Kupanda na kuanguka kwa utawala wa tatu Ujerumani - The rise and fall of the third Reich

Kupanda na kuanguka kwa utawala wa tatu Ujerumani - The rise and fall of the third Reich

Paul Alex

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2012
Posts
4,351
Reaction score
9,838
Mwandishi William L. Shirer amefanya kazi ya kutukuka sana katika kitabu hiki.

Ni kitabu kirefu kidogo ila hebu fuatana na Mimi na nikuhakikishie, hautajua kimeishaje.. hisia na taarifa + mpangilio wa matukio vitakuacha kinywa wazi Kila wakati.

Fungeni mkanda watu wangu wa nguvu tuanze na msikwazike mara Moja Moja nikiwaomba vocha.

.......….........

Basi yalikua majigambo ya Hitler kuwa utawala huu utadumu kwa miaka elfu Moja.Ila badala yake ulidumu kwa miaka 12 tu. Japo ndani ya haya maisha mafupi ya utawala wa tatu yalijaa mnyororo wa matukio ya kutisha ambayo utaratibu wa maisha ya magharibu haukuwahi kuyaona.

William Shirer ni Moja kati ya wanahistoria wachache sana kupata fursa adhimu ya kupitia kumbukumbu za Siri za Ujerumani ambazo zilikamatwa na majeshi ya pamoja ya (Uingereza, Ufaransa, Marekani, n.k) zikiwa hazijaharibiwa. Alibahatika pia kuhudhuria muendelezo wa kesi zilizotokana na vita huko Nuremberg.

'Siwezi kufikiria kitabu kingine ambacho nitakiweka kwenye mikono ya yeyote ambaye anataka kufahamu Nini kilitokea Ujerumani kati ya mwaka 1930 na 1945, na kwanini historia ya miaka hiyo haipaswi kamwe kusahaulika'. - Alan Bullock Monumental.

'kina uzani mzuri, na wakati wote kina alama na uelewa wa mwandishi. Ni kitabu kizuri; kumbukumbu nzuri'.- Bernard Levin.

'Kitabu Cha viwango, na hakika historia sahihi ya u-nazi. Tunapaswa kuwa na shukrani kwa mwanahistoria ambaye kazi ngumu aliyofanya itatu za kumbukumbu za ukweli kwa muda wote'.- Hugh Trevor - Roper

Abiria funga mkanda, chopa inataka kupaa... Itaendelea!
 
SURA YA KWANZA.

KUZALIWA KWA UTAWALA WA TATU

Mwanzoni tu wa kuzaliwa kwa utawala wa tatu, homa ya mvutano iliikamata Berlin. Jamuhuri ya Weimar ilionekana wazi kwa karibu Kila mtu kuwa ilikuwa imefikia ukingoni. Kwa zaidi ya mwaka mzima ilikuwa ikianguka kwa haraka.

Jenerali Kurt von Schleicher, ambaye kama alivyokuwa mtangulizi wake, Franz von Papen, alijali kidogo sana kuhusu Jamuhuri na kidogo zaidi kwa demokrasia yake, na ambaye, kama tu mtangulizi wake, alitawala kama Kansela kwa amri za rais -presidential decree bila ridhaa ya bunge, alikuwa amefikia mwisho wa kamba yake baada ya siku 57 ndani ya ofisi. Jumamosi ya Januari 28, 1933, alisimamishwa ghafla na rais Mzee wa jamuhuri, Field Marshal von Hindenburg.

Adolf Hitler, kiongozi wa chama cha kijamaa- National Socialists, chama kikubwa zaidi Cha siasa Ujerumani, alitaka apewe u- Kansela wa jamuhuri ya kidemocrasia aliojiapiza kuitokomeza. Uvumi wa hatari ambayo ingeweza kujitokeza ulikuwa umejaa mji mkuu mwisho wa wiki hii muhimu ya majira ya bariidi, na uliotisha zaidi haukukosa ushahidi.

Kulikuwa na report kuwa Schleicher, kwa kushirikiana na Jenerali Kurt von Hammerstein, kamanda mkuu wa jeshi, walipangilia mapinduzi kwa msaada wa Potsdam garrison kwa malengo ya kumuweka rais chini ya ulinzi nakuanzisha utawala wa kidikteta chini ya jeshi.

