Kupangiwa kazi vijijini tayari unakuwa umeuliwa kifikra na kitaaluma

Kupangiwa kazi vijijini tayari unakuwa umeuliwa kifikra na kitaaluma

Kama umekulia na kufanya kazi Dar kuna mda unawaza kubadilisha mazingira uwende hata Mikoani huko(Umechoka kuishi mjini)!
 
Kijijini pazuri sana,hakuna kasino(kumbi za starehe),wadangaji,pisi kali,mboga unakula za kienyeji,nyama Hadi sikukuu,chumba 5000,seem ya kazi ni kalibu hutumii garama za usafiri,shamba unapewa bule,ardhi hela ndogo,ukiwa mkulima,mfugaj,mlanguaji mazao nyumba gari ni haraka sana kupata,wale wa mjini sasa tunapanga Hadi kufa
 
Hicho ni kijiji cha ndotoni
 
Nimekaa Kijijini kwa Miaka 2 ila hakuna cha maana nilichofanya, maaana watu ni wale wale, vitu ni vile vile.
Kila kitu kibaya kuanzia maji ya kuogea hadi chakula

Mtu anayesema kijijini kuna fursa za kulima hajui wanavyopitia tabu
Mkuu kuna vijiji upatikanaji wa kila kitu ni mgumu mfano maji,huduma za fedha,chakula, na kadhalika.
Hali hiyo ndio huwa fursa kwa wenye akili za kujiongeza.
Ukiwa ni mtumishi uliyepangwa kijiji cha aina hiyo na ukalalamika maisha magumu nitakushangaaa!.
Mwaka 2012 nilipangwa kazi kijijini yaani ni kijiji chenye changamoto za kila aina -:
1.Hakuna duka linalouza unga wala mchele.
2. Hakuna huduma ya mgahawa ,badala yake kuna vilabu vya ULABU tu!
3.Hakuna huduma za kifedha zote
4. Mshahara ukiingia Watumishi wa sekta fulani mnajichanga mnampa mwenzenu kadi akawatolee pesa.
5. Hakuna maji kabisaaaa hasa msimu wa kiangazi maji pekee yaliyokuwa yakipatikana ni maji ya MVUA!
5. Hakukuwa na maduka wala magenge hata ya kuuza nyanya!
6.Hakukuwa na migahawa wala Mama na Baba lishe

7. Mboga pekee salama ya kula ni kununua kuku na kuchinja tofauti na hapo utakula chakula bila mboga !
SASA MSWAHILI MIYE NIKASOMA MAZINGIRA NIANZE NA MRADI GANI.? Maana FURSA NI NYINGI NA WALIOPO HAWAZIONI!
Watumishi walikua wakipangwa mahala hapo walikuwa ama wanahama fasta na wengine huamua kuacha kazi kabisaaa.
MRADI WA KWANZA UKAWA KISIMA CHA KIENYEJI CHA MAJI NIKAWEKA WEKA PAMPU NIKAFUNGA BOMBA NA KUANZA KUUZA MAJI.

MRADI WA 2. DUKA
Huduma ya pesa.
Mahitaji yote muhimu
Mbogamboga na nyama .
Kiukweli namshukuru MUUMBA niliweza kuanzisha miradi mingi kidogo kidogo na hatimae nikawa na miradi mikubwa ya biashara, kilimo na kadhalika .
Na bado ninaishi huku na maisha ni murua kabisaa sikumbuki ni lini mara ya mwisho kutumia mshahara wangu kwa kununua chakula mavazi na mambo madogomadogo.
KIUKWELI,

KUISHI VIJIJINI NIFURSA !
SHARTI KUU "USIFANANE NAO"!
 
Kwamba hela unahonga sana kwa watoto wakichaga ama??
Tatizo siyo hela.
  • Hakuna ardhi
  • Kiwanja/kiamba KUUZIWA mpaka ukoo uamue nanukoonunaweza kuamua Bado wajukuu wakaja kukuzingua vile vile
  • Biashara huku ni pombe, kitimoto na vyakula vya kuku, na kila mtu anafanya, na wewe chasaka ni ngumu kufanikiwa
  • Ufugaji huku ni mgumu, maana hakuna ufugaji huria, inabidi mifugo yako ukatie majani, na wewe chasaka huna sehemu ya kukata majani inabidi ununue. Hata kuku Chakula Cha kununua
-Huku hakuna shamba kwahiyo huwezi kulima

Usione Kilimanjaro imejaa wazee ukafikiri ni bahati mbaya, vijana wanakimbia huku maisha magumu sana
 
