Kupanda na kuanguka kwa utawala wa tatu Ujerumani - The rise and fall of the third Reich

Kupanda na kuanguka kwa utawala wa tatu Ujerumani - The rise and fall of the third Reich

Tuendelee...

Miezi mitano baada ya ndoa yake ya kwanza, mwaka 1824, mtoto wa kiume alizaliwa, ila mtoto na mama hawakuishi. Miaka 18 baadae, akifanyakazi huko Duerenthal, alimuoa mwanamke mkulima wa miaka 47 kutoka Kijiji Cha Strones, Maria Anna Schicklgruber. Miaka mitano kabla ya ndoa, June 7, 1837, Maria akipata mtoto asiye halali aliyemuita Alois na ndiye aliyekuja kuwa baba wa Adolf Hitler. Inawezekana sana kwamba baba wa Alois alikuwa Johann Hiedler, ila ushahidi wa uhakika umekosekana. Kwa hesabu zozote zile, hatimaye Johann alimuoa huyo mwanamke, ila kinyume na Mila zilizozoeleka katika suala kama Hilo, hakujisumbua na kumhalalisha mtoto baada ya ndoa.Mtoto alikuwa akiitwa Alois Schicklgruber.

Anna alifariki mwaka 1847, wakati ambao Johann Hiedler alitokomea kwa miaka 30, na kuja kujitokeza akiwa na miaka 84 katika mji wa Weitra huko Waldviertel, ambapo Sasa jina lake lilitamkwa kama Hitler, na kutoa ushahidi mbele ya hakimu, wakiwepo na mashahidi watatu kuwa yeye ndiye baba wa Alois Schicklgruber.

Kwanini huyu Mzee alisubiri muda mrefu hivyo kuchukua hii hatua, au kwanini baadae aliichukua, haikufahamika kwa kumbukumbu zilizopo. Kama alivyosema Heiden, Alois baadae akitoa Siri kwa rafiki yake kwamba ilifanyika kumsaidia kupata sehemu ya urithi kutoka kwa mjomba wake, kaka wa akina Miller, aliyemlea akiwa mdogo kwenye familia yake.

Kwa makadirio yoyote Yale, utambulisho huu wa mashaka ulifanyika June 6, 1876, na November 23, paroko wa Doellersheim, ambaye ofisi yake ilitumiwa nakala ya kiapo, alilifuta jina la Alois Schicklgruber kwenye Cheti Cha ubatizo na kuandika jina la Alois Hitler. Kuanzia muda huo kwenda mbele baba yake Adolf alitambulika kisheria kama Alois Hitler, na kwa utaratibu wa kawaida kijana wake akalirithi.

Ilikuwa mpaka miaka ya 1930 ambapo mwanahabari aliyechipukia huko Vienna, akipitia kumbukumbu za makabrasha ya parokia, aligundua ukweli juu ya watangulizi wa Hitler, juu ya jitihada za Mzee Johann Georg Hiedler za kifanya lililo sahihi kwa mtoto wake huyu wa haramu, na kujitahidi kumshupalia huyu kiongozi wa wa-Nazi jina la Adolf Schicklgruber.

Kuna mabasiliko mengi ya ajabu kwenye hatma ya maisha ya kushangaza ya Adolf Hitler, ila hakuna linaloshangaza kama hili lililotokea miaka 13 kabla ya kuzaliwa kwake. Kama huyu mzururaji Miller (miaka 84) asingejitokeza kujitambulisha kama baba kwa kijana wake (miaka 39) karibu miaka 30 baada ya kifo Cha mama yake, Adolf Hitler angezaliwa kama Adolf Schicklgruber. Panaweza pasiwe na jambo kubwa kwenye jina, ila nimewasikia wajerumani (mwandishi) wakibashiri kama Hitler angekuwa mtawala wa Ujerumani kama angejulikana ulimwenguni kama Schicklgruber. Inaleta sauti flani hivi ya vichekesho kama likitamkwa na mtu kutoka Ujerumani ya kusini.

Mtu anawezaje kudhania umma wa wajerumani uliohamasika ukimshangilia Schicklgruber kwa mshindo wa sauti zao "Heils"? "Heil Schicklgruber!"?
Sio tu kama "Heil Hitler!" ilitumika kama shangwe ya kipagani na umma katika mikusanyiko ya wa - Nazi, bali ilikuja kuwa salamu ya lazma kati ya wajerumani kwenye utawala wa tatu, hata kwenye simu ambapo ilichukua nafasi ya salamu "Hello". "Heil Schicklgruber!"? Ni ngumu kidogo kumeza.

Itaendelea.... tuwe pamoja
 
Tuendelee...

