Asalam Ailekum wandugu,
Nahitaji mtaalam wa kunifanyia makadirio ya ujenzi wa nyumba hususan kupaua kwa kutumia bati. Nyumba ipo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Natanguliza Asante.
--------------------
Nahitaji mtaalam wa kunifanyia makadirio ya ujenzi wa nyumba hususan kupaua kwa kutumia bati. Nyumba ipo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Natanguliza Asante.
--------------------
usihofu mama, iko namna hii,
Nyumba ina sehemu kuu 3
sehemu ya kwanza ni msingi
sehemu ya pili ni boma na
sehemu ya tatu ni paa
kati ya hizo sehemu kuu 3 sehemu ya msingi na sehemu ya paa ni part 2 zinazohitaji umakini sana na zinakuwa na gharama kubwa kidogo,
sehemu ya paa ni part inayotumia skilled labour na ni sehemu yenye risk,
mbali ya swala la kiufundi, paa kwenye nyumba ndo linaweza kubadilisha nyumba iwe nzuri au iwe mbaya,
sasa natoa mfano tu wa nyumba ndogo ya vymba 3 vya kulala, sitting room, dining, kitchen na store jumlisha veranda zote za mbele na nyumba, chukulia mfano hiyo nyumba ina jumla ya ukubwa wa 140sqm,
kutegemea na aina (design) ya hiyo ramani na paa lake labda paa lina ukubwa wa 270sqm
mahitaji ya kupaua mfano wa hiyo nyumba yapo kama ifuatavyo.
1), mbao za dawa, hasa mbao nzuri ni za SAO HILL, kama bati litatumika la Industrial Trough (I.T) (hilo ni bati la migongo mipana, manake mbao za papi hazitakuwa nyingi kama mbao za makenchi, hapo kwa SAO HILL ukubwa wa nyumba kama hiyo (tunayo'assume) jaribu kutenga pesa isiyopungua 3m za mbao tu
2), Bati kama nilivyoainisha hapo juu ni I.T mfano na running meter ni 270 , kwa mabati ya ALAF ya IT gauge 28 wanauza kwa meter moja 13500/= kupitia agent, bila agent ni 13800/= manake ni kwamba bati tu hapo litagharimu karibia 4m
3), kofia na valley labda zipo jumla 40, kofia moja wanauza 21,000/= (hizo ni kofia zenye urefu wa 3m,
manake kofia na valley zinaweza kugharimu karibia milioni moja
4), mengineyo kama misumari ya kupigia makenchi, misumari ya bati, usafiri vyote kwa pamoja weka milioni 1
5), ufundi (tafuta local fundi) labda akakufanyia kwa bei ya 2m,
ila ukumbuke local fundi akija anaagalia nyumba imejengwaje na anabuni tu namna paa litakavyokuwa na si kwa kuffuata ramani inaonyeshaje, tarajia makosa mbali mbali hapo, ila pia na ushauri atakaokuwa anakupa local fundi ujue unaweza kukugharimu wewe baadae nakubaki kulalamika kuwa nilishauriwa hivi na fundi,
kwa maelezo zaidi ni'PM email yako ntakutumia sample za ramani na budget zake na ukipenda unaweza kuzitembelea kama upo hapa dar, au mwanza, arusha na moshi,
Nyie mnafanya masikhara na paa,jamaa yuko sahihi kabisa,mi nimegonga paa imekula karibu mil 22,nyumba ya mita 17 kwa 21,nimepiga bati ya Kigae ya Jeshini mbao tu imekula 8M,Bati 6M,kofia 1.2 M,Misumari special ya Bati 0.7M,Misumari ya kawaida ya mbao 0.5M,Kofia na Valley 1.2M,Usafiri na Vibarua kwenye mbao,bati,kofia na valley jumla 1M,Ufundi 2.8M.
Msilalamike sana upauaji unategemea mambo mengi kwa mfano ukubwa wa nyumba,aina ya bati,idadi ya mbao,ramani ya paa etc,kwa mfano mtu aliyepiga bati la kawaida,bati la migongo mipana,bati la kigae na kigae hawa lazima watofautiane bei,vilevile bei ya mbao na ufundi wa bati la kigae na bati la kawaida haiko sawa bati la kigae linakula mbao nyingi zaidi,ukubwa wa nyumba ya sqm 140 hauwezi kuwa na gharama sawa ya upauaji na nyumba ya sqm 240, vilevile ramani za paa nyingine ni very complicated kwamba upauaji wake ni mgumu sana hauwezi kuwa bei sawa na mgongo wa tembo,sijui kama mnanielewa?ila kama hamkubali sio kesi nadhani kuna ambao wanaweza kunielewa hata kwa mbali sina la ziada ni hayo tu.