Nimekaa Kijijini kwa Miaka 2 ila hakuna cha maana nilichofanya, maaana watu ni wale wale, vitu ni vile vile.
Kila kitu kibaya kuanzia maji ya kuogea hadi chakula

Mtu anayesema kijijini kuna fursa za kulima hajui wanavyopitia tabu
Mkuu HIMARS upo kijiji gani maana naamini hapo fursa ni bwelele
 
Inabidi fikra zetu tujiulize yafuatayo :-
  • Kwanini unafanya kazi na kwanini kazi fulani na sio kazi nyingine ?
  • Je kazi ni means to an end au unafanya kazi fulani sababu upo enganged kwenye hio kazi hivyo basi bila hata ujira ungeweza / ungependa kuifanya
Majibu yako hapo yanaweza kukwambia kama jamii tumekuwa na utamaduni wa kuweka a Cart before a Horse..., Hivyo usishangae mtu ni Bwana Shamba na analalamika kupangiwa kazi sehemu zenye wakulima na mashamba,

By the way huenda hata baadhi ya vijiji vya leo yana facility kuliko hata miji ya zamani; kama ni habari na connectivity ya dunia yote kinganjani hivyo kuweza kujiendeleza ni uamuzi tu.....

Tatizo siyo hela.
  • Biashara huku ni pombe, kitimoto na vyakula vya kuku, na kila mtu anafanya, na wewe chasaka ni ngumu kufanikiwa
Kwahio bei ni ndogo sababu ya competition ?
  • Ufugaji huku ni mgumu, maana hakuna ufugaji huria, inabidi mifugo yako ukatie majani, na wewe chasaka huna sehemu ya kukata majani inabidi ununue. Hata kuku Chakula Cha kununua
-Huku hakuna shamba kwahiyo huwezi kulima
Ambacho kila mtu anatengeneza na unaweza kununua kwao au hawakuuzii ?
Usione Kilimanjaro imejaa wazee ukafikiri ni bahati mbaya, vijana wanakimbia huku maisha magumu sana
Ugumu wa maisha ni upi ?, Binafsi nadhani ni perspective huenda Kiu yao / their dreams ni tofauti (mchagga na pesa ni pete na kidole vilevile competition ya kuwa nazo zaidi ya mwingine watu wanakwenda huku na kule ku-accumulate pesa / utajiri sababu mwisho wa siku kwao ndio mafanikio / kipimo cha kufanikiwa (ile status ya mmasai na mifugo kwao ni pesa)

Hivyo kwa mtu wa kuridhika umesema kuna chakula, pombe n.k. hapo kasoro niliyoiona ni hospitality kwa mgeni huenda isiwepo wewe usipokuwa kabila hilo na culture hizo huenda ukawa kama mkimbizi; Kwahio utofauti wako huenda ndio ukawa a disadvantage (Na hayo ndio waasisi walijaribu kuyamaliza ili tuwe na umoja wa kitaifa) lakini kuanzia Awamu iliyopita na sasa kuendelea naona kama tunataka kuyarudisha hence kupoteza the only advantage tuliyokuwa nao kama watanzania tofauti na Dunia nzima....
 
Tatizo siyo hela.
  • Hakuna ardhi
  • Kiwanja/kiamba KUUZIWA mpaka ukoo uamue nanukoonunaweza kuamua Bado wajukuu wakaja kukuzingua vile vile
  • Biashara huku ni pombe, kitimoto na vyakula vya kuku, na kila mtu anafanya, na wewe chasaka ni ngumu kufanikiwa
  • Ufugaji huku ni mgumu, maana hakuna ufugaji huria, inabidi mifugo yako ukatie majani, na wewe chasaka huna sehemu ya kukata majani inabidi ununue. Hata kuku Chakula Cha kununua
-Huku hakuna shamba kwahiyo huwezi kulima

Usione Kilimanjaro imejaa wazee ukafikiri ni bahati mbaya, vijana wanakimbia huku maisha magumu sana
Kwa mahali hapo mkuu fursa zipo ila hujaziona niambie ni Kilimanjaro ipi upo na kuna aina gani ya mimea ya kudumu na muda mfupi huko.

FURSA SIO LAZIMA ULIME AU UFUGE
 
Kwahio bei ni ndogo sababu ya competition ?
Bei ni ndogo ya kitu gani?

Possibly.

Yaani mtu akatie majani ng'ombe au nguruwe wake kuanzia mdogo mpaka anapata nyama utegemee Bei itakuwa ndogo?

Kitimoto kilo 8000 tsh, Ng'ombe 8,000 kilo.
Ambacho kila mtu anatengeneza na unaweza kununua kwao au hawakuuzii ?
Kila mtu anaweza kutengeneza Nini?