Kwakuwa wazazi wa Alois hawakuwahi kuishi pamoja, hata baada ya ndoa, baba huyu ajaye wa Adolf Hitler aliishi na mjomba wake, ambaye pamoja na kuwa alikua kaka yake na Johann Georg Hiedler alitamka jina lake tofauti, alitambulika kama Johann von Nepomuk Huetler. Katika mtazamo wa chuki isiyoisha ambayo kiongozi huyu wa wa-Nazi alikuja kutengeneza kutoka ujana juu ya watu wa Czech, ambao taifa lao atakuja kuliangamiza, hili jina la kikristu Lina sababu ya kutajwa.

Johann von Nepomuk alikuwa mtakatifu wa taifa la watu wa Czech na baadhi ya wanahistoria wanaona kwa mtu wa familia ya Hitler kupewa jina hili ni ishara ya kuwa na damu ya watu wa Czech ndani ya familia. Alois Schicklgruber mwanzo alijifunza kazi ya ufundi viatu katika Kijiji Cha Spital, lakini akiwa hajatulia, kama baba yake, mapema aliondoka kutengeneza utajiri wake huko Vienna. Akiwa na miaka 18 alijiunga na askari wa mpakani katika idara ya huduma za mipakani ya Austria karibu na Salzburg, na kwakupandishwa cheo tu kwenye hiyo kazi, miaka tisa baadae akamuoa Anna Glasl- Hoerer, mtoto wa ku 'adopt' wa afisa wa Custom.
Mwanadada huyu alimpatia mahari kidogo na kumuinua daraja kijamii, kama ambavyo mambo yalivyokuwa yakifanyika katika umangimeza wa kizamani wa Austro- Hungary.

Ila hii ndoa haikuwa ya furaha. Mwanamke alikuwa amemzidi jamaa miaka 14 , akiwa na afya iliyokuwa ikidhoofika, na hakuwahi kupata mtoto. Baada ya miaka 16 waliachana na miaka mitatu baadae, mwaka 1883, alifariki. Kabla ya kuachana, Alois, Sasa akifahamika kisheria kama Hitler, alianza mahusiano na msichana mdogo mpishi wa hoteli, Franziska Matzelsberger, aliyemzalia mtoto wa kiume aliyempa jina la Alois mwaka 1882. Mwezi mmoja baada ya kifo Cha mke wake alimuoa huyu mpishi na miezi mitatu mbele alimzalia msichana, Angela.

Hii ndoa ya pili haikudumu kwa muda mrefu. Ndani ya mwaka mmoja Franziska alifariki kwa ugonjwa wa kifua kikuu. Miezi sita baadae Alois Hitler alioa kwa mara ya tatu na mara ya mwisho.

Huyu mchumba mpya, Klara Poelzl,ambaye baadae kidogo atakuwa mama wa Adolf Hitler, alikuwa na miaka 25, mime we 48, na walifahamiana kwa muda mrefu. Klara alitokea Spital, Kijiji chenye chimbuko la uzao wa kina Hitler. Babu yake alikuwa Johann von Nepomuk Huetler, ambaye binamu yake , Alois Schicklgrube- Hitler aliishi nae. Kwahivyo Alois na Klara walikua mabinamu wa upili na waliona ni muhimu, kama tulivyoona , kuomba ruhusa maalum ya kanisa kuruhusu ndoa. Ulikuwa ni muungano ambao maafisa wa Custom waliitafakari kwa miaka kabla, wakati alipompeleka Klara katika nyumba yake iliyokuwa haina mtoto kama mtoto wake mwenyewe katika ndoa yake ya mwanzo.

Huyu mtoto aliishi kwa miaka mingi na kina Schicklgruber huko Braunau, na mke wa kwanza alipokuwa akiugua Alois alionekana kuwa na fikra za kumuoa Klara mara tu mkewe atakapofariki. Uhalali wake na jinsi alivyokuja kupata urithi kwa mjomba wake ambaye alikuwa Babu wa Klara vilitokea wakati huyu msichana akiwa na miaka 16, umri wa kutosha kuolewa kisheria. Ila, kama tulivyoona, mwanamke aliendelea na maisha yake baada ya kuachana, na, labda kwasababu Alois wakati huo alishaanza mahusiano na mpishi Franziska Matzelaberger, Klara, akiwa na umri wa miaka 20, aliachana na huo mji na kwenda Vienna, alipopata kazi kama dada wa kazi za ndani.
Alirudi miaka minne baadae kumsaidia binamu yake kazi za ndani; Franziska pia, katika miezi ya mwisho ya uhai wake, aliondoka kwenye nyumba ya mumewe.

