Kupangiwa kazi vijijini tayari unakuwa umeuliwa kifikra na kitaaluma

Kupangiwa kazi vijijini tayari unakuwa umeuliwa kifikra na kitaaluma

Kijijini Kila kitu bure kuanzia kuni,maji, chakula unaweza pewa na wanakijiji inategemea na UKARIBU nao, nyumba bure za Serikali au Kodi chini chumba za kisasa hakizidi elf 20,hakuna nauli,mjini mfanyakazi wa chini bila elf 10 ajatoka na kurudi jioni kwake kwa mshahara wa laki 7 wa mjini bila rushwa amalizi mwez wa kijijini mshahara unakutana.
Ulimwengu huu wa internet unakuaje masikini Sasa huku umezungukwa na fursa.
Utakuwa masikini Kama utaki kulink na external world
Internet inaleta pia?
 
Hivi wewe umewahi Fanya kazi kijijini? Unavifahamu vijiji vya mkoa wa Simiyu au shinyanga? Huku wenyeji hawataki muona mgeni akifanikiwa uchawi Kila Kona tena hadi watumishi wanatumia ndumba hasa wenyeji wa huko unakuta Kijiji kina kaya 400 katika hizi kaya 97 ni za waganga wa kienyeji kaya 250 ni wachawi kaya zilizobaki ndo Zina ahueni umasikini ni WA kutupa halafu kuna mtu anasema vijijini kuna fursa ninawasi wasi utakuwa umetembelea vijiji vya DSM pekee! Kuna vijiji huku greda halijawahi fika kuna Barbara za ng'ombe tu usiombe upate dharula wakati wa masika utajuta.
Mshamba wa Dar atakwambia kijijini kuna Fursa...... fursa ukiwa na hela sio pa kuchomokea
 
Inaonekana wewe ulikuwa mvivu au hukuipenda kazi ya Ualimu.
Vutu unavyolalamikia ulikuwa utaratibu wa kawaida kabisa ila wewe unaona kama vike ulionewa
Ningebaki kule sasa hivi ningekuwa nimezeeka😅😅😅
 
Eee nshawahi kuwa mwalimu bana sisee hapakuwa mbali na mjini ila vimbi kha!

Ukisikia mtu ni mwalimu mpe heshima zake mimi yalinishinda.

Sijui mnanielewa ama? Ati wanafunzi wakifunga mimi nibaki maeneo ya shule yaani siwezi kwenda nyumbani kama sina likizo ati nibaki nareport shulen kila siku 🤣

Kubwa kuliko yote nikibaki shulen kumbuka wanafunzi wako likizo shulen nakutana na mbuzi ndo zinakuwa zinazunguka viwanjani nyieeee!

Kuandaa sijui assessment sijui ya mwaka sijui nini dah!
Kunifanyia eti kukaguzi wa kustukiza tena niko darasani, siku hiyo nilimuacha darasani nikawaaga wanafunzi nikawaambia sijiskii vizuri.

Bado kufika kazini ikishafika saa 7:30 kitabu cha kusaini kusharudishwa kwa HM

Vumbi la barabarani nikiwa naenda kazini nyieeee!

Wachawi kulala wananiniga usiku!

Niliandika barua ya kwenda masomoni na ndo ukawa mwisho wa ualimu.

Nyie heshimuni watumishi walioko vijiji hasa walimu dah.

""Niliandika barua ya kwenda masomoni na ndo ukawa mwisho wa ualimu.""
Kwasasa wewe ni nani?

#YNWA
 
Kwani maisha ni taaluma tu huwezi kulima kufanya biashara na nk acha kukariri maisha popote
 
Upo sahihi kabisaaa

Wale wa Halmashauri za Wilaya zile ngumuuu kama

1. Ukerewe
2. Momba
3. Mpimbwe
4. Mlele
5. Tanganyika

Watakuelewa vizuri sanaaa. Ukiwa halmashauri hizi Kutoboa ki exporure, academic na financially ni taabu sanaaaaaa.

Raia wa humo huwaza kulima na kufuga tu.

#YNWA
YNWA
 
Back
Top Bottom