Kulikuwa pia na uvumi wa mapinduzi ya wa-Nazi. Askari wa kuzuia ghasia Berlin, wakisaidiana na wafuasi wa wa-Nazi ndani ya polisi, walikia wavamie Wilhelmstrasse, ambapo ikulu ya rais na wizara nyingi za serikali zilikuwepo.

Kulikuwa na uvumi pia wa mgomo wa nchi nzima. Jumapili ya Januari 29, wafanyakazi laki Moja walikusanyika Lustgarten katika ya Berlin kuonyesha pingamizi lao la kumfanya Hitler Kansela. Moja ya viongozi wao alijaribu kuwasiliana na Jenerali von Hammerstein kupendekeza nguvu ya pamoja kati ya jeshi na wafanyakazi kama Hitler angetangazwa kuongoza serikali mpya. Kipindi Cha nyuma katika mapinduzi ya Kapp 1920, mgomo wa watu wote ulisaidia kuokoa jamuhuri wakati serikali ilipikimbia mji mkuu.

Karibu usiku mzima wa jumapili kuamkia jumatatu Hitler alikuwa akipanda na kushuka katika chumba chale katika hoteli ya Kaiserhof huko Reichskanzlerplatz, mtaa mmoja tu Toka ilipo Chancellery. Pamoja na shauku aliyokuwa nayo alikuwa na hakika kuwa saa yake imewadia. Kwa karibu mwezi mzima amekuwa kwa Siri aki...

....Mambo yanaanza mdogo mdogo... Tutaendelea
 
Mwandishi William L. Shirer amefanya kazi ya kutukuka sana katika kitabu hiki.

Ni kitabu kirefu kidogo ila hebu fuatana na Mimi na nikuhakikishie, hautajua kimeishaje.. hisia na taarifa + mpangilio wa matukio vitakuacha kinywa wazi Kila wakati.

Fungeni mkanda watu wangu wa nguvu tuanze na msikwazike mara Moja Moja nikiwaomba vocha.

.......….........

Basi yalikua majigambo ya Hitler kuwa utawala huu utadumu kwa miaka elfu Moja.Ila badala yake ulidumu kwa miaka 12 tu. Japo ndani ya haya maisha mafupi ya utawala wa tatu yalijaa mnyororo wa matukio ya kutisha ambayo utaratibu wa maisha ya magharibu haukuwahi kuyaona.

William Shirer ni Moja kati ya wanahistoria wachache sana kupata fursa adhimu ya kupitia kumbukumbu za Siri za Ujerumani ambazo zilikamatwa na majeshi ya pamoja ya (Uingereza, Ufaransa, Marekani, n.k) zikiwa hazijaharibiwa. Alibahatika pia kuhudhuria muendelezo wa kesi zilizotokana na vita huko Nuremberg.

'Siwezi kufikiria kitabu kingine ambacho nitakiweka kwenye mikono ya yeyote ambaye anataka kufahamu Nini kilitokea Ujerumani kati ya mwaka 1930 na 1945, na kwanini historia ya miaka hiyo haipaswi kamwe kusahaulika'. - Alan Bullock Monumental.

'kina uzani mzuri, na wakati wote kina alama na uelewa wa mwandishi. Ni kitabu kizuri; kumbukumbu nzuri'.- Bernard Levin.

'Kitabu Cha viwango, na hakika historia sahihi ya u-nazi. Tunapaswa kuwa na shukrani kwa mwanahistoria ambaye kazi ngumu aliyofanya itatu za kumbukumbu za ukweli kwa muda wote'.- Hugh Trevor - Roper

Abiria funga mkanda, chopa inataka kupaa... Itaendelea!
Paul...
Marhaba....

Ahsante sana kwa kututia darasani.
Unasema tunataka kupaa?

Mbona tayari ushatutia mawinguni?

Nilimuuliza Kai Kresse wa Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin hii ni taasisi kubwa sana ya utafiti wa historia Ujerumani wanajisikiaje wanaposomesha historia ya Nazi Germany.

