Umeongea vizuri mnooo, na hiki ndicho ambacho watu hawakioni au wanajifanya mbuni... Mimi miaka ya nyuma nimefanya kazi vijijini na niliweza kupata mashamba ya kutosha, tena mazuri, mengine yana matunda yanayozaa kama miembe, machungwa, machenza, migomba nk... Nimeuziwa nyumba iliyojengwa mpaka kwenye lenta iliyoko kwenye eneo la heka 3 kwa bei chee na ya kulipa kwa awamu. Leo ukifika hapo kwangu shambani unaweza kudhani mimi nilikuwa tajiri mkubwa kumbe walaaa.... Wanakijiji ukiishi nao vizuri, akiwa na shida atakutafuta ili kama utapenda kununua mali yake akuuzie. Mimi kwa sasa niko mjini, lakini kule kijijini kwenye mji wangu huo nakutegemea mnooo na sijawahi kujuta.