Sijakuelewa, maana nazungumzia biashara common kwa wenyeji.
Ugumu wa maisha ni upi ?, Binafsi nadhani ni perspective huenda Kiu yao / their dreams ni tofauti (mchagga na pesa ni pete na kidole vilevile competition ya kuwa nazo zaidi ya mwingine watu wanakwenda huku na kule ku-accumulate pesa / utajiri sababu mwisho wa siku kwao ndio mafanikio / kipimo cha kufanikiwa (ile status ya mmasai na mifugo kwao ni pesa)
Ugumu wa maisha ni:
  • Kutegemea Mshahara pekee Kama unao
  • Kununua kilo ya Nyama Tsh 8,000 Tena kijijini
  • Kununua kopo la dagaa wa Mwanza 2500 tsh.

  • Kununua samaki wa nyumba ya Munhu, kipande 2,000.
  • Kupanga chumba kimoja Tsh 40,000 kijijini
  • Kupanga mpaka siku ya kustaafia
Hivyo kwa mtu wa kuridhika umesema kuna chakula,
Chakula ni Bei ghali kuliko hata Dar.
pombe n.k.
Pombe ni Bei ya kawaida Kama sehemu nyingine, na vile vile ni option.
hapo kasoro niliyoiona ni hospitality kwa mgeni huenda isiwepo wewe usipokuwa kabila hilo na culture hizo huenda ukawa kama mkimbizi; Kwahio utofauti wako huenda ndio ukawa a disadvantage (Na hayo ndio waasisi walijaribu kuyamaliza ili tuwe na umoja wa kitaifa) lakini kuanzia Awamu iliyopita na sasa kuendelea naona kama tunataka kuyarudisha hence kupoteza the only advantage tuliyokuwa nao kama watanzania tofauti na Dunia nzima....
👆
 
MoseKing

Ulichosema mwanzo na unachojibu sasa naona kama kuna utofauti mkubwa let me qoute sentensi mbili

  • Biashara huku ni pombe, kitimoto na vyakula vya kuku, na kila mtu anafanya, na wewe chasaka ni ngumu kufanikiwa
Kwahio naongelea hio biashara ya vyakula vya kuku ambayo kila mtu anafanya

  • Ufugaji huku ni mgumu, maana hakuna ufugaji huria, inabidi mifugo yako ukatie majani, na wewe chasaka huna sehemu ya kukata majani inabidi ununue. Hata kuku Chakula Cha kununua
Kwahio mfano ukifuga kuku ambao chakula inabidi ununue ambacho kila mtu anafanya sababu hata wewe ukifanya huwezi kufanikiwa hence supply ni kubwa au ?

Nadhani tatizo kubwa la huko kama nilivyosema mwanzo itakuwa sio ushirikiano / kushirikishwa wewe kama mgeni.... ila technically tukienda word by word kwa ulichoandika your argument does not hold water....
 
Vingi ni kweli, lakini mara yako ya mwisho kufika hapo ni lini? sahv pamechangamka kidogo mkuu
Mkuu yale maeneo bado nanda hata sasa hivi ardhi ekari moja wanauza kwa laki mbili tu. Maji kiangazi hiki hayapatikani ktk kijiji cha rutoro. Ukienda mishambya yaleyale, kyarutare, kyobuheke na byengeregere ndiyo usiseme kabisa.

Kata yenye ukubwa wa mamia ya kilomita za mraba haina hata zahanati. Kuishi kule ni sawa na kuishi jehanamu ya duniani. Naamini wanaoishi huko Mungu kashawasamehe dhambi zao maana wanaishi jehanamu.

Mvua ikinyesha njia hazipitiki kiasi kwamba mwendo wa kilomita kumi unaweza kutumia muda wa masaa mawili kwa pikipiki kisa utelezi.

Hewa ya kule ni nzito utadhani kuna mtu ameminya pua usipumue kwa sitarehe. Maeneo hayo nayafahamu sana sababu nimewahi fanyia kazi huko sina hata hamu nako kabisa.

Wanaosifia vijijini waende maeneo hayo wake hata mwezi mmoja tu halafu warudi kutoa ushuhuda.
 
Ni kweli mkuu
Enzi hizo nikiwa bado msaga mashine wa kijiji kule kijijiji kwetu nimewala sana waalimu wapya maana mie ndo nilikuwaga mjanja mjanja ambaye niliwahi kufika Dasilamu[emoji38]
Dasilamu oyee😂😂😂, kumbe stori za kidibwi mnapendaga
 
Back
Top Bottom