The introvert
JF-Expert Member
- Sep 15, 2023
- 1,508
- 3,136
Habari za muda huu wajuzi wa mambo.
Sote tunajua ya kwamba teknolojia ndiyo kichocheo cha ukuaji wa kidijitali.
Kwa sasa nchi yetu ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya watumiaji wa intaneti hasa katika upande wa mitandao ya kijamii kwa miktadha mbalimbali.
Kumbukumbu zinaonesha kuwa kabla ya mwaka 2021 Tanzania ilikuwa ni miongoni mwa nchi zenye gharama nafuu zaidi kwenye vifurushi vya intaneti (TSh 1,000 kwa GB 1) .
Hivi ni kipi kilipelekea gharama za vifurushi kuongezeka kutoka gharama ya hapo juu mpaka kuwa TSh 3,000 kwa GB 1 na baadae baada ya lawama kadhaa kutoka kwa watumiaji kupunguzwa mpaka Tsh 2,100 kwa GB 1 ambayo tunatumia mpaka sasa. ? Hili ni swali la kwanza
Kwa sasa kumekuwa na malalamiko ya watumiaji wengi wa huduma ya intaneti kuwa vifurushi vinawahi kuisha kuliko kawaida na gharama za vifurushi vya intaneti bado viko juu kulinganisha na pato la mtumiaji mmoja (Hapa nazungumzia vijana na wafanyabiashara) ambao ndiyo wanabeba asilimia kubwa ya watumiaji wa intaneti.
Sikuhizi limekuwa ni jambo la kawaida kuweka GB 1 then baada ya muda mfupi
Salio kuisha (Wale wazee wa umetumia 75% ya bando lako 😂)
Je mamlaka husika (TCRA) na serikali kwa ujumla zina mpango gani juu ya swala hili kwani limekuwa likiumiza asilimia kubwa ya watumiaji wake (Nazungumzia gharama na uhalali wa vifurushi)