"Inafadhaisha lakini lazima isomeshwe ili wananchi waijue tusije kurudia makosa.",

Alinialika ZMO kwa kufanya mhadhara, kutafiti na kuandika chochote nipendacho.

ZMO ipo kwenye jengo ambalo lilikuwa makao ya Gestapo.
Katika jengo hili nilipewa ofisi moja nitumie wakati nikiwa hapo.

Nilifika Potsdam.
Si mbali na ZMO .

Nakuwekea picha ya kitabu kurasa 1436 unakiona kimechoka hata mbele jalada halipo nilifanya ''binding.''.

Kitabu hiki nimekisoma labda miaka 40 iliyopita enzi hizo nakunywa kurasa hizo kama juisi bila kusinzia.

Ujana una raha zake.
Vijana tumieni vyema ujana wenu msije mkajuta.

Tupige goti hapa kwa Alex tusome bila jasho.
Tumshukuru sana Alex kwa hisani hii.
 
Mwandishi William L. Shirer amefanya kazi ya kutukuka sana katika kitabu hiki.

Ni kitabu kirefu kidogo ila hebu fuatana na Mimi na nikuhakikishie, hautajua kimeishaje.. hisia na taarifa + mpangilio wa matukio vitakuacha kinywa wazi Kila wakati.

Fungeni mkanda watu wangu wa nguvu tuanze na msikwazike mara Moja Moja nikiwaomba vocha.

.......….........

Basi yalikua majigambo ya Hitler kuwa utawala huu utadumu kwa miaka elfu Moja.Ila badala yake ulidumu kwa miaka 12 tu. Japo ndani ya haya maisha mafupi ya utawala wa tatu yalijaa mnyororo wa matukio ya kutisha ambayo utaratibu wa maisha ya magharibu haukuwahi kuyaona.

William Shirer ni Moja kati ya wanahistoria wachache sana kupata fursa adhimu ya kupitia kumbukumbu za Siri za Ujerumani ambazo zilikamatwa na majeshi ya pamoja ya (Uingereza, Ufaransa, Marekani, n.k) zikiwa hazijaharibiwa. Alibahatika pia kuhudhuria muendelezo wa kesi zilizotokana na vita huko Nuremberg.

'Siwezi kufikiria kitabu kingine ambacho nitakiweka kwenye mikono ya yeyote ambaye anataka kufahamu Nini kilitokea Ujerumani kati ya mwaka 1930 na 1945, na kwanini historia ya miaka hiyo haipaswi kamwe kusahaulika'. - Alan Bullock Monumental.

'kina uzani mzuri, na wakati wote kina alama na uelewa wa mwandishi. Ni kitabu kizuri; kumbukumbu nzuri'.- Bernard Levin.

'Kitabu Cha viwango, na hakika historia sahihi ya u-nazi. Tunapaswa kuwa na shukrani kwa mwanahistoria ambaye kazi ngumu aliyofanya itatu za kumbukumbu za ukweli kwa muda wote'.- Hugh Trevor - Roper

Abiria funga mkanda, chopa inataka kupaa... Itaendelea!
Paul...
Marhaba....

Ahsante sana kwa kututia darasani.

Unasema tunataka kupaa?

Mbona tayari ushatutia mawinguni?

Nilimuuliza Kai Kresse wa Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin hii ni taasisi kubwa sana ya utafiti wa historia Ujerumani wanajisikiaje wanaposomesha historia ya Nazi Germany.

"Inafadhaisha lakini lazima isomeshwe ili wananchi waijue tusije kurudia makosa."

Alinialika ZMO kwa kufanya mhadhara, kutafiti na kuandika chochote nipendacho.

ZMO ipo kwenye jengo ambalo lilikuwa makao ya Gestapo.

Katika jengo hili nilipewa ofisi moja nitumie wakati nikiwa hapo.

Nilifika Potsdam.
Si mbali na ZMO.

Nakuwekea picha ya kitabu kurasa 1436 unakiona kimechoka jalada la mbele halipo nimefanya ''binding..

Kitabu hiki nimekisoma labda miaka 40 iliyopita nakunywa kurasa hizo kama juisi bila kusinzia.