Alois Hitler na Klara Poelzl walioana January 7,1885, na miezi minne na siku 10 baadae, mtoto wao wa kwanza, Gustav, alizaliwa. Alifariki akiwa mchanga kama tu ilivyokua kwa mtoto wapili, Ida, aliyezaliwa 1886. Adolf alikuwa mtoto wa tatu katika ndoa hii ya tatu. Mdogo wake wa kiume, Edmund, aliyezaliwa 1894, aliishi kwa miaka sita tu. Mtoto wa Tano na wa mwisho, Paula, alizaliwa 1896, na aliishi kuona maisha ya kaka yake. Wadogo wa Adolf kwa upande mama Franziska Matzelsberger, Alois na Angela pia waliishi na kukua.

Itaendelea....
Vipi? Tuongeze speed?
 
Tuendelee...

Angela, mwanamke mzuri kwa muonekano aliolewa na afsa wa mapato aliyeitwa Raubal na baada ya kifo Cha mume wake alifanya kazi huko Vienna kama mfanyakazi wa ndani kwa muda,kama taarifa za Heiden ni sahihi, alifanya kazi kwenye jiko la kujitolea la wayahudi. Mwaka 1928 Hitler alimpeleka huko Berchtesgaden kama mtumishi wake wa ndani, na baada ya hapo kulikuwa na minong'ono ndani ya wa-Nazi juu ya vyakula vya Vienna ambavyo alimtengenezea Hitler na Hitler alivipenda sana.

Alimuacha Hitler mwaka 1936 na kuolewa na professor wa uhandisi huko Dresden, na Hitler wakati huo akiwa Kansela na Dikteta, alipingana na kuondoka kwake na akazira kutuma zawadi ya harusi. Alikuwa mtu pekee katika familia ambaye katika miaka ya mwisho ya Hitler alionekana kuwa karibu naye - ila Kuna tofauti Moja. Angela alikuwa na mtoto wa kike, Geli Raubal, msichana mrembo mwenye nywele za haki (blonde) ambaye, kama tutakavyokuja kuona, Hitler kwake alikuwa na mapenzi mazito na ya pekee katika maisha yake. Adolf Hitler hakutaka kusikia jina la kaka yake wa pembeni. Alois Matzelsbeeger, aliyekuja kujisajili baadae kama Alois Hitler, baadae alikuwa mhudumu wa bar, na kwa miaka mingi maisha yake yalikuwa ya mvutano na vyombo vya sheria.

Kumbukumbu za Heiden zinaonyesha kuwa, akiwa na miaka 18 alihukimiwa kifungo Cha miezi mitano Hela kwa wizi na akiwa na miaka 20 alihukimiwa Tena miezi nane jela kwa makosa hayohayo. Baadae alihamia Ujerumani, na kujikuta ameingia kwenye matatizo zaidi. Mwaka 1924, wakati Adolf Hitler akiwa jela kwa kusababisha fujo za kisiasa huko Munich, Alois Hitler alihukumiwa miezi sita jela na mahakama ya Hamburg kwa kosa la ndoa za mitara. Baada ya hapo, Heiden anaandika, alielekea Uingereza, ambapo haraka alianzisha familia na Kisha kuikimbia.

Kuingia madarakani kwa chama cha kijamaa Cha kitaifa (National Socialist party) kulileta nyakati nzuri kwa Alois Hitler. Alifungua 'Bierstube' - nyumba mdogo ya bia - pembezoni mwa Berlin, na kabla ya vita kuihamishia Wittenberplatz, magharibu mwa mji mkuu uliochangamka. Ilitembelewa mara kwa mara na maafisa wa ki-Nazi na katika kipindi Cha mwanzo Cha vita wakati wa uhaba wa chakula, penyewe chakula kilikuwa chakutosha. Nilikuwa nikienda hapo (mwandishi) mara kwa mara wakati huo. Alois alikuwa anakaribia miaka 60, akiwa mnene kiasi, mtu wa kawaida na mtu mzuri tu akifanania kwa mbali sana ki muonekano na kaka yake maarufu - wa pembeni lakini hakutofautiana sana na wamiliki wengine wa pub ndogo waliokuwepo Ujerumani na Austria.

Biashara ilikuwa nzuri, na bila kujali maisha ya nyuma, alionekana kabisa kufurahia maisha ya mafanikio. Alikuwa na wasiwasi mmoja tu : kwamba kaka yake wa pembeni, akikasirika anaweza kumfutia leseni. Wakati mwingine kulikuwa na minong'ono ndani ya hii nyumba ndogo ya bia kiwa Kansela na kiongozi mtawala alijutia hii kumbukumbu ya maisha duni ya familia ya Hitler. Alois mwenyewe, nakumbuka , alikataa kabisa kuingizwa kwenye mazungumzo yoyote yaliyomhusisha kaka yake wa pembeni - tahadhari ya busara ila iliyotughadhabisha sisi tuliotaka kujifunza yote tuliyoweza juu ya maisha ya nyuma ya mtu ambaye kwa wakati huu alishajipanga kuitawala Ulaya.

