Ukweli ni kwamba Mungu mwenyewe aliweka kitu kinachoitwa love/upendo kwa viumbe wote ili iwepe furaha na amani ndio maana kama umewahi bahatika kuishi na mtu mliopendana kweli kuna raha ambayo unaipata hakuna mfano,kwanza unakuwa ni mtu wa furaha,moyo wako hauna vinyongo wala chuki,amani ya moyo,utulivu wa akili kiufupi love ni dawa ya majanga yote haya yanayotokea duniani
ila shida ilikuja pale watu walipo anza kutumia love kwa mambo yao binafsi na wengine wakaenda mbali wakaingiza vigezo vya mtu kupendwa au kumpenda mtu
mara sijui uwe na pesa,uwe mrefu,uwe na shepu namba nane,uvae nguo fulani,sijui uweke nywele mtindo fulani vigezo vyote hivyo ni kutokana na kupotea kwa upendo miongoni ya watu
Hii imepelekea watu kuanza kuweka vitu feki kwenye body zao na kufanya visivyompendeza Mungu yote hayo ni kutafuta true love lakini wapi bado mambo magumu kila siku binadamu tunajifunza ubinafsi na kuwa watu wa maslahi
Kwa Sasa wengine wemeshakata tamaa na true love kama mtoa mada hapo ameanza kuona true love ni kama virus furani hivi na kiukweli ukiangalia sasa kupenda now days imekuwa ni hasara ya maisha kutokana na ubinafsi kuzidi mioyoni miongoni ya watu
Hatakama Yote hayo haitabadilisha ukweli kwamba true love ipo na ndio dawa ya majanga yote hapa dunianiš