Ujana una raha zake.
Vijana tumieni vyema ujana wenu kujielimisha msije mkajuta.

Tupige goti hapa kwa Alex tusome bila jasho.
Tumshukuru sana kwa hisani hii.

1683295954909.jpeg
 
Inaendelea...

akijaribu kuafikiana na Papen na viongozi wengine wa chama cha kihafidhina mrengo wa kulia. Kuna mambo alipaswa kukubaliana nayo. Asingeweza kuaimamisha serikali tupu ya ki- Nazi. Ila angeweza kuwa Kansela wa serikali ya muungano ambayo wajumbe wake, nane kati Yao ambao hawakuwa wa wa-Nazi, walikubaliana kuitokomeza utawala wa kidemocrasia wa Weimar. Ni rais Mzee tu na aliyekuwa hana mashiko aliyeonekana kuzuia njia yake. Karibuni tu kama Januari 26, siku mbili kabla la tukio hili muhimu la mwisho wa wiki, huyu field Marshal Mzee alikuwa amemwambia Jenerali von Hammerstein kuwa hakuwa na nia hata chembe ya kumfanya huyu koplo wa Austria waziri Wala hata Kansela wa utawala huo. Ila chini ya ushawishi wa mwanae, Meja Oskar von Hindenburg na Otto von Meissner, katibu mkuu wa serikali, Papen na wajumbe wengine wa makazi ya rais, Camarilla, rais hatimaye alipoteza nguvu. Alikuwa na umri wa miaka 86 na uwezo wake wa kumbukumbu ulishapungua sana.

Mchana wa jumapili ya Januari 29, wakati Hitler akipata kahawa na keki pamoja na Goebbels na wasaidizi wengine, Hermann Goering, Rais wa bunge - Reichstag na wapili ukiacha Hitler kwenye chama cha Nazi aliingia ghafla na kuwajulisha kuwa ni rasmi kuwa kesho yake Hitler angeteuliwa kama Kansela. Muda mfupi kabla ya saa sita mchana siku ya jumatatu, Januari 30, 1933, Hitler akaendesha gari yake kuelekea ofisi za Kansela kwa mahojiano na Hindenburg ambayo baadae yaligeuka balaa kwake mwenyewe na kwa Dunia nzima. Kutokea dirisha la hoteli ya Kaiserhof, Goebbels, Roehm na viongozi wengine wa Nazi walichungulia kwenye malango ya ofisi za Kansela kwa shauku, ambapo Kansela mpya alitegemewa kutoka nje muda sio mrefu.
"Tungeona tu kwenye uso wake ikiwa amefanikiwa au la!", Goebbels aliandika kwenye kumbukumbu zake. Kwasababu, hata mpaka hapo hawakuwa na uhakika Moja kwa Moja. " Mioyo yetu iliraruliwa huku na kule kati ya wasiwasi, matumaini, furaha na mkato wa tamaa," Goebbels aliandika kwenye kumbukumbu zake. " Tumevunjwa moyo mara nyingi sana kiasi Cha kushindwa kuamini Moja kwa Moja kwenye muujiza huu mkubwa". Muda kidogo baadae walishuhudia huo muujiza. Mtu mwenye mustachi kama mchekeshaji Charlie Chaplin ambaye alikuwa wa daraja la chini na kama uchafu huko Vienna katika ujana wake, askari asiyefahamika wa vita kuu ya kwanza ya Dunia - WWI, mtu aliyejikatia tamaa huko Munich katika siku za giza zilizofuatia vita, kiongozi Fulani wa masihara aliyeongoza mapinduzi ya ukumbi wa bia yaliyoshindwa, huyu mbahatishaji ambaye hakuwa hata mjerumani bali mu-Austria , na aliyekuwa na miaka 43 tu, alikuwa ametoka kula kiapo Cha kuwa Kansela wa utawala wa Ujerumani. Akaendesha gari yadi mia Moja kuelekea Kaiserhof na punde akawa na washkaji zake wa zamani, Goebbels, Goering, Roehm na wa-Nazi wengine ambao walimsaidia katika njia ya majabali na mapambano kuelekea madaraka.

