Kupima uwezo wa Rais Jakaya Kikwete??

Labda ni style yake..wengine wanaiita tolerance wewe unasemaje?, wanafiki wanaomsifia ni kina nani? wakati tunaongelea vitu vinavyonekana kwa macho yenu kila siku...kila mahali unaweza kuficha barabara? unaweza kuficha watuhumiwa wanaohaha mahakamani na kesi?..
 
Mkuu wangu mifano kama hii ndio huniacha hoi kabisa! Lakini yanibidi kukubali kwamba sikutegemea kabisaaa na bado siamini..Ama kweli kila kitu kina sura mbili,
Wadhungu wanasemaga Don't judge a book by it's cover!
 
Mkuu mchango mzuri ila majibu yake kwa ufupi
1. Matumaini > kuliko matokeo hii ni kila mahali hata Obama wamerakani walitagemea makubwa lakini mara nyingi reality is always different from the expectations
2. Maisha bora hii ndugu very subjective kuna improvement kwa watu mbalimbali sehemu tofauti mfano:- walio pata JK loans, waliopata barabara na walienda shule kwa level zote Primary mpaka chuo kikuu nafasi ambazo hawakutegemea kabla....watu wenye access na dispensary kwa kila kata ni maisha bora hayo..usisahau financial crisis lakiniJK amaejitahidi japo anapita kwenye tanuri..lol
3. Ufisadi..gosh! waulize kina yona, mgomja, mramba wanavyohaha kwasababu ya dhambi hiyo ya ufisadi..najua unatamani sana RA,EL awemo kwenye list lakini rais si DPP wala AG hao ndio wataalamu wenye dhamana ya kushitaki au kuacha ...kutegemeana na ushahidi??? get your record right
JK amefanikiwa kwa vigezo vingi japo si vyote...next?
 
..............
Tuangalie mambo mengine mengi anayoyafanya na kufanikiwa mfano:

Kabla ya yote wewe ni mwanasiasa???? au?

a) Kuongezeka kwa enrollment kuanzia primary mpaka university kwa miaka ya ke minne --kielimu siyo mafanikio hayo??


Kuongezeka huko kumeleta manuufaaa gani tupe tasmini kila jambo alilolitenda kwenye elimu na wanafunzi wametoka na kitu gani???? we wasemea enrollment! Je lack of facilities kuwafanikishia masomo yao yaende vyema, hebu nijibu kwa elimu ipi Form 4 anaweza kujiimalisha kiuchumi ktk nchi hii au hata uyo aliyetoka University??? yani usitake niseme namachungu sana mie

b) Kuna program za kujenga zahanati kila kata..kusogeza huduma za afya karibu na wananchi---siyo mafanikio??


Zahanatiiii!!!!!!! teh teh teh teh mkulu mfano Mwananyamara Hospital tu inakasheshe nchi zima inaongoza kwa bad service kikubwa tu vifo vya wamama wajawazito wanapojifungua, hiyo tu tatizo no.1 kwa iyo scandal! wameshindwa kutunga tu sheria na utaratibu wa kumsaidia mtanzania mwenye kipato cha chini ya dolla mmoja na kumpa huduma tu yakumsikiliza nini shida yake???? nurse anataka kujua kama ana hela au raaaah jamani???? Hiyo ni mfano tu hapo ni JIJINI Dar inatokea hiyo tena its not even more than 15Km mahali anapo ishi Rais i mean Nyumbani kwa JK,Iweje leo unategemea huo mpango wa Zahanati utafanikiwa hata japo kwa 30%???? Je huko kijiji Kyela, Mureba,Mpanda, Makete? waambie warekebishe mfumo wa uongozi kwanza na ndio wataweza hilo.


c) Kuongezeka kwa utalii na watalii tangu ashike nchi..siyo mafanikio hayo???


Teh teh Utaliiiiiii unajua nini kuhusu utaliii mpwa wangu? wajua tuna mbuga ngapi weye?Do u know how much Nationa Parks zetu zina earn??? Na ni mikakati gani wanaboresha hizo Parks zetu????? Per Annum twaingiza ngapi??? Uliza South Africa Per Annum wanaingiza ngapi??? Hata tangazo la world Cup kwenye DSstv tu tumeshindwa kuliweka kama kweli kwenye utalii tume perform better,
Mkulu ar u joking au??

d) Barabara za lami mpaka kigoma.rukwa nasikia dodoma-arusha 😕is on track..siyo mafanikio hayo?? kwa miaka minne


we kijana tembea uyaone acha porojo za kusikia kwa Radio au misafara ya hao viongozi. Dodoma Arusha its almost 490km kipande tokea minjingu kwenda babati ovyo tupu na ukitoka babati ndio wamekudanganya na hata kama ikijengwa ni kwaaajili ya siasa kwani uchaguzi ni 2010 walikuwa wapi iyo 4yrs???? na watuambie ni lini watatoka Dar Kuamia DODOMA?????Miundombinu ya DODOMA wataikarabati lini?? Dodoma haiwagharimu chochote mkuuu bali ni urasimu tuuuu, kwanini DAR yani watu hampumui mwang'ang'ania weeee kunani?? yania kiajana achana na ndoto za hao eti watakupotezea ramani zaidi mpwa, Chalinze mzeee ukipita kidogo tu kuelekea segera-tanga wanashindilia rami kama nini badala ya kuipanua kama Chalinze Moro wao wanaongezea rami, nisehemu chache sana tena za kuhesabu ndizo wanazo panua esp maeneo ya vitongoji au makazi ya watu huko porini kupishana tu esp usiku utaogopa mbaya.

e) Uhuru wa habari and tolerance of our president to the freedom of expression..zitto ameliona hili naye..


Hapo sina uhakika sana maaaan uhuru wa kujieleza umepewa nafasi na umejawa na siasa na ahadi za uongo mie kwangu naona ni wanafiki na waaandishi wa habari kila kukicha ni habari za wanasiasa na siasa tuuuuuu hawazungumziii maendeleo hata hayo wewe unayoyadai ati yapo sasa, huo ni ushahidi tosha free media press inaongelea nini sasