Kupaua nyumba (Makadirio ya gharama)

Dena Bura

Member
Joined
Mar 7, 2011
Posts
15
Reaction score
24
Asalam Ailekum wandugu,

Nahitaji mtaalam wa kunifanyia makadirio ya ujenzi wa nyumba hususan kupaua kwa kutumia bati. Nyumba ipo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Natanguliza Asante.


--------------------


 
Nyumba ina ukubwa gani? Hata hivyo andaa fedha za mbao treated timber kama 3.5m na bati 5m na ufundi 3m, kama hujapata fundi ni PM nije nicheki site then tutaongea.
 
nyumba ina ukubwa gani? hata hivyo andaa fedha za mbao treated timber kama 3.5m na bati 5m na ufundi 3m, kama hujapata fundi ni PM nije nicheki site then tutaongea.
,

Umetisha,
Hata ukubwa wa nyumba hujaufahamu/hajakupa umetaja bei. Unamaanisha nyumba yenye 100sqm itagharimu sawa na nyumba yenye 250sqm? Vipi kuhusu aina ya mabati anayotaka kutumia - bei yako inakuwa sawa kwa mabati ya aina zote?

Anyway: Mimi pia nipo nahitaji gharama za kuezeka nyumba iliyopo Makongo (DSM) yenye sqm 200. siyo ya ghorofa, bati za wanazotengeneza ALAF (za rangi).
 
Mkuu nimejaribu tu ku'assume nyumba yake ya kawaida around 120sqm to 140sqm na bati la Alaf au Ando ambazo kwasasa ndo kama fassion.
Mkuu ufundi wa kuezeka tu mil 3? @zembemkuu
Mkuu nyumba ikipauliwa vibaya hata iwe imejengwa vizuri namna gani na kufanyiwa finishing nzuri namna gani itachukiza kwenye macho ya watu tu. 3m ni gharama ya kawaida kabisa,
 
mie nguvu zikaniishia kabisa maana ndo nitakaribia stage hizo sasa huku sikutishana uku.
Usiogope maana hata majibu yenyewe hayaja dadavua vizuri, mfano hizo bati za kisasa lazima ujue vipimo halisi na aina la paa sasa hapo sijui ametumia vipimo gani, pia ikijulikana aina ya paa itasadia kujua mbao kiasi gani na za size gani
 
Asante Dancani maana hela ngumu hii, taarifa za wadau wengine wenyw uzoefu ni muhimu
 
Mkuu kupaua gharama ndiyo maana nyumba nyingi zinakwama kwenye linta.

Sio kwamba nigharama sana sema huwezi piga kench ukae baada ya miezi saba upige bati no unatakiwa uwe nayo kwa mara moja yote pesa ya bati fundi na mbao ndiyo maana kuezeka ni tabu tupu but for 3 M too much may be 4 times that the supposed price
 
Jamani kupaua ni gharama kuna rafiki yangu alitajiwa jumla ya 17M (ufundi, mbao, bati-ALAF, ukubwa around 15x20). Hapahapa DSM, Akaomba apunguziwe walau 14, ikashindikana. Akaahirisha. Kama huyo rafiki yangu akiiona hii post, atampigia huyu jamaa mara moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…