"Hakusema chochote, na sisi wote hatukusema chochote", Goebbels aliandika "Ila macho yake yalijaa machozi". Jioni hiyo kuanzia giza lilipozama mpaka baada ya saa sita usiku watuliza ghasia wa kinazi waliokuwa na hamasa walipiga parade wakiwa tochi zinazowaka kusherehekea ushindi. Kwa makumi ya maelfu, walitokea kwenye mistari iliyonyooka kutoka katikati ya Tiergarten, wakapita kwenye upinde wa ushindi wa geti la Brandenburg na kuelekea Wilhelmstrasse, bendi zao zikipuliza 'martial airs' za zamani na ngoma zilizotoa sauti ya radi, sauti zao zikiimba nyimbo mpya ya Horst Wessel tuni nyingine za zamani kabisa Ujerumani. Mabuti yao yakipiga mshindo mzito kwenye pavement,

Inaendelea.....
 
Paul...
Marhaba....

Ahsante sana kwa kututia darasani.

Unasema tunataka kupaa?

Mbona tayari ushatutia mawinguni?

Nilimuuliza Kai Kresse wa Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin hii ni taasisi kubwa sana ya utafiti wa historia Ujerumani wanajisikiaje wanaposomesha historia ya Nazi Germany.

"Inafadhaisha lakini lazima isomeshwe ili wananchi waijue tusije kurudia makosa."

Alinialika ZMO kwa kufanya mhadhara, kutafiti na kuandika chochote nipendacho.

ZMO ipo kwenye jengo ambalo lilikuwa makao ya Gestapo.

Katika jengo hili nilipewa ofisi moja nitumie wakati nikiwa hapo.

Nilifika Potsdam.
Si mbali na ZMO.

Nakuwekea picha ya kitabu kurasa 1436 unakiona kimechoka jalada la mbele halipo nimefanya ''binding..

Kitabu hiki nimekisoma labda miaka 40 iliyopita nakunywa kurasa hizo kama juisi bila kusinzia.

Ujana una raha zake.
Vijana tumieni vyema ujana wenu kujielimisha msije mkajuta.

Tupige goti hapa kwa Alex tusome bila jasho.
Tumshukuru sana kwa hisani hii.

Basi tulia ili tupate historia toka kwa Paul Alex
 
Nilikuwa porini kwa muda ila nimerudi na Niko poa!
Samahani kwa usumbufu uliojitokeza..
Naomba tuendelee
 
Tuendelee....

tochi zao zilizonyanyuliwa juu na kuunda mzunguko wa miale ya mwanga iliyomulika usiku huo na kusababisha shangwe za watazamaji waliojazana pembeni ya Barabara. Kutokea kwenye dirisha la Ikulu, Hindenburg alitazama chini kuangalia parade hii, kwa muda akifarijika kuwa angalau ameteua Kansela ambaye anakubalika na wajerumani kama ilivyo kwa desturi za Kijerumani.

Ikiwa huyu Mzee, katika fikra zake alijua chochote juu ya dhahama iliyoianzisha, inatia wasiwasi. Habari ambayo haikuwa ya uhakika sana haraka ilisambaa Berlin kwamba katikati ya parade alimgeukia Jenerali mmoja Mzee na kusema." Sikujua kama tumechukua mateka wengi hivi wa Urusi".

Umbali wa kurusha jiwe la mkono kutoka Wilhelmstrasse, Adolf Hitler alisimama katika dirisha lililo wazi ndani ya ofisi za Kansela, akiwa peke yake, mwenye furaha sana, akirukaruka kwa furaha, Kila mara akinyoosha mkono wake akitoa salute ya ki-Nazi, akitabasamu na kucheka mpaka macho yake yalipojaa tena machozi.

