Surya
JF-Expert Member
- Jun 7, 2015
- 8,774
- 13,566
Sijui wangapi watanielewa lakini kiukweli kupenda kunatesa jamani
Nina falsafa yangu huwa naisema sana kujikumbusha lakini bado hata mimi najikwaaa.
"What you Love, is what will make you suffer. "
Kile unachokipenda ndio kitafanya uteseke..
kuteseka nikimaanisha kuutesa mwili na Akili.
Udhaifu wangu ni kumpenda binadamu mwenzangu. kwa wengi raha ya maisha ni kusifiwa, kuwa mtu mashuhuri, mcheshi na wakutegemewa sana.
Kutamani vingi hivyo sikutaka kabisa, nilitamani sana walau niwe na marafiki wachache tu tutakao aminiana sanaaa Lakini hayupo hata mmoja.
Sijui ni wangapi wananielewa, mm sijawa mume wala baba wa yeyote.
Nitumie neno BFF best friends forever, Kuna raha yake ya pekee kuwa na mtu hata mmoja ambae ni best friend kwako, mshauri na mtu mnae elewana sana. Lakini hayuko.
Mungu pekee anachukua nafasi hiyo lakini bado nahitaji binadamu mwenzangu.
Bible story.
mahusiano kati ya roho na roho ni janga kubwa.
Mungu alipojaribu kutengeneza mahusiano na Mwanadamu.
Mungu alilichagua taifa la Israel na kulitoa utumwani kwa uweza na ukuu mwingi kama alivyotoa ahadi yake kwa baba yao Ibrahimu, lakini kwa wakati mfupi taifa hilo lilisahau yote hayo na kutengeneza miungu mipya na kuabudu, Biblia inaita Uzinzi, kumuacha Bwana wako na kuelekea miungu migeni.
Mungu alikasirika sana hadi kumwambia Musa nataka nikiangamize kizazi hichi kilicho niasi na nitakufanya wewe Musa kuwa taifa kubwa.
Sasa uzuri ni kwamba Mungu anaweza kusamehe uovu wowote, tofauti na mm mwanadamu nikiumizwa na binadamu mwenzangu aliyekosa uaminifu inauma sana.
Pengine ni bora kujaribu maisha ya peke yako lakini bado hayana furaha, binadamu tunategemeana kwa kiasi kikubwa sana.
Kuna video nimesikiliza ya kijana mmoja anatamba Tiktok kwa kuringishia Utajiri na anajiita Tajiri na kuwaambia vijana wengine watafute hela,
cha ajabu na pesa zake hata ukichunguza kauli zake utagundua kapitia maisha ya msoto na kukataliwa na watu, kidonda hicho hakijapona bado, aliwahi kulelewa na mwanamke ambaye waliachana pindi akiwa bado yeye hajatusua.
Ukimsikiliza huyo kijana utagundua kitu.
Tumekatishwa tamaa na tuwapendao lakini bado tunarudia kupenda 😭😢
Love is a beautiful thing created by God.
na hata yeye mapenz yamemtoa jasho