Ukiacha kwenye kitabu Cha Mein Kampf, ambako historia kidogo ya Hitler iliyopo inapotosha na iliyoacha vitu vingi vya msingi, ni mara chache sana Hitler aliongelea - au kuruhusu majadiliano akiwepo - juu ya historia ya familia yake na maisha yake ya mwanzo. Tumeshaona historia ya familia yake ilivyokua. Je, maisha ya mwanzo ya Adolf Hitler yalikuwaje?

Fuatana na Mimi kwenye simulizi linalofuata....
 
Tuendelee...

MAISHA YA MWANZO YA ADOLF HITLER.

Mwaka ambao baba yake alistaafu kutoka kazi ya Custom akiwa na umri wa miaka 58, Adolf akiwa na miaka sita alianza kusoma shule ya umma katika Kijiji Cha Fischlham, umbali mfupi kusini magharibi mwa Linz. Hii ilikuwa 1895. Kwa miaka minne au mitano huyu Mzee mstaafu asiyetulia alihama kutoka Kijiji kimoja kwenda kingine karibu na Linz. Wakati kijana alipofikisha miaka 15 aliweza kukumbuka mabadiliko Saba ya anwani na shule tano tofauti.Kwa miaka miwili alihudhuria darasani katika nyumba ya watawa ya Benedict huko Lambach, karibu na ambako baba yake alikuwa amenunua shamba. Hapo aliimba kwenye kwaya na kuingia kwenye madarasa ya kuimba na, kwa kumbukumbu zake mwenyewe, alitamaani siku moja kupokea maagizo matakatifu.

Baadae huyu mstaafu wa Custom akaweka makazi ya kudumu katika Kijiji Cha Leonding, kusini pembezoni mwa Linz, ambako familia ilimiliki nyumba ya kawaida na bustani. Akiwa na miaka 11, Adolf alipelekwa shule ya sekondari huko Linz. Hii iliwakilisha kujitoa kifedha kwa baba yake na ilitoa ishara ya nia kwa kijana kufuata hatua za baba yake na siku Moja kuwa mtumishi wa umma. Hilo ni jambo ambalo huyu kijana hakuwahi kulifikiria. "Wakati huo nikikaribia miaka 11", Hitler baadae aliandika, " nililazimishwa kupingana na baba kwa mara ya kwanza... sikutaka kuwa mtumishi wa umma."

Simulizi ya mapambano machungu ya huyu kijana akiwa bado haja komaa, dhidi baba mkorofi na mwenye msimamo ni Moja ya vipengele vichache vya historia ya maisha binafsi ya Hitler ambavyo aliviandika kwa undani na wakati huu kwa ukweli ndani ya kitabu Cha 'Mapambano Yangu' - Mein Kampf.
Ugomvi huu ulitoa picha kwa mara ya kwanza juu ya ukorofi, msimamo usioyumba ambao baadae ungempeleka mbali sana pamoja na magumu na vikwazo alivyopitia alisimama thabiti na waliokuja mbele yake na kuweka mhuri usiofutika juu ya Ujerumani na Ulaya yote.
...sikutaka kuwa mtumishi wa umma, hapana, na Tena hapana. Majaribio yote kwa upande wa baba ya kunipa moyo kwa upendo au kwa starehe juu ya fani hii kwa hadithi kutoka katika maisha yake yalipata Matokeo kinyume chake kabisa. Niliumwa tumbo Kila mara nilipowaza kukaa ofisini, nikikosa uhuru wangu; nikishindwa kusimamia muda wangu mwenyewe na kulazimishwa kujaza mambo yote juu ya maisha yangu katika fomu ambazo zilipaswa kujazwa... siku Moja ilikuwa dhahiri kwangu kwamba ningekuwa mchoraji wa kutumia rangi, msanii... Baba yangu alibaki kinywa wazi. "Mchoraji? Msanii?" Alikuwa na mashaka na utimamu wa akili yangu, au alidhani amesikia vibaya au alinielewa tofauti. Ila alipokuwa ameelewa somo, na hasa alipoona uthabiti wa nia yangu, alinipinga na nia ya utu wake wote..."Msanii! Hapana! Kamwe haitatokea nikiwa hai!"... Baba yangu hakuwahi kuondoka kwenye "Kamwe!"na Mimi nikakomaa na "Hata kama!"

Moja ya Matokeo ya huu mtafaruku, Hitler baadae alielezea, ni kwamba aliacha kusoma shuleni. "Nilifikiri kwamba mara baba atakapoona maendeleo yangu hafifu sekondari angeniacha nijikite kwenye ndoto yangu, bila kujali angependa au asingependa. Haya yaliyoandikwa miaka 34 baadae yanaweza kuwa sehemu ya sababu za yeye kufeli shule. Alama zake kwenye shule ya msingi zilikuwa nzuri tu. Ila katika sekondari ya Linz zilikuwa za chini kiasi kwamba mwishoni, bila kupata Cheti Cha Custom, alilazimika kuhamia kwenye sekondari ya serikali huko Steyr, ambali kiasi kutoka Linz. Alikaa hapo kwa mda mchache na baadae aliondoka bila kumaliza. Kufeli kwa Hitler shuleni kulimkereketa ndani yake kwenye maisha baadae, alipotoa dhihaka kwa daraja la wasomi, digree na diploma zao na mbinu zao za kufundishia.

Itaendelea....
 
"... Baba yangu hakuwahi kuondoka kwenye "Kamwe!"na Mimi nikakomaa na "Hata kama!"

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Hii kichwa ilikuwa kweli ya kiume hasa.
 
Tuendelee...

Hata katika miaka yake mitatu au minne ya mwisho katika makao makuu ya jeshi, ambako aliamua kuingia kwa undani kwenye mikakati, mbinu na utaratibu wa uongozi wa kijeshi, aliweza kuchukua jioni moja ya mapumziko kukumbushana na marafiki zake wa zamani katika chama juu ya upumbavu wa walimu aliokuwa nao katika ujana wake.

Baadhi ya tafakuri za kipanga huyu mwenye ukichaa, ambako kwa sasa alikuwa kiongozi wa juu wa kivita binafsi akiyaongoza majeshi yake makubwa kutokea 'The Volga' mpaka 'The English channel' zimehifadhiwa.

"Ninapotafakari juu ya watu waliowahi kuwa waalimu wangu, natambua kuwa wengi kati yao walikua wehu kidogo. Wale ambao wangeweza kuchukuliwa kuwa waalimu wazuri walikuwa wa tofauti sana. Ni hatari kufikiri kwamba watu wa aina hiyo wana nguvu ya kuzuia njia ya kijana."
March 3, 1942

"Nina kumbukumbu mbaya sana juu ya waalimu walionifundisha. Muonekano wao wa nje haukuwa msafi; ukosi wa mashati yao haukuwekwa sawasawa...walikuwa zao kizazi cha wafanyakazi walionyimwa kabisa uhuru wao binafsi wa kufikiri, wakitambulishwa na ujinga usio na mfano uliofaa sana kuwafanya kuwa nguzo system dhaifu ya kiserekali ambayo, namshukuru Mungu, ni kitu kilichopita.- April 12, 1942.

"Ninapovuta kumbukumbu ya waalimu wangu shuleni, nagundua kuwa nusu kati yao hawakuwa kawaida... Sisi wanafunzi wa Austria ya zamani tulikuzwa tukifunzwa kuwaheshimu watu wazee na wanawake. Ila kwa maprofesa wetu hatukuwa na huruma; walikuwa ni maadui wetu wa jadi. Wengi kati yao walikuwa na mtindio wa ubongo, na wachache sana walimaliza siku zao Kama wazandiki walio watu wema kwa Mungu.... Binafsi nilikuwa na harufu mbaya sana kwa waalimu. Sikuonyesha kuhamasika na lugha za kigeni- japo ningeweza, Kama sio kwa mwalimu kuwa mwehu wa akili. Sikuweza kuvumilia kumtazama."- August 29.1942

"Walimu wetu walikuwa madikteta kamili. Hawakuwa na huruma na vijana; lengo lao moja lilikuwa kujaza bongo zetu na kutugeuza kuwa kima kama walivyokua wao. Na Kama mwanafunzi yoyote alionyesha dalili ya kujitambua, walimtesa bila kukoma, na wanafunzi wa 'mfano' ambao niliwahi kuwafahamu wameshindwa kabisa baadae katika maisha". -September 7, 1942.

Mpaka siku yake ya kufa, ilikuwa wazi, Hitler hakuwahi kuwasamehe waalimu wake kwa alama za chini walizokua wakimpatia - na wala hakuweza kusahau. Ila aliweza kupotosha kwa kiwango kisichomithilika.
Muonekano alioutengeneza juu ya waalimu wake, iliyokusanywa baada ya yeye kuwa mtu maarufu duniani, imerekodiwa kwa ufupi.

Moja kati ya wakufunzi wachache Hitler alioonekana kuwapenda alikuwa profesa Theodor Gissinger, aliyejitahidi kumfundisha Sayansi. Gissinger baadae alinukuliwa akisema," Kwa jinsi nilivyofahamu, Hitler hakuacha picha nzuri wala mbaya huko Linz. Hakuwahi kuwa kiongozi wa darasa. Alikuwa mwembamba na mrefu, uso wake ukiwa umepoteza rangi na mwembamba, akiangalia kwa uangavu usio wa kawaida na macho yaliyongaa".