Mtazamaji mmoja mgeni aliangalia matukio yaliyokuwa yakiendelea usiku huu huku akiwa na hisia tofauti kabisa. "Mto wa moto ulitiririka Kando ya ubalozi wa Ufaransa", Andre Fran, coisPoncet, balozi aliandika, " nikiwa na moyo mzito na mashaka ya yajayo mbele, nilitazama mwangaza wa mwanzo wake". Akiwa amechoka ila mwenye furaha, Goebbels alifika nyumbani kwake saa tisa usiku na kuandika kwenye diary yake kabla ya kulala: " Ni kama vile ndoto... simulizi zuri ... Utawala mpya umezaliwa. Miaka 14 ya kazi imevikwa taji la ushindi. Mapinduzi ya Ujerumani yameanza!" Utawala huu watatu uliozaliwa Januari 30, 1933, Hitler alitamba, ungedumu kwa miaka elfu Moja, na kwa kauli za wa-Nazi uliitwa "Utawala wa miaka Elfu Moja". Ulidumu kwa miaka 12 na miezi minne, ila kwa muda huu mdogo, kama historia inavyojieleza, ulisababisha mlipuko katika hii Dunia wa kikatili na uharibifu zaidi kuwahi kutokea, ukiwanyanyua watu wa Ujerumani katika ukubwa wa nguvu za madaraka ambazo hawakuwa kufahamu zaidi ya milenia nyuma, ukiwafanya katika wakati mmoja watawala wa Ulaya kutokea Atlantic mpaka Volga, kutoka Cape ya kaskazini mpaka Mediterranean, na Kisha kuwatumbukiza katika kina Cha uharibifu na kutengwa baada ya vita kuu ya Dunia ambayo taifa lao liliianzisha kwa makusudi na katika kipindi ambacho liliasisi utawala wa kigaidi juu ya mataifa yaliyotawaliwa na Ujerumani ambayo kwa hesabu za mauaji ya maisha na mioyo ya watu, yalizidi kwa mbali mateso yote ya miaka yote iliyopita duniani yakijumlishwa kwa pamoja!

Mtu aliyeuasisi utawala huu watatu, aliyeuongoza kwa mkono wa chuma na mara nyingi kwa ubinafsi usiokua wa kawaida, na aliyeupeleka kwenye ukubwa wa mamlaka usiomithilika na baadae kwenye mwisho unaotia huruma, alikuwa ni mtu mwenye weledi wa juu kabisa wa uovu usiokuwa na mashaka.

Ni kweli kwamba, alipata katika wajerumani, ambao walikua wameandaliwa na matukio ya miaka ya nyuma, silaha ambayo aliweza kuitumia kwa malengo yake maovu. Ila kwa Adolf Hitler, aliyekuwa amevamiwa na nafsi ya kishetani, nia thabiti, hisia zisizoyumba, mkono wa chuma, weledi wa kupigiwa mfano, mtazamo mchungu, na mpaka karibu na mwisho, wakati amelewa madaraka na mafanikio, alijipatia mwenyewe - uwezo wa kushangaza wa kutawala watu na matukio; bila ambavyo kusingekuwa kamwe na utawala watatu. " Ni Moja kati ya mifano maarufu", kama ambavyo Friedrich Meinecke, mwanahistoria maarufu wa Kijerumani, alisema, " juu ya nguvu za nafsi moja zisizomithilika katika maisha ya kihistoria".

Kwa baadhi ya wajerumani na, bila wasiwasi, kwa wageni wengi ilionekana kama tapele wa kisiasa amekuwa kiongozi wa Berlin. Kwa wajerumani walio wengi, Hitler alikuwa amepata- au angepata katika muda mfupi - kukubalika kama kiongozi mwenye Karisma ya kweli. Na walimfuata kikipofu, kama vile alikuwa na maamuzi matakatifu, kwa miaka 12 iliyojaa Kila aina ya makwazo.

Inaendelea.....
 
Chopa itembee....

MWANZO WA ADOLF HITLER.

Ukizingatia asili yake na maisha yake ya mwanzo, Inakuwa ngumu kudhania mtu mwingine asiyefanania kurithi dhana ya Bismark, watawala wa Hohenzollern na rais Hindenburg kuliko huyu mu-Austria mmoja wa jamii ya daraja la chini la wafanyakazi wa mashambani aliyezaliwa saa kumi na mbili na nusu jioni ya April 20, 1889, huko Gasthof Zum Pommer, nyumba ya kawaida ya wageni katika mji wa Braunau am Inn, karibu na mpaka wa Bavaria. Sehemu ya kuzaliwa katikati ya eneo lenye mvutano kati ya Austria na Ujerumani ilikuja kuwa na maana kubwa, kwakuwa mapema katika maisha yake, akiwa kijana wa kawaida, Hitler alitatizwa na wazo kwamba hakukupaswa kuwa na mpaka katikati ya hizi jamuhuri mbili zinazozungumza lugha ya Kijerumani, na kuwa zote zinapaswa kuwa chini ya utawala mmoja.

