Kupigwa na Kalynda sio mwisho wa utapeli Tanzania, bado tutapigwa sana

Kupigwa na Kalynda sio mwisho wa utapeli Tanzania, bado tutapigwa sana

2019

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,130
Reaction score
4,735
Nasema haya najua kuna watu watapuuza ila baadae ndio wataelewa.

Kwanza kabisa hawa matapeli wana mbinu kama za shetani...kivipi? Shetani ili akupate hawezi kuja mwenyewe sababu utamwogopa na hutamwaanini,lazma aje kupitia marafiki na watu wako wa karibu yani unaowaanini.

Hivyo hivyo hizi kampuni za investments sijui network marketing lazma mtu atakaekuunga awe mtu wako wa karibu huenda hata kwa msisitizo akakukopesha msingi wa kuingia.

Majamaa yana akili yana,hapa ndio ile kauli TOA PESA UPATE PESA. Mwanzo wa kupigwa mm,nilipigwa kwenye sky investment 10$ 2018 ikaniuma kimtindo muda ukapita,hawa kalynda wamekuja kama kwa kasi ya 5G na mbinu ya mbawa mwitu alievaa ngozi ya kondoo.

Wamekuja na mtaji,wana vielelezo vyote vya serikali,wamepanga ofisi kwenye jengo lenye hadhi,kubwa kuliko wamelipia matangazo kila kona kwenye televisheni na barabarani. Kwanini usiwaamini?.

Tusema mwekezaji alikuja na msingi wa milioni 500 kugharamia vibali na mishahara ya wafanyakazi kwa miezi 3 au 4. Aya akapata members 100k tufanye kamadirio ya chini kila mtu aliwekeza 20k tu.
50000×50000=2,500,000,000-500,000,000 faida 2bls

Binafsi nilingii ila kwa tahadhari,sababu huwa najiuliza swali moja tu. Unaweka pesa unapata faida 4% kila siku akija tajiri akaweka bilioni 2 faida yake kwa siku shilingi ngapi? Bila usumbufu wa TRA manispaa mara kodi ya pango na wafanyakazi kazi gharama za uendeshaji wa biashara. Si kila mtu angewekeza huko?

Hizi kampuni kuwekeza huko ni kama kubet tu,wa kwanza watapiga ila wa mwisho watapigwa tu. Hakuna anaeweza kufanya biashara bila kupata faida.

Kalynda wameondoka watakuja wengine kwa mbinu nyingine mpya na za kuvutia zaidi kama za kweli kabisa na bado watanzania tutapigwa tena. Asanteni na pole yetu tuliojilipua na kula na kusepa.
 
Kupigwa kupo kwingi tu

Kuaminishwa unapendwa kumbe mizengwe tu
Kuaminishwa nyongeza 23% afu ndo vile Tena
Kuaminishwa ni bikra kumbe kapaka malimao
Kuaminishwa ataishi nawe daima ukimwoa anadai talaka Ili mpasuliane Mali
Kuamishwa upo peke Yako kumbe mpo debe
Kuaminishwa unatafutiwa Kaz then unaambulia block
Kuaminishwa yeye ni mtulivu ila unaambulia fungus

Kuaminishwa hajawahi zaa kumbe Watoto wapo Kwa bibi,dada,vituo vya Watoto yatima
Kuaminishwa yeye ni kiongoz Bora kumbe wako Sawa tu tofauti Yao ni jinsi
 
Nineipenda hii
 
Kweli aisee,tusiwaone waliopigwa na kalynda kama wajinga .Wengine wanapigwa nauli kila siku na wadangaji.Viongozi wetu pia wanatupiga tu,iwe cash au kura kwenye sanduku.Wizi mtupu!
 
Kweli aisee,tusiwaone waliopigwa na kalynda kama wajinga .Wengine wanapigwa nauli kila siku na wadangaji.Viongozi wetu pia wanatupiga tu,iwe cash au kura kwenye sanduku.Wizi mtupu!
Dunia ya sasa ukikaa vibaya unapigwa tu
 
Kuna interview moja romy jones kafanya na Salama alikuwa anaulizwa ilikwaje ukaingia kwenye kutuma madawa ya kulevya lile jibu lake mpaka leo nakubaliana nae

Alisema mjinga hawezi kutumia madawa ya kulevya ila ukijifanya mjanja unataka kutest kila kitu basi utaingia tu kwenye uraibu wa madawa
Na hata kwenye haya mambo ya mr kuku qnet pamoja na kalyanda wengi ni wasomi ukiwa mjinga kila kitu unaogopa ila wajanja ndo wanapigwa hapa kwenye issue hzi.
 
Mchezo wowote unao husu hela huwa sichezi
 
Mtapigwa ww na familia yako.usiniweke na mm sw
 
NCHII INA WAJINGA NA WPMBV WENGI SANA,NA NI MTAJI MZURI SANA KWA HAO WATU AINA YA KYLANDA
NGOJA WAJE WENGINE WAJIPIGIE

ova
 
Dah! Jamani Kalynda!! Bado kuna wengine wako Kwimba ngudu mkoani Mwanza wanaitwa " Timiza ndoto zako" nao wana nyaraka zote za serikali wakihamasisha pesa inazaa pesa baada ya siku 3 mfano ukiwekeza 100,000 baada ya siku 3 unapata 200,000, nchi huu uhuni na ulaghai umezidi aisee!
 
Ziko nyingi hizi.
Mbona wengine ni wazoefu tu wanapiga huko za kimataifa kimya kimya na kuugulia maumivu kimya kimya wakipotea?

USHAURI.
Biashara yoyote ni Risk hilo huwezi epuka cha msingi ni kujua muda sahihi wa kuingia.

Online business ndio new generation kwenye biashara. Tukipata mda tusome zaidi.

Crypto haiepukiki. Jikiteni kwenye elimu ya FOREX mpige na kupigwa wenyewe. Ukishindwa kusoma signal vizuri utayeyusha mtaji mwewnyewe na ukijua kuzisoma utapiga mwenyewe bila kumtegemea mtu.

Tenga mda set hesabu zako kusanya vidola vyako japo 50 kwa siku tulia. Nendeni huko FOREX
 
Back
Top Bottom