Professor Eduard Hurmer, aliyetambulishwa na Hitler Kama mwehu wa akili hapo juu - kwakuwa alifundisha kifaransa - alikuja Munich mwaka 1923 kutoa ushahidi juu ya mwanafunzi wake wa zamani, aliyekuwa akituhumiwa kwa 'treason' wakati huo.
*Alielezea simulizi juu yake katika hali ya kutia huruma jioni ya January 8 - 9, 1942, katika makao makuu.
(Mazungumzo ya Siri ya Hitler, ukurasa wa 160).


....Inaendelea...
 
Tuendelee..

Pamoja na kwamba alipigia chapuo malengo ya Hitler na kusema kwamba anatamaani kweli kutoka kwenye uvungu wa moyo wake kwamba Hitler afanikiwe kutimiza malengo yake, ila alitoa vielelezo ya muonekano wa Hitler akiwa mwanafunzi wa High school: Kwa hakika Hitler alikuwa na kipaji, pamoja na kwamba ni kwa baadhi tu ya masomo, ila hakuwa na utulivu wa kujiongoza, na kusema kwa uchache alikuwa mtu mbishani, Mangimeza, mwenye mitazamo ya peke yake na mwenye hasira mbaya na ambaye alishindwa kwendana na nidhamu ya shule.

Hakuwa pia mtu wa kujituma; vinginevyo angepata matokeo mazuri zaidi kwa kipaji alichokuwa nacho. Kulikuwa na mwalimu mmoja huku 'Linz high school' ambaye alikua na ushawishi zaidi kwa Hitler na kama ilivyokuja kutokea baadae ushawishi uliokuja kuwa sehemu ya maisha ya Hitler baadae. Huyu alikuwa mwalimu wa historia, Dr. Leopold Poetsch, aliyetokea katika mpaka wa mkoa wa kusini wa lugha ya kijerumani ambako unakutana na ule wa kusini mwa Slovakia na ambaye uzoefu wake pale na ubaguzi wa asili ulimfanya kuwa mjerumani mzalendo kindakindaki.

Kabla ya kuja Linz alifundisha huko Marburg, ambapo baadae, wakati eneo lilipohamishiwa Yugoslavia baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia, pakaitwa Maribor.
Pamoja na kwamba Dr. Poetsch aliwapatia wanafunzi wake alama za wastani tu, alikuwa mwalimu pekee wa Hitler kutolewa wasifu mzuri katika kitabu cha Hitler 'Mein Kampf'. Hitler alikuwa tayari kukiri deni lake kwa huyu mtu.

"Ilikuja labda kuwa na maamuzi kwa maisha yangu yote ya baadae kwamba bahati nzuri ilinipatia mwalimu wa historia aliyetambua, Kama wachache walivyotambua, hii kanuni ...ya kukumbuka mambo ya msingi na kusahau mambo yasiyo na msingi...katika mwalimu wangu, Dr. Leopold Poetsch wa 'high school Linz' hili takwa lilitekelezwa kwa namna sahihi sana. Huyu mzee mstaarabu, mkarimu ila wakati huohuo akiwa na misimamo imara, aliweza sio tu kupata usikivu wetu kwa uongeaji wake mzuri ila kutuchukua sisi kifikra pamoja na yeye. Hata leo nakumbumbuka ya nyuma kwa hisia za kiungwana juu ya huyu mtu mwenye mvi, ambaye kwa moto wa maneno yake, wakati fulani alitufanya kusahau yanayoendelea Sasa; ambaye Kama vile kwa mazingaumbwe, alitusafirisha katika nyakati zilizopita na, kutoka katikati ya milenia ya wakati, akageuza kumbukumbu kavu za kihistoria kuwa uhalisia unaoishi.

Hapo tulikaa, tukiwa na moto wa kiu ya ufahamu, muda flani hata tukitokwa na machozi... Alitumia uzalendo wetu kwa taifa Kama namna ya kutuelimisha, mara kwa mara akitaka tuonyeshe hisia za heshima ya utaifa wetu.
Huyu mwalimu alifanya Historia kuwa somo langu pendwa.
Na kwakweli, japo hakuwa na nia hiyo, ilikuwa baada ya hapo nikwa mwanamapinduzi kijana."

Miaka 35 baadae, 1938, alipoitembelea Austria kwa ushindi baada ya kuikata na kuiingiza kwenye utawala wa tatu, kansela Hitler alisimama kule Klagenfurt kumwona mwalimu wake wa zamani, wakati hio akiwa kwenye mapumziko ya uzee. Alifurahi kugundua kuwa huyu mzee alishakuwa mwanachama wa maaskari kanzu wa Nazi S.S, ambacho kilipigwa marufuku katika uhuru wa Austria.
Alizoza nae kwa faragha kwa lisaa limoja na baadae alisema na wanachama wa cha chake, "Huwezi kuamini ni kiasi gani ninadaiwa na huyu mzee".

