Kupatiwa mawazo juu ya afya yangu

Naxria abdalla

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2025
Posts
204
Reaction score
379
Habari zenu wana jamvi leo nimekuja kwa unyenyekevu mkubwa ndugu yenu naumwa hlf sijui nini kinanisumbua najua itawashangaza ila na huu ukubwa nilonao sijui naumwa nini ni vile najiskia vibaya mwili unakosa nguvu mda mwengine viungo vinauma tu mda mwengine kama nataka kutapika inafika mwezi wa 4 nikienda hosptal za serikali wananipima tu malaria wananipa dawa hakuna afadhali ninayopata,sasa nimeamua kwenda hosptal za binafsi ila kabla sijaenda nataka ushauri vipimo gani niombe kufanya au doctor nikimuelezea ataelewa nini anipime?mana nateseka mno
 
Ila Tanzania ni nchi ya kipekee sana

No wonder watawala waovu wanafurahia aina hii ya watu tulivyo haswa sisi vijana wa kileo

Yani mtu anasumbuliwa kwa namna isiolezeka na inampa wakati mgumu badala akafanye full check up eti anakuja kutafuta faraja humu ndani.

SCUM! 🤡🤡
 
Pima vidonda vya tumbo, hizo ulizotaja zote ndio dalili zake
 
Watanzania wengi tunapona bila kutumia dawa au kwa kutumia dawa za kienyeji... Hali ikiwa mbaya ndipo mtu anakimbilia hospital 😊
 
Wewe ungetoa tu ushauri bila kuhusisha nchi kwani ungebadilika nini?wewe alokwambia mm nimekuja kutafuta faraja ni nani?au nimeandika wapi kama nataka faraja?hebu ishia apo nisije kukwambia maneno mabaya ukanichukia
 
Kama umekutwa na marelia tumia sindano

Hizi dawa za 2000 acha nazo

Pia nenda,hosptali inayoeleweka kubwa
 
Pima Presha, Sukari, Mimba, UTI, Typhoid, H pylori...
 
Hakikisha unapima na upungufu wa kinga mwilini mkuu..pole kwa changamoto
 
Una vidonda vya tumbo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…