Kupanda Ligi Kuu kwa timu ya KenGold inadhihirisha kwamba Mbeya ni mkoa wa soka na Vipaji. Kwanini Serikali haijengi uwanja wa kisasa Mbeya?

Uwanja wa Kisiasa wa nini tena? Nchi imejaa wanasiasa... Tuanze tena kuwajengea na uwanja? Duh!!!

Bora ijenge tu uwanja wa mpira wa kisasa.
 
Pia tunaitaka pamba wana tp lindanda warudi kwenye ligi kuu, mwanza ilipoa sana kisoka, uwanja wa kirumba uchangamke tena. Kuna arusha na moshi zimepotea sana kisoka muda mrefu tangu zama za afc na ushirika nazo ziibuke tena
Mkuu Police Tz ilikuwa ya wapi?
 
Mkuu Police Tz ilikuwa ya wapi?
ilikuwa ya moshi na uwanja wao ulikuwa wa ushirika. Hiyo polisi ya moshi haikuleta shangwe kubwa kama ile ya wakati wa ushirika. Kumbuka pia polisi walikuwa na timu zao nyingi mikoani kama polisi kigoma, polisi mara, polisi singida zilishiriki mpaka ligi daraja la nne za mikoani kwao ziliko. Timu za majeshi hazina vibe kubwa kama timu zingine zisizo za majeshi. Timu za uraiani ndizo zenye mashabiki wengi kuliko za majeshi
 
Ni kweli kabisa, hili nililisema sana. Mikoa ambayo ingepewa kipaumbele katika ujenzi wa viwanja vipya ni Mbeya, Mwanza na Morogoro. Tungepata long-term return katika uwekezaji siyo tu kwa mapato lakini katika ukuaji wa vipaji. Uwanja wa Arusha utadoda na huo wa Dodoma unaenda kujengwa kisiasa. Viwanja vya Arusha na Dodoma ungefanyika ukarabati wa kawaida wa kuweka viti uwanja mzima kwa matumizi ya ligi za ndani ingetosha sana kwa sasa.

Labda kinachoikwamisha Morogoro ni kutokuwepo kiwanja cha ndege cha kisasa lakini kwa watu walio serious, wakati wa kufanya hivyo ungekuwa ni huu sambamba na kujenga uwanja.
 
Kosa la Mbeya ni kuichagua Chedema kwa iyo hawawezi kubet kuanzisha mradi mkubwa huku wakiwa hawana uhakika pengine wanaweza kutolewa. Angalia tu barabara ya Nsalaga mpaka Songwe imesainiwa toka mwaka jana wakisema mkandarasi ataanza sio muda chakushangaza mpaka leo hakuna kinachofanyika.

Siasa kila mahali. Mbeya instahili mengi sana
 
Serikal imebugi sana kuupeleka uwanja wa soka kwa wamaasai huko,bora wangeujenga mbeya,moro,au dom
Wamaasai na mpira wap na wap mikoa ya mbeya,iringa,songea huko kuna vipaji vingi sana kama uwanja ungejengwa hata mbeya basi ingekuwa chachu ya vijana kujituma katika soka na kupata ajira
 
Nafikiri tu wana tajiri la maana . Pesa!
Mengine mbwembwe
 
Acha kulalamika mtoa mada.Huo uwanja wa sokoine kwani ni msitu au bwawa kwamba mpira hauchezeki?Serikali haiwezi kufanya vitu vyote kwa wakati mmoja.
Hata kama Kuna vipaji lakini siyo sababu ya kuzumnguza kauli za kibaguzi na uchonganishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…