Kijijini fursa nyingi sana, hasa kwenye sekta ya ardhi, kilimo, ufugaji (ng'ombe wa maziwa, mbuzi...), usafirishaji, uvuvi (kwa baadhi ya maeneo), maji, na viwanda vidogo (kama kufyatua tofali, kutengeneza makochi, kushona nguo...).
Pia kijijini wana jamii wanakuwa na ushirikiano mkubwa sana kwa wataalamu wa afya, jambo linalokupatia faraja kubwa ambayo ina thamani kubwa isiyoweza kupimwa kwa kipato cha pesa.
Kijijini pia unapata muda wa kuwa karibu na familia yako kama unayo.
Kijijini unaweza kupata nyumba ya serikali bure, au ukapata nyumba nzuri kwa gharama nafuu, hivyo kusave something.
In short kijijini fursa ni nyingi kuliko mjini kwa watu wenye mshahara unaolingana, na kwa mwenye akili inachangamka zaidi nje ya your comfort zone kuliko kudumaa mjini na vijiwe (kufanya fani moja pekee).