Tetesi: Kupata samaki Kanda ya Ziwa ni kama Almasi, waziri ndivyo tumekuwa tukiishi siku zote?

Tetesi: Kupata samaki Kanda ya Ziwa ni kama Almasi, waziri ndivyo tumekuwa tukiishi siku zote?

Mimi naishi Kanda ya Ziwa hakuna taarifa kama hiyo. Mhe.Mpina kaza kamba ili samaki waongezeke.
Mbuge yule Wa Geita Musukuma alisema bungeni. Samaki ni bidhaa adimu kanda ya ziwa. Akamsema waziri aache mihemuko.
Waziri akajibu kuwa kuna viongozi Wa kisiasa ni wavuvi haramu. Na musukuma akiwemo.
So, ukweli upo hapo.
 
Inauma sana tunakoelekea, hata kma ni kutaka sifa za vyeo lkn tutaumizana kwa style hii. Nasema ni kama tetesi kwa savabu siamini hiki nilichoambiwa, labda nipate na uthibitisho kutoka kwa watu wa humu jukwaani ambao wameenda huko na kushuhudia hii hali. Iko hivi, Kuna rafiki yangu yuko huko kanda ya ziwa, nimemwambia ukiwa unarudi mkuu, nikutumie hata ka ten unichukulie hata dagaa (vimena), jibu alilonipa ni kwamba gari ikipigwa mkono, unashuka na begi lako kukaguliwa hivyo anaogopa kuchukua chchte kwa jina la samaki kutoka kanda ya ziwa, je, hivi nyie mnaotufanyia hivi mnataka wananchi wa kawaida tuishije, hata dagaa ni ishu sasa, hadi imeshoot bei juu, hlf Waziri anayehusika anatokea huko huko kanda ya ziwa, amejitoa ufahamu bila kujua kuwa watu wa hiyo kanda tegemeo lao kubwa ni samaki..niishie hapo.

Tuache siasa katika maswala ya maendeleo.

Hakuna ubishi kuwa uvuvi haramu, pamoja na uchafuzi wa Ziwa Victoria, siyo tu unatishia uhai wa viumbe majini, umesababisha madhara makubwa ya kijamii na uchumi. Kama ni mwenyeji wa eneo hilo unajua nina maana gani. Kuna aina za samaki hazionekani kabisa, au ziko chache sana.

Ni hatua sahihi zinazochukuliwa na Wizara husika ili uhai wa Ziwa urejee katika hali yake stahiki, kabla ya kuruhusu uvuvi unaosimamiwa. Isitoshe samaki huzaliana sana na hukua katika kipindi kifupi kisichozidi miezi 6.

TUWE NA SUBIRA TU kama tulivyovumilia vyuma kukaza. Tusisubiri hadi Ziwa limeharibika kabisa, ndiyo tuanze kulaumiana na kuishutumu Serikali kwa kutokuchukua hatua mapema.
 
Yani Acha huku Kilimanjaro ni majanga. Samaki hatuli tena maana Nyumba ya Mungu imefungwa, ukikutwa na samaki no shida Kubwa. Wananchi wa Hali ya chini tupo matatani. Nadhani serikali ingekuwa inafunga upande mmoja mwingine uachiwe ili wananchi wapate Kitoweo.
 
Back
Top Bottom