Hisia zake zilikuwa na nguvu na zilidumu kiasi kwamba akiwa na miaka 35, ndani ya magereza Ujerumani aliandika kitabu ambacho kilikuja kuwa mwongozo wa utawala wa tatu. Mistari yake ya mwanzo kabisa ilijikita kwenye umuhimu wa kiishara wa sehemu yake ya kuzaliwa. Mein Kampf - (Mapambano yangu) ni kitabu kilichoanza na maneno haya : Leo ninaona kuwa nimependelewa kwa hatma kuchagua Braunau am Inn kama sehemu yangu ya kuzaliwa. Kwakuwa mji huu mdogo uko mpakani mwa jamuhuri mbili za Kijerumani ambao sisi wa kizazi kipya angalau tumeifanya kuwa kazi ya maisha yetu kuziunganisha kwa namna yoyote Ile iliyo mbele yetu... Mji huu mdogo mpakani unaonekana kwangu kama ishara ya mkakati mkubwa.

Adolf Hitler alikua mtoto wa tatu wa kiume katika ndoa ya tatu ya mfanyakazi wa kawaida wa Custom aliyezaa mtoto asiye halali na ambaye katika miaka 39 ya mwanzo alitumia jina la upande wa mama yake, Schicklgeuber. Jina la Hitler linajitokeza upande wa mama na pia kwa upande wa baba. Bibi zake Hitler wote kwa upande wa mama na Babu yake kwa upande wa baba waliotwa Hitler, au majina mengine yanayofanania, kwakuwa jina la familia liliandikwa mara kadhaa kama Hiedler, Huetler, Huettler, na Hitler.

Mama yake na Adolf alikuwa binamu wa pili wa baba yake, na ruhusa maalum ya kanisa ilihitajika kwaajili ya ndoa. Watangulizi wa mtawala wa Ujerumani ajaye waliishi vizazi na vizazi huko Waldviertel, wilaya iliyo Austria ya chini kati ya Danube na mpaka wa Bohemia na Moravia.

Katika siku ambazo niliishi Vienna (mwandishi) wakati mwingine nilipita hapo kuelekea Prague au Ujerumani. Ni nchi ya milima na misitu yenye vijiji vya wakulima na mashamba madogo, na japo ilikuwa mile 50 kutoka Vienna, inaonekana kutengwa na kuwa masikini, kama vile mawimbi ya maisha ya Austria yameipita Kando. Wakazi wake wanaonekana kupooza kama tu wakulima wa Czech kaskazini kidogo na wao. Kuoana ndani ya familia ni kawaida, kama ilivyokuwa kwa wazazi wa Hitler, na watoto wasio halali ni wa mara kwa mara.

Kwa upande wa mama kulikuwa na msimamo kiasi. Kwa vizazi vinne familia ya Klara Poelzl ilibaki kwenye makazi ya wakulima namba 37 katika Kijiji Cha Spital. Historia ya watangulizi wa wazazi wa Hitler ni tofauti kabisa. Matamshi ya jina la familia yanabadilika kama tulivyoona; sehemu ya makazi pia. Kuna roho ya kutotulia katika kina Hitler, msukumo wa kuhama kutoka Kijiji kimoja kwenda kingine, kutoka kazi Moja kwenda nyingine, kuepusha mifungamano na watu wengine na kufuata aina Fulani ya maisha ya ki-Bohemia katika mahusiano na wanawake. Johann Georg Hiedler, Babu wa Adolf, alikuwa ni mtu aliyejihusisha na usagaji wa nafaka, akifanya shughulizake Kijiji kimoja kwenda kingine huko Austria ya chini.

Inaendelea...
 
Back
Top Bottom