Kupangiwa kazi vijijini tayari unakuwa umeuliwa kifikra na kitaaluma

Watu wengi wakistafu wanarudi mjini Sasa na mipango mizuri sikuzote wekeza zaidi pale ambapo una malengo ya kustafu Sasa hii miradi au fursa ulizotaja hapa ukishastafu na kurudi mjini unaenda kuanza upya tena inakuwa umefanya kazi bure au ndio unampango wa kuzeekea na kufa huko porini.
 
Unarudi Mjini kuishi ila shughuli zako zinasalia kuwa Kijijini,mjini hakuna mashamba
 
Kirahisi tu namna hio. Mshahara wa laki 4 na nusu unajengaje godauni🤣
 
Ni kweli mkuu
Enzi hizo nikiwa bado msaga mashine wa kijiji kule kijijiji kwetu nimewala sana waalimu wapya maana mie ndo nilikuwaga mjanja mjanja ambaye niliwahi kufika Dasilamu[emoji38]
Unatupiga fix kiaina haya twende kaz.
 
Momba wenye unafuu wa maisha ambao niliona Wana ule unafuu ni watumishi walioajiriwa kule juu (Sumbawanga road)
Ila kule bondeni, HAKUNA ASIYEWAZA KUHAMA KULEE.

Hata huyu SHAZ96 anakuzingua tu ukute ni ajira mpya.

Hivi unajua Kuna watu wanaajiriwa huko Momba, ila wanafika tu kazini huwa wanaacha hapohapo???

Jamaa angu yeye alijikomboa (ni mtendaji kata)

Kila juma5 tuko nae mjini tunafanya biashara, ila anakwambia "Ukiajiriwa Momba dishi lazima liyumbe"

#YNWA
 
Hata uwe na solar kama mazingira yanayokuzunguka ni watupori lazima na wewe uwe pori
Pengine hujafika hivyo vijiji ninavyomaanisha unadhani nikisema kijiji namaanisha kijiji cha Makumbusho Dar[emoji1787]
Ili uendelee na kupanuka kifikra lazma uzungukwe na watu waliofanikiwa zaidi. Ndio maana mjini humu watu wanashindana na kupambana kuiba ili wajenge mijengo mikali, ndinga kali na miradi kama mahoteli, mashule, ma lodge na mabiashara makubwa.

Sasa ukae kijijini ambako wewe mwenye Rav 4 dume ndio unakuwa role model wao. Hakuna mtu ambaye anaku motivate. Vijiwe ni vilabu vya komoni, ulanzi, choya ambako wenye akili humo wanawaza kuvuna heka 3 na kuongeza wake tu. Kujenga nyumba ya tofali za kuchoma bure kabisa. Very odd thinking ukiwa mtu wa kusikilizia utashangaa umefika 50s huna cha maana zaidi ya kishamba cha mihogo na kijumba cha tofali za kuchoma.
 
M
mwanangu una akili sana achana na mtoa post akili yake ipo kwenye comfort zone bado imejaa tope
 
Hakuna mwajiriwa anayeweza kusave kama yule wa kijijini kama hatopenda starehe za kwenda kwenda visafari vya mjini.

Kijijini kuna uzuri wake pia na changamoto zake, changamoto kubwa kuliko zote siyo maji wala umeme bali ni kuishi na wanakijiji wa pale, ukileta umjini pale unakufa au kuacha kazi bila kujua. Ishi nao kwa akili sana inabid ufanane nao kila kitu.
 
Hivi Kuna maeneo bado wanatumia mafuta taa?
Kwamba hata solar hamna?

Umaskini upo lakini sio kama ulivo-potray hapa
Hayo maeneo yapo lakini ni kwamba kwa sasa wafanyabiashara wa sola wamefika huko. Ila wengi wao hawana umeme wa Tanesco wala hawana sola ya umeme wa kutosheleza mahitaji labda sola hizi tochi za kuwasha kwa ajili ya mwanga tu.

Mi kuna kitongoji jirani na kijiji chetu hawana access ya umeme wa Tanesco ila huduma zao wanakuja kwetu kama kusaga nafaka, kuchaji simu, n.k
 
Uzuri ni kwamba ukiacha wengine wanaajiriwa..

Siku Moja nimeenda site kuoneshwa Ili tuchonge Barabara ni Mwambao mwa Ziwa Tanganyika yaani Kuna Vijiji vingi sana havina Barabara usafiri wao ni maji na Kwa maboti ya kienyeji..

Sasa tukaanza safari ndio ilikuwa mara ya kwanza kusafiri kwenye mi via mitumbwi ya kienyeji no life jacket no nini? Aisee niliogopa nikafikiria mara mbili kwamba hivi hakuna kazi nyingine ya kufanya Hadi hii inayohatarisha maisha yangu?

Nikamwambia mwenyeji Wetu mtendaji kata kwamba Mimi kama ndio maisha haya daily naweza acha kazi,akacheka akasema ukixoea utaona kawaida akatutia Moyo wewe yaani hapo mnarushwa Juu na mawimbi harafu unashuka paa yaani kufa Nje Nje..

Hapo ndio nikasema Vijiji vya dizaini hiyo hapana ,Hadi Leo nilisema wakija kusema niende tena ntawajibu Nina kizungu zungu,kusafiri km 40 ndani ya maji sio mchezo.
 
Sasa ukilima na kufuga ukapata mahela unataka NN ?
 
Sawa Tajiri wa Mjini choko Fulani hivi 🤪🤪
 
Ni bora ni ishi Town kwa maisha ya kuunga unga lakini napata huduma zote muhimu kuliko kuishi kijijini kwenye mazingira hatarishi kwa mshahara wa 400k.....hata ufanyeje kuishi kijijini akili zitayumba utotofautiana na wenyeji wako hapo ni kulea umasikini na kuua kizazi chako bure kwa kutaka kuonyesha uzalendo uchwara. Mimi kijijini siendi hata unipe mshahara wa 1m haya maisha ni mafupi sanaa.
 
Mil.1 unaisikia au unaleta mzaha? Ni risk kwa hizo 450k lakini sio Kwa 800k and above maana unakuwa doni wa Kijiji yaani wote wanakuja kwako lazima utoboe.
 
Ajira Mpya msihofu , Serikali inakazana sana kuboresha maisha ya Vijijini Kwa Sasa kuhakikisha Huduma zote zinapatikana..

Hamjasikia siku hizi Kijijini ni kama mjini? Nunua boda yako mambo yaendelee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…