Mpende jirani yako kama nafsi yako. Malawi ni jirani yetu ni wajibu tuwasaidie hata kama tuna shida zetu. Uungwana wetu na upendo wetu kwa Waafrika wenzetu ni jadi na utamaduni wetu kama Taifa.
Kusaidiana kupo na ni vizuri ukamsaidia jirani yako apatapo shida. Kama baba/mama mwenye nyumba utaonekana kituko kusaidia jirani wakati ndani kwako hakuna chakula cha kutosha kushibisha wanao
Ila kuchangia wakati watoto wako wanakalia mawe madarasani (kwa kukosa madawati) na kuwafanya wafeli na pengine kuharibu maisha yao yote; nafikiri tunatakiwa tuliangalie vizuri.