Paul Alex
JF-Expert Member
- Jul 14, 2012
- 4,351
- 9,838
- Thread starter
- #21
Tuendelee...
Miezi mitano baada ya ndoa yake ya kwanza, mwaka 1824, mtoto wa kiume alizaliwa, ila mtoto na mama hawakuishi. Miaka 18 baadae, akifanyakazi huko Duerenthal, alimuoa mwanamke mkulima wa miaka 47 kutoka Kijiji Cha Strones, Maria Anna Schicklgruber. Miaka mitano kabla ya ndoa, June 7, 1837, Maria akipata mtoto asiye halali aliyemuita Alois na ndiye aliyekuja kuwa baba wa Adolf Hitler. Inawezekana sana kwamba baba wa Alois alikuwa Johann Hiedler, ila ushahidi wa uhakika umekosekana. Kwa hesabu zozote zile, hatimaye Johann alimuoa huyo mwanamke, ila kinyume na Mila zilizozoeleka katika suala kama Hilo, hakujisumbua na kumhalalisha mtoto baada ya ndoa.Mtoto alikuwa akiitwa Alois Schicklgruber.
Anna alifariki mwaka 1847, wakati ambao Johann Hiedler alitokomea kwa miaka 30, na kuja kujitokeza akiwa na miaka 84 katika mji wa Weitra huko Waldviertel, ambapo Sasa jina lake lilitamkwa kama Hitler, na kutoa ushahidi mbele ya hakimu, wakiwepo na mashahidi watatu kuwa yeye ndiye baba wa Alois Schicklgruber.
Kwanini huyu Mzee alisubiri muda mrefu hivyo kuchukua hii hatua, au kwanini baadae aliichukua, haikufahamika kwa kumbukumbu zilizopo. Kama alivyosema Heiden, Alois baadae akitoa Siri kwa rafiki yake kwamba ilifanyika kumsaidia kupata sehemu ya urithi kutoka kwa mjomba wake, kaka wa akina Miller, aliyemlea akiwa mdogo kwenye familia yake.
Kwa makadirio yoyote Yale, utambulisho huu wa mashaka ulifanyika June 6, 1876, na November 23, paroko wa Doellersheim, ambaye ofisi yake ilitumiwa nakala ya kiapo, alilifuta jina la Alois Schicklgruber kwenye Cheti Cha ubatizo na kuandika jina la Alois Hitler. Kuanzia muda huo kwenda mbele baba yake Adolf alitambulika kisheria kama Alois Hitler, na kwa utaratibu wa kawaida kijana wake akalirithi.
Ilikuwa mpaka miaka ya 1930 ambapo mwanahabari aliyechipukia huko Vienna, akipitia kumbukumbu za makabrasha ya parokia, aligundua ukweli juu ya watangulizi wa Hitler, juu ya jitihada za Mzee Johann Georg Hiedler za kifanya lililo sahihi kwa mtoto wake huyu wa haramu, na kujitahidi kumshupalia huyu kiongozi wa wa-Nazi jina la Adolf Schicklgruber.
Kuna mabasiliko mengi ya ajabu kwenye hatma ya maisha ya kushangaza ya Adolf Hitler, ila hakuna linaloshangaza kama hili lililotokea miaka 13 kabla ya kuzaliwa kwake. Kama huyu mzururaji Miller (miaka 84) asingejitokeza kujitambulisha kama baba kwa kijana wake (miaka 39) karibu miaka 30 baada ya kifo Cha mama yake, Adolf Hitler angezaliwa kama Adolf Schicklgruber. Panaweza pasiwe na jambo kubwa kwenye jina, ila nimewasikia wajerumani (mwandishi) wakibashiri kama Hitler angekuwa mtawala wa Ujerumani kama angejulikana ulimwenguni kama Schicklgruber. Inaleta sauti flani hivi ya vichekesho kama likitamkwa na mtu kutoka Ujerumani ya kusini.
Mtu anawezaje kudhania umma wa wajerumani uliohamasika ukimshangilia Schicklgruber kwa mshindo wa sauti zao "Heils"? "Heil Schicklgruber!"?
Sio tu kama "Heil Hitler!" ilitumika kama shangwe ya kipagani na umma katika mikusanyiko ya wa - Nazi, bali ilikuja kuwa salamu ya lazma kati ya wajerumani kwenye utawala wa tatu, hata kwenye simu ambapo ilichukua nafasi ya salamu "Hello". "Heil Schicklgruber!"? Ni ngumu kidogo kumeza.
Itaendelea.... tuwe pamoja