Kupangiwa kazi vijijini tayari unakuwa umeuliwa kifikra na kitaaluma

Naunga mkono hoja mkuu.
 
Hivi Kuna maeneo bado wanatumia mafuta taa?
Kwamba hata solar hamna?

Umaskini upo lakini sio kama ulivo-potray hapa
 
Katika dunia ya utandawazi kuishi mahali pasipo na umeme wala mtandao kisa kilimo na nyumba za bure zisizo na umeme ni ufala.

Sitakaa eneo la namna hii tena bora kufa masikini.

Wanasiasa wanakula bata kwenye ma-V8 hawakumbuki wenzao wa vijijini eti kisa hata mbuyu ulianza kama mchicha.

Unaweza kuishia kuwa mchicha kiboya
 
Nikipata ajira huko ni mwaka tu au miwili nawabwagia kazi yao.

Serikali inachezea sana hatima za watu
 
Hayo sawa, shida ni kukosekana fursa za kujiendeleza kitaaluma huku ukiwa kazini
 
Hivi wewe umewahi Fanya kazi kijijini? Unavifahamu vijiji vya mkoa wa Simiyu au shinyanga? Huku wenyeji hawataki muona mgeni akifanikiwa uchawi Kila Kona tena hadi watumishi wanatumia ndumba hasa wenyeji wa huko unakuta Kijiji kina kaya 400 katika hizi kaya 97 ni za waganga wa kienyeji kaya 250 ni wachawi kaya zilizobaki ndo Zina ahueni umasikini ni WA kutupa halafu kuna mtu anasema vijijini kuna fursa ninawasi wasi utakuwa umetembelea vijiji vya DSM pekee! Kuna vijiji huku greda halijawahi fika kuna Barbara za ng'ombe tu usiombe upate dharula wakati wa masika utajuta.
 
Eeh kwa kuzungumza tu fursa huwa nyingi sana fika kijijini sasa
Mm ninazungumza kwa experience.
Nimewahi kufanya kijijini, mpakani na Malawi, nilihudumia vijiji viwili kwa wakati mmoja, Katumbasongwe na Mpunguti.

Uchawi hata mjini upo. Kama huwezi kupambana sio kosa lao wao.

Umesema hata watumishi ni wachawi, kwa issue sio kijijini ni imani yako binafsi.

Changamoto za masika nimeziishi na mafuriko pia. Lakini nilipambana, baada ya miaka mitatu nikapata fursa kurudi masomoni ndio namna nilivyochomoka.
 
Niko halmashauri ya vijijini kwa miaka 13 sasa ila nachowaza ni kuhama tu.

Watu wengi wanaoniambiaga "usihame kijijini Kuna fursa" huwa nawajibu "Njoo wewe huku mi nije mjini" naonaga hukaa kimyaa na hawanijibu.

#YNWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…