Alois Hitler alifariki kwa shida ya mapafu, January 3,1903, akiwa na umri wa miaka 65. Alizidiwa akiwa kwenye matembezi ya asubuhi na akafariki muda mchache baadae katika lodge ya karibu kwenye mikono ya jirani yake. Wakati kijana wake wa miaka 13 alipoona mwili wa baba yake aliangua kilio. Mama yake aliyekuwa na miaka 42 , alihamia kwenye makazi nadhifu kiasi huko Urfahr, mji kidogo nje ya Linz, ambako alijitahidi kujitunza mwenyewe na wanae wawili waliosalia, Adolf na Paula, kwa hakiba kidogo na mafao aliyoachiwa. Alijisikia kuwa na wajibu, Kama Hitler alivyogundua kwenye
 
Tuendelee...

Mein Kampf, kuendeleza elimu yake kama yalivyokuwa matamaanio ya baba yake - "kwa maneno mengine", kama anavyoyaweka," kwa mimi kusoma kwaajili ya kazi ya umma". Pamoja na kuwa mjane huyu kijana alikuwa na ushawishi kwa mwanae, na Hitler alionekana kumpenda kwa dhati, ila alikuwa " na nia ya dhati kuliko mwanzo" Kama alivyosema," kuto kuwa mtumishi wa umma". Na hivyo, pamoja na mapenzi mazuri kati ya mama na mtoto, kulikuwa na msigano na Adolf akaendelea kupuuza masomo yake.

"Kisha mara ugonjwa ukaja kunisaidia na kwa wiki chache ukaamua hatma ya maisha yangu ya baadae na mgogoro wote ndani ya nyumba." Ugonjwa wa mapafu ambao Hitler aliupata akikaribia miaka 16 ulilazimisha aache shule kwa angalau mwaka mmoja. Alipelekwa kwa muda kwenye familia kijijini Spotal, ambako alikaa kupata nafuu katika nyumba ya dada wa mama yake, Theresa Schmidt, mwanamke mkulima.

Alipopona alirudi kwa muda mfupi katika Steyr high school iliyokuwa shule ya serikali. Report yake ya mwisho, ya September 16, 1905, inaonyesha alama za 'wastani' kwenye somo la kijerumani, kemia, Fizikia, Geometry na Geometrical drawing. Kwenye geografia na historia alipata alama za 'vizuri'; na kwenye michoro ya mikono akapata alama ya 'vizuri sana'. Alijisikia furaha sana kwa kuondoka shule moja kwa moja kiasi kwamba kwa mara ya kwanza na ya mwisho katika maisha yake alikunywa pombe.

Kama alivyokuja kukumbuka kwenye miaka ya baadae aliomotwa karibu na asubuhi, akiwa amelala barabarani katika barabara iliyoelekea vijijini nje kidogo ya Steyr. Aliokotwa na mfanyakazi wa kuuza maziwa na kurudishwa mjini, akiapa kutokurudia tena. Miaka miwili au mitatu iliyofuata Hitler aliielezea Kama miaka ya furaha zaidi kwenye maisha yake. Wakati mama yake aliposhauri - na ndugu wengine kugusia - kwamba aende kufanya kazi na kujifunza ujuzi, yeye alitosheka na ndoto za maisha ya baadae kama msanii na kuwaza maisha ya furaha pembeni ya Danube.

Hakuwahi kusahau "maisha laini" ya miaka hiyo kuanzia miaka 16 hadi 19 wakati kama "kipenzi cha mama" alifurahi ukamilifu wa maisha yasio na mikingamo."
Pomoja na kuwa huyu mjane aliyekuwa mgonjwa alipata wakati mgumu kukidhi mahitaji ya familia kwa kipato kiduchu, Adolf kijana alikataa kusaidia kwa kutafuta kazi. Wazo tu la kupata chakula chake mwenyewe kwa kazi ya kuajiriwa halikumwingia na ilibaki hivyo kwa maisha yake yote yaliyofuata. Kilichofanya miaka yake ya mwisho ya kukaribia utu uzima iwe ya furaha kwa Hitler ulikuwa ni uhuru wa kutokufanya kazi, ambao ulimpa uhuru wa kufikiri, kuwa na ndoto mbalimbali, kutumia siku zake akizurura katika mitaa ya jiji au vijijini akitafuta ambacho hakikua sawa katika ulimwengu na kujaribu kuona njia ya kutatua, na jioni akiwa anajisomea kitabu au akiwa nyuma ya nyumba ya opera huko Linz au Vienna akisikiliza kazi za kipagani za Richard Wagner.

