Tetesi: Kupata samaki Kanda ya Ziwa ni kama Almasi, waziri ndivyo tumekuwa tukiishi siku zote?

Mimi naishi Kanda ya Ziwa hakuna taarifa kama hiyo. Mhe.Mpina kaza kamba ili samaki waongezeke.
Mbuge yule Wa Geita Musukuma alisema bungeni. Samaki ni bidhaa adimu kanda ya ziwa. Akamsema waziri aache mihemuko.
Waziri akajibu kuwa kuna viongozi Wa kisiasa ni wavuvi haramu. Na musukuma akiwemo.
So, ukweli upo hapo.
 

Tuache siasa katika maswala ya maendeleo.

Hakuna ubishi kuwa uvuvi haramu, pamoja na uchafuzi wa Ziwa Victoria, siyo tu unatishia uhai wa viumbe majini, umesababisha madhara makubwa ya kijamii na uchumi. Kama ni mwenyeji wa eneo hilo unajua nina maana gani. Kuna aina za samaki hazionekani kabisa, au ziko chache sana.

Ni hatua sahihi zinazochukuliwa na Wizara husika ili uhai wa Ziwa urejee katika hali yake stahiki, kabla ya kuruhusu uvuvi unaosimamiwa. Isitoshe samaki huzaliana sana na hukua katika kipindi kifupi kisichozidi miezi 6.

TUWE NA SUBIRA TU kama tulivyovumilia vyuma kukaza. Tusisubiri hadi Ziwa limeharibika kabisa, ndiyo tuanze kulaumiana na kuishutumu Serikali kwa kutokuchukua hatua mapema.
 
Yani Acha huku Kilimanjaro ni majanga. Samaki hatuli tena maana Nyumba ya Mungu imefungwa, ukikutwa na samaki no shida Kubwa. Wananchi wa Hali ya chini tupo matatani. Nadhani serikali ingekuwa inafunga upande mmoja mwingine uachiwe ili wananchi wapate Kitoweo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…