Tuendelee...
"KIPINDI CHA HUZUNI ZAIDI KATIKA MAISHA YANGU"
Miaka minne iliyofuata, kati ya mwaka 1909 na mwaka 1913, iligeuka kuwa miaka ya mateso makali na unyonge kwa huyu kijana mpambanaji kutoka Linz. Katika miaka hii ya mwisho kabla ya kuanguka kwa Hapsburgs na ukomo wa hili jiji kama makao makuu ya himaya ya watu millioni 52 katikati ya Ulaya, Vienna ilikuwa na muonekano na uchangamfu uliokuwa tofauti sana na miji mikuu mingine ulimwenguni.
Sio tu uhandisi wake, ila sanamu zake, muziki wake, ila katika mioyo mikunjufu na inayopenda starehe ya watu wake ambayo ilotoa muonekano ambao hakuna jiji lingine la magharibi lilitambua.
Ikiwa kandokando ya Danube ya blue na chini ya vilima vyenye misitu vya Wienerwald, vilivyopendezeshwa na miti ya matunda ya njano na kijani, Ilikuwa sehemu ya uzuri wa asili uliowavutia wageni na kufanya watu wa Vienna waamini kwamba uumbaji umewapendelea kwa namna ya kipekee sana. Muziki ulitanda kwenye hewa, muziki mkubwa wa nyimbo za asili za vipaji, wanamuziki wakubwa kuwahi kutokea Ulaya, Haydn, Mozart, Beethoven na Schubert, na, katika miaka ya mwisho ya majira ya joto ya India, mwanamziki shoga kipenzi cha Vienna, Johann Strauss.
Kwa watu waliobarikiwa hivi, na ambao walikuwa na chapa ya maisha ya starehe, maisha yenyewe yalikuwa Kama ndoto na watu wazuri wa jiji hili walimaliza siku zao nzuri mchana na usiku wakifurahia muziki na mvinyo, au katika mazungumzo ya hapa na pale katika migahawa ya kahawa, wakisikiliza miziki na kutazama sinema na maigizo, au katika kutomasana na kufanya mapenzi, wakitumia muda mwingi katika maisha yao kwenye starehe na ndoto.
Ili kuwa na hakika, hii himaya ilipaswa kuongozwa, jeshi la ardhi na jeshi la maji walisimamia, mawasiliano yalitunzwa, biashara ziliendelea na kazi zilifanyika. Ila ni wachache tu ndani ya Vienna waliofanya kazi masaa ya ziada - au hata masaa kamili yanayohitajika kazini - katika mambo hayo.
Kulikuwa na upande mwingine wa shilingi bila shaka. Hili jiji, Kama tu majiji mengine yote, lilikuwa na masikini wake : waliokosa mlo kamili, waliokuwa na mavazi makuukuu na walioishi sehemu za hovyo. Ila Kama mji mkubwa wa viwanda katika ulaya ya kati na pia Kama makao makuu ya himaya, Vienna ilikuwa na maendeleo, na haya maendeleo yalisambaa katikati ya watu na kuteremka chini. Wengi kati ya wale wa daraja la chini la kati walishikilia jiji katika siasa; wafanyakazi waliendesha sio tu vyama vya wafanyakazi ila pia chama chenye nguvu cha siasa cha aina yake, "The Social Democrats".
Kulikuwa na mabadiliko katika maisha ya jiji, ambalo Sasa wakazi wake walifikia watu milioni mbili. Demokrasia ilikuwa ikiondoa utawala wa kizamani wa kiimla wa Hapsburgs, elimu na utamaduni vikifunguka kwa kwa walio wengi hivyo kwamba wakati Hitler alipokuja Vienna mwaka 1909 kulikuwa na fursa kwa kijana huyu asiyekuwa na shilingi kupata elimu ya juu au kupata maisha mazuri tu ya kawaida, kama moja kati ya millioni wanaoingiza mshahara, kuishi katika maisha ya kiungwana ambayo makao haya makuu yaliwapatia watu wake.
Si hata rafiki yake wa pekee, Kubizek, masikini na aliyekosa fursa Kama yeye, tayari alikuwa akijijengea jina katika Academy ya muziki! Ila kijana Adolf hukufuatilia matamaanio yake ya kujiunga na shule ya uhandisi. Ilikuwa iko wazi kwake pamoja na kukosa diploma ya elimu ya juu. Vijana walioonyesha kipaji cha tofauti waliandikishwa bila hicho cheti - ila kwa jinsi inavyofahamika mpaka sasa hakufanya maombi hayo. Wala hakuhamasika kujifunza fani au kuomba ajira yoyote ya kudumu. Ila alipendelea kufanya kazi ngumu Kama: Kupiga chepe kuondoa barafu, kuosha makapeti, kubeba mabege nje ya kituo cha reli cha magharibi, mara kadhaa kwa siku chache akifanya kazi kama 'saidia fundi' kwenye ujenzi.
Inaendelea....