehemu wanatumia matango kama nyanya Ktk kachumbari.

Leo nimeshangaa pia eti bamia moja inauzwa 100 mtaani.
Vitunguu na mbogamboga poa ziko juu.

Sababu
Nimefuatilia sababu wanasema mvua zilizozidi ndio chanzo.

Utatuzi wa kudumu na ushauri

Ule utamaduni wa kupanda maua majumbani ubadilishwe Kwa kupanda mbogamboga.

Mfano ukipanda kaeneo kadogo matembere yatastawi hata ukimwagilia maji ya sabuni.

Panda mbogamboga, nyanya, Vitunguu, karoti Ktk makopo.


Hii itasaidia kupunguza gharama ndogondogo zinazoepukika.

Mkeo, housegirl, ndugu unaoishi nao, watoto wako au wewe mwenyewe badala ya kufanya jogging gym, au barabarani, au kuangalia movies kuhudumia bustani ya nyumbani hata nusu saa ni zoezi tosha Kwa wenye Muda.
Ila wale wanaoishi magorofani sijui itakuwaje kwa hii,au itabidi wapande mbogamboga kule summit au kwenye vibaraza vyao.....
 
Kwa kuongezea pia unaweza kukausha mbogamboga kipindi cha mavuno na kuweka kwenye container ukatumia kwa mwaka. Waweza kukausha nyanya, vitunguu, tangawizi, tembele, majani ya kunde, n.k

Hii mimi naiona kama fursa kipindi nyanya huwa nyingi mpaka zinaoza ni muhimu ziwe zinakaushwa kwa sasa nyanya moja Kitaani ni 400-500 very expensive aisee ni changamoto
 
Back
Top Bottom