Kupasua Chungu na kufunga kwaajili ya kesi ya Ugaidi ya Mbowe kuna madhara kwa wasiotenda haki na vizazi vyao?

Hii ngoma kama ikielekezwa kama ilitotumwa /ombwa kwa mizimu na ikajibiwa kama ilivyoombwa kwa kweli itaondoka na vizazi kwa vizazi.yaani isikieni tuu kuna familia huko zimeteketea nyumba haziishi watu vizazi vineangamia kwa hili jungu
 
Chadema mnahangaika sana!
Mlipofurahia Sabaya kufungwa kimizengwe sasa ni zamu ya mwenyekiti Mbowe.
Acheni mahakama ifanye kazi yake.

Una uthibitisho kuwa Sabaya alifungwa kimizengwe??
Ushahidi wa ujambazi wa sabaya na mateso aliyokuwa akiwapa watu upo wazi!
Sabaya siyo jambazi tu bali yeye ndiye tafsiri halali ya gaidi!
 
Tuletee proof na sio story za vijiweni magufuli alijiekea kinga coz kuna watu aliowatumbua walitaka kummaliza. Na wamefanikiwa na baada ya hapo wakataka waue image yake
Kinga dhidi ya kuvunja katiba sio ma bodyguard. Kama walifanikiwa kummaliza basi wana akili kumzidi japo alikuwa na dola.
Mjini kuna wenye mji ukifika waheshimu, hata Nyerere alijua hilo japo nae alikoswa koswa mara 2.
Mji mkubwa huu.
 
Ndugu zangu, siku zote, MUNGU husimama upande wa yule anayeonewa yaani mwenye Haki. Kama kweli wanambambikia kesi Freeman, hata wakilogwa, wajue Mungu hayuko upande wao. Wakivunjiwa vyungu hakika wataumia.
 
Chadema mnahangaika sana!
Mlipofurahia Sabaya kufungwa kimizengwe sasa ni zamu ya mwenyekiti Mbowe.
Acheni mahakama ifanye kazi yake.
kuna kesi mpya ya ubakaji ya Sabaya inakuja , sisi tutaendelea na mila zetu za kupasua chungu na kufunga , mwaka huu ukiisha salama kabla mtu fulani hajapinda mdomo sijui !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…