Kupandishwa vyeo, mishahara na mengineyo: Watumishi wa umma mna maoni gani?

Kupandishwa vyeo, mishahara na mengineyo: Watumishi wa umma mna maoni gani?

Kikao hiki ni muhimu sana kwa mustakabali wa maisha yetu.

Awamu ya tano imeweka rekodi ya kutunyima kupanda madaraja na mishahara tena kwa dharau.

Kura zeru zinatosha kupeleka ujumbe kwamba sisi pia ni binadamu.

Wao wanapesa hadi za kugawa mitaani, na kununua jogoo kwa laki moja lakini swala la mishahara yetu linaonekana ni la kipuuzi.

Agenda.

1. Wafanyakazi wa umma kwenda kupiga kura.. Hamasa.

2. Kukataa jina la mtu jeuri asiye thamini wafanyakazi wa umma.

3. Mengineyo.

Karibu mwenyekiti na wajumbe kikao kimefunguliwa.


View attachment 1530815
sisi JUDICIARY tushateta jambo letu, mpira kwenu
 
Ndugu zanguni nipo chini ya miguu yenu, nawaombeni tusiishie tu kucomment bali october wote kwa umoja tuungane tukapige kura. Kura yako ndiyo italeta mabadiliko
 
Ukipanda daraja lazima mshahara upande?
Mwaka jana madaraja kuna baadhi walipandishwa. Mwaka huu mapendekezo ya wapandishwa yalishafijishwa kwa wahusika, uzembe upo Utumishi. Mkuchika kazeeka sana waweke waziri mwingine mwenye nguvu.
 
Huwa nachat na jamaa zangu wawili walitia nia kanda ya ziwa, wanasema Lissu ajiandae kuunda serikali ya mseto maana CCM itapata wabunge wengi lakini JPM atakosa ushindi. Hali ya maisha ni ngumu sana, LISU aangalie asifanye makosa ya kudharau hali ya maisha ya watu na kuhangaika na magorofa. Watanzania ni watu sio magorofa....
 
Eti Tanzania iwe kama ulaya.. nani alikwambia maisha ya ulaya ni bora kuliko maisha yetu..


Tena africa tinaishi maisha marefu zaidi
Huwa nachat na jamaa zangu wawili walitia nia kanda ya ziwa, wanasema Lissu ajiandae kuunda serikali ya mseto maana CCM itapata wabunge wengi lakini JPM atakosa ushindi. Hali ya maisha ni ngumu sana, LISU aangalie asifanye makosa ya kudharau hali ya maisha ya watu na kuhangaika na magorofa. Watanzania ni watu sio magorofa....
 
Watumishi wa umma wamekuwa wanaulizana na mwaka huu hawatapanda madaraja mbona kimya sana?

Licha ya mwaka jana wengine kupanda na wengine kuachwa kigezo cha masomoni wanashangaa tena mwaka huu serikali kupitia wizara ya utumishi wapo kimya.

Kupanda daraja ni haki ya mtumishi na kwa mjibu wa sheria za utumishi wa umma,kutopandishwa kwa wakati ni kuwanyima watumishi haki zao na kuwavunja moyo na mbaya zaidi kwa watumishi ambao wanaenda kustafu kupunjwa malipo yao kwa kutopandishwa madaraja.

Waliokuwa masomoni wanalalama hawakupanda madaraja, waliopo kazini wanalalama, wakulima wanalalama, wafanyabiashara wanalalama, wazabuni wanalalama, wanaohitimu wanalalama hakuna ajira.

Serikali hii haijamsaidia mtu yoyote Tanzania
 
Hajaeleza kuwa ndani ya miaka mitano hakuna mshahara kuongezeka na halafu raisi anataka kura za watumishi, huu ni utani mbaya. Mimi naona angepita kwenye hizo fly over, bombardier na ahamie kwenye hilo bwawa la umeme ili wale wanaomwelewa wamfuate huko. Hakuna kitu kibaya kama unafanya kazi bila kupewa stahiki zako afu mtu anakuhubiria mambo ya fly over.
 
Na bado, na shauri apunguze salary kwa 50% ili kwa pamoja wachukue hatua. kulalamika pekee haitoshi.
 
Rais asiye na tija yoyote ile kwa Watumishi wa Umma! Ameona kutugawa ndiyo njia sahihi kwake. Wachache wanamfurahia sana, huku walio wengi nikiwemo mimi tukimuona kama kiumbe asiye na faida yoyote ile kwenye maisha yetu ya kila siku. Haiwezekani toka mwaka 2015, tunazungushwa tu!

JK alikuwa ndiye Rais wa kweli!Kika baada ya miaka 3, daraja linapanda. Achilia mbali Annual Incriment kila mwishoni mwa mwezi wa 7! Hakika atakumbukwa sana na Watumishi wa Umma. Ika siyo huyu anayependa kusifiwa na kutukuzwa muda wote, hata katika mambo ambayo siyo ya msingi.
 
Nini madaraja, nakuhakikishia hata ikitokea wamepunguziwa mishahara wataendelea kuchapa kazi.... huu ni uzalendo!
 
Back
Top Bottom