Rafiki yake katika ujana baadae alimkumbuka kama mtu aliyekosa uchangamfu, mgonjwamgonjwa, kijana aliyepoa sana, ambaye pamoja na kwamba mara nyingi alikuwa na aibu na akirudi nyuma kwenye mambo, ila alikuwa anaweza kuonyesha hisia kali za ghafla za hasira dhidi ya wanaopingana nae.

Kwa miaka minne nafsi yake ilianguka kwenye penzi zito na mfanyakazi aitwae Stefanie mwenye nywele nyekundu, na pamoja na kwamba alikuwa akimtazama kwa hisia na matamaanio alipokuwa akipanda na kushuka katika ngazi huko Linz akiwa na mama yake. Hakuwahi kufanya jitihada yoyote kukutana nae, akifurahia zaidi kumuacha, Kama vile vitu vingine, katika ulimwengu wa vivuli wa matamanio yake makali.

Inaendelea...
 
Tuendelee...

Kwakweli, ndani ya mashairi yasiyo na idadi ya mapenzi aliyomuandikia japo hakuwahi kumtumia ( moja kati yao liliitwa "tenzi za sifa kwa mpendwa") na ambao alisisitiza kumsomea rafiki yake kijana mwenye subira, August Kubizek.

Pamoja na kuwa Hitler alinuia kuwa msanii, zaidi kama mchoraji wa rangi au angalau mhandisi, alishaanza kuvutiwa na siasa akiwa na miaka 16.
Wakati huo alishajenga chuki ya fujo juu ya Monarch ya Hapsbirg na watu wengine wasio na asili ya kijerumani katika himaya ya mataifa mengi ya Austro - Hungary ambako iliongoza, na ugendo wa fujo kwa kiasi hichohicho kwa kila kitu cha kijerumani. Katika miaka sita alishakuwa jinsi ambavyo angebaki mpaka mauti yake : mjerumani mwenye uzalendo wa kupitiliza.

Alionekana kutokuwa na ule moyo wa 'kutokujali' wa ujana pamoja na huduma zote za mama yake. Matatizo ya ulimwengu yalimuelemea yeye. Kubizek baadae alikumbuka, " Katika kila mahali aliona tu vizuizi na uadui... Alikuwa wakati wote dhidi ya Jambo na mgogoro na ulimwengu... Sikuwahi kumwona akichukuloa jambo lolote kwa wepesi..."

Ilikuwa katika hiki kipindi ambapo kijana aliyeshindwana na shule akawa msomi mwenye bidii, akijiunga na maktaba ya elimu ya watu wazima huko Linz na kujiunga na jamii ya makumbusho, ambako aliazima vitabu kwa idadi kubwa.
Rafiki yake wa ujana alimkumbuka kama mtu aliyezungukwa na vitabu wakati wote, ambavyo alivyovipenda zaidi vikiwa vitabu katika historia ya Ujerumani na Germany mythology.

Kwakuwa Linz ulikuwa mji mdogo, haikuchukua muda mrefu kabla Vienna, mji mkubwa uliong'aa na makao makuu ya himaya, kuanza kumtambua kijana mwenye malengo makubwa, matamaanio na fikra. Mwaka 1906, baada tu ya birthday yake ya 17, Hitler aliondoka akiwa na fedha alizopatiwa na mama yake na ndugu wengine kutumia miezi miwili kwenye vituo vikubwa vya usafiri. Japo baadae lilikuja kuwa eneo la machungu kwake kwa miaka ya baadae, ambako mara kadhaa aliishi kwenye 'gutter - makinga maji'/ kofia za kukinga maji ya mvua, Vienna kwenye hii safari ya kwanza ilimvutia. Alizunguka mitaani kwa siku kadhaa, akijawa na matumaini kwa kutazama majengo marefu kwenye mzunguko na katika hali ya furaha sana kwa alichoona kwenye makumbusho na nyumba za opera na kumbi za maonyesho.

Pia aliulizia juu ya taratibu za kujiunga na Academy ya sanaa ya Vienna, na mwaka mmoja baadae, October 1907, alirudi kwenye haya makao makuu kufanya mitihani ya kujiunga Kama hatua yake ya kwanza ya kivitendo katika kutimiza ndoto zake za kuwa mchoraji wa rangi. Alikuwa na miaka 18 na akiwa na matumaini makubwa, ila yalitupiliwa mbali. Mpangilio wa orodha ya wanaoingia kwenye academy unajieleza.
Wafuatao walifanya mtihani na kuwa na matokeo hafifu, na hawakuandikishwa... Adolf Hitler, Braunau a. Inn, April 20, 1889, Mjerumani mkatoliki. Baba mtumishi wa umma. Madarasa manne high school. Majaribio ya uchoraji hayaridhishi.

Inaendelea...
 
Back
Top Bottom