Kupangiwa kazi vijijini tayari unakuwa umeuliwa kifikra na kitaaluma

Kwa nini volunteers kutoka Ukaya na USA wanamudu kuishi vijijini Tanzania bila malalamiko? Msiseme wote ni wapelelezi! Wengine ni raia wa kawaida kabisa na wamekuja Afrika kupata ajira wakitokea huko kwao.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Kwani wanaka kwa miaka mingapi au miezi tu? Wewe unajilinganisha na watu wanao lipwa mshahara na allowance inao zidi kipato chote cha kijiji wewe unaota, kijijini ni nusu jahanamu unaishi kama mnyama wakufuga.
 
Huwa nawaonea huruma sana hasa waalimu wa kike yaani unakuta binti kakulia Dar halafu anakuja kupangiwa kazi kijijini ndani kabisa tena mkoa tofauti unakuta wakazi wa huko hawajui hata kiswahili wanaongea kirugha chao tu, kijiji kizima hakuna hata duka na internet haikamati hata simu yenyewe mtandao unasoma kwa taabu!
Mbaya zaidi hakuna umeme wala maji
Ni mwendo wa kibatari na maji ya kisima tena ya kufuata kijiji cha tatu
Hapo ni mwaka mmoja tu binti wa watu keshazeeka kachooka kama kikongwe wa miaka 90
Unakuta ameshakuwa chakula cha wafugaji[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
wapi huko,nko zangu hapa kijijini nimejenga kijumba changu,umeme IPO na kisima changu cha fully maji net inasoma 4G Mungu anipe Nini Sasa zaidi ya UHAI tu
 
Hivi wewe umewahi Fanya kazi kijijini? Unavifahamu vijiji vya mkoa wa Simiyu au shinyanga? Huku wenyeji hawataki muona mgeni akifanikiwa uchawi Kila Kona tena hadi watumishi wanatumia ndumba hasa wenyeji wa huko unakuta Kijiji kina kaya 400 katika hizi kaya 97 ni za waganga wa kienyeji kaya 250 ni wachawi kaya zilizobaki ndo Zina ahueni umasikini ni WA kutupa halafu kuna mtu anasema vijijini kuna fursa ninawasi wasi utakuwa umetembelea vijiji vya DSM pekee! Kuna vijiji huku greda halijawahi fika kuna Barbara za ng'ombe tu usiombe upate dharula wakati wa masika utajuta.
ACHA kupotosha watu,mi mzawa wa shinyanga na nafanyia KAZI shinyanga Kuna wakulima huku wanalima tumbaku wanapiga zaidi ya milioni 20 Kwa msimu ,Sasa watamuonea wivu Gani mtumishi asie na pesa hata mambo ya waganga huo ni uongo 100%.
 
Kwa nini volunteers kutoka Ukaya na USA wanamudu kuishi vijijini Tanzania bila malalamiko? Msiseme wote ni wapelelezi! Wengine ni raia wa kawaida kabisa na wamekuja Afrika kupata ajira wakitokea huko kwao.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Tuambue hao volunteers wa kizungu wapo kijiji gani ili nipate uhakika, niende nikajionee maajabu.
 
Mtumishi usipotoboa kijijini utatoboa wapi Sasa,kule Kila kitu ni bure matumizi ya pesa ni machache utabakia na saving ya kutosha mtaji,maji bure, Kuni bure, chakula ishi vizur na wanakijiji wanakupa bure,cheap labour elf 5 kwa kazi ya trekta.Kijijini ukawe Kama daraja la kuunganisha uhitaji wa mijini na kijijini
Ndio mnavojidanganya, eti mtafanya serving, serving ya nyokwe! Kuna vijiji tuu kufata huduma nauli boda elfu 30, wakati mtu anatoka chanika to makumbusho kwanauli ya buku tuu
 
wapi huko,nko zangu hapa kijijini nimejenga kijumba changu,umeme IPO na kisima changu cha fully maji net inasoma 4G Mungu anipe Nini Sasa zaidi ya UHAI tu
Mungu akubariki asee
 
Ndio mnavojidanganya, eti mtafanya serving, serving ya nyokwe! Kuna vijiji tuu kufata huduma nauli boda elfu 30, wakati mtu anatoka chanika to makumbusho kwanauli ya buku tuu
Kuna vijiji maji ndoo moja ni 2000
 
Ndio mnavojidanganya, eti mtafanya serving, serving ya nyokwe! Kuna vijiji tuu kufata huduma nauli boda elfu 30, wakati mtu anatoka chanika to makumbusho kwanauli ya buku tuu
Hizo huduma unafata kila siku, mbali na hospital ni huduma ipi utaikosa kijijini.
 
Kwani wanaka kwa miaka mingapi au miezi tu? Wewe unajilinganisha na watu wanao lipwa mshahara na allowance inao zidi kipato chote cha kijiji wewe unaota, kijijini ni nusu jahanamu unaishi kama mnyama wakufuga.
😂😂😂😂 waambie hawa, mtumishi wa kijijini hana tofauti na mfungwa, na tabia zinaanza kubadirika na kuwa kama za mbuzi na pia hata ustaharabu unaanza kupotea.
 
Hizo huduma unafata kila siku, mbali na hospital ni huduma ipi utaikosa kijijini.
Vyakula, pia ukute kituo cha kazi kiko sehemu hakuna nyumba hata za kupanga, inabidi usafiri km10+ kwenda, hapo hakuna daladala kama mjini

Pili ukikuta unakaa huko huko porini kwenye nyumba za kituo, huduma za masoko unazifata 10+ km

Kifupi unaishi kama mnyama

Hayo maji unayosema ni ya bure, unakuta ni ya ma lambo yapo kilometer 5+ ulipo
 
Watumishi wa mjini hawajui ili kila muda ni kuropoka tu mara kijijini kuna fursa mara utapewa chakula bure mara utapewa mifugo bure.
 
Akili zao ni kwamba kijijini hakuna matumizi [emoji1][emoji1][emoji1] kwamba unafanya tuu serving
 
Back
Top Bottom