Kupika vs kula kwa mama ntilie ni kipi nafuu na kusave hela?

Kupika vs kula kwa mama ntilie ni kipi nafuu na kusave hela?

Inategemea na ukubwa wa familia. Kama upo mwenyewe kula kwa mama ntilie ni cost effective. Pia bei ya kwa Mama Ntilie inategemea. Ikiwa around 2000 kula Kwa mama ntilie unaokoa muda wa kuosha vyombo, kupika etc. Pia kuna socialization yenye faida kwa mama ntilie.

NB; Uwe bachelor
 
Kupika si tatizo ila kuosha vyombo.
Uwiiiii ni shida.
Inategemea na ukubwa wa familia. Kama upo mwenyewe kula kwa mama ntilie ni cost effective. Pia bei ya kwa Mama Ntilie inategemea. Ikiwa around 2000 kula Kwa mama ntilie unaokoa muda wa kuosha vyombo, kupika etc. Pia kuna socialization yenye faida kwa mama ntilie.

NB; Uwe bachelor

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ubora na Kusave pesa kunatokana na Mtu mwenyewe.
Naamini utakuwa kijana wa Chuo mwenye nia ya Kupanga auTayari umepanga.

Nitakushauri kama ifuatavyo.
PIKA endapo;

1.
Mpo zaidi ya Mmoja (wawili na kuendelea).
-Hapo itakusaidia kisave money sana.

2. Upo maeneo ambapo chakula chake ni ghali sana na Ni special kwa ajili ya starehe na sio kwa kijana kama wewe ambae unataka ule ushibe kisawa sawa.
-Mfano Chakula >3000 ni bora upike.

3.Ubora wa Chakula kwa maman'tilie.
Kuna maeneo chakula wanachoandaa unaweza sema ni special kwa nguruwe mf.kipindi nasoma nilipanga Mwenge- Mpakani hawa akina mama wote wabovu kwenye kupika.

4.Upatikanaji wa Chakula.
- Kuna maeneo mengine kupata sehemu wanayouza Vyakula ni mtihani unaweza tembea takribani 1km ndio upate hiyo R& B

5.Kama sio Mvivu Kupika na Kuosha Vyombo

6.Uwe Unajua Kupika.
-Sio unapika Vyakula vya ajabu mara wali mbichi|Boko boko, Mafuta hayaivi n.k

Usipike kama;

1 .Chakula ulipo kinapatikana kirahisi na kwa bei rahisi.
Mfano Maeneo karibu na Vyuo.
Hapo unapoteza muda wako tu.

2.Kama upo pekee.
Usijaribu kupika BUT Jaribu kurejea ushauri hapo Juu uone kama kuna sababu ya msingi inayoweza kuificha|kuiondoa hii sababu.


Nimechoka kutype. (N.K)
 
Kupika chakula cha peke yako gharama sana + muda.
Ingawa ukipika mwenyewe ndio utapata ladha nzuri.
 
Kama ni bachela, pika mwenyewe! Utapunguza sana gharama. Huna sababu ya kula kwa mama ntilie. Halafu unatakiwa ule mara mbili tu kwa siku. (Breakfast plus Lunch) na Dinner.

Viporo kwa wingi! na hayo ndiyo maisha ya geto. Ukipika wali leo, unakula mpaka kesho. Hakuna kumwaga chakula. Vyombo unaosha mara moja tu kwa wiki! Jiko la gesi ndiyo mpango mzima.
 
Kama wewe mwanaume usihangaike,tafuta mama ntilie mtongoze akikubali utaishi maisha yenye raha mstarehe hautajuta,ila ukishindwa kufanya hivyo kupika mwenyewe ni kusev pesa kuliko kununua

Sent using Jamii Forums mobile app
Mhhh, unataka kumwingiza kwenye matumizi makubwa ya pesa, badala ya kupata hyo faida ya kupikiwa na kuoshewa vyombo atajikuta anaongeza na pesa ya biashara Ila kutaka a tena ni kubwa tu..
Kijna mwenzangu nakushauri kama unataka uondokane na kadhia yote hyo bora uoe mazima, kwanza kama Sie waislam ndoa zetu ni za mtu 5 tu imepita
 
Gharama hapo ni kuosha vyombo sio kupwika, bora ukale kwa mama ntilie hautajutia Mzee!!!
 
Inategemea na uko wapi ?? Vyakula vinapatikana kwa urahic , na je unaishi peke yako au uko na watu wengine km upo peke yako ni vyema ukala kwa mama ntile kuserv hela

sent from toyota Allex
 
Aseee kama upo peke ako mama ntilie ndio kimbilio la ku save pesa,Kupika kuna save pesa kama ni mpo kuanzia wa 3 hivi kuendelea ila kama mpo wawili au peke ako asee Tafuta mama ntilie wako Jenga kambi.

Kupika Ukiwa peke ako pika tu siku una hamu ya chakula chako kitamuuuuu kizuriiiii na kweli una hamu ya kutumia Jiko hiyo siku maana siku napika Fujo zake n kama nina wageni mzeee.

Changamoto n 1. "Kuosha vyombo" Aseeeeee hili eneo hili Eee baba 2020 naomba nibadilishe
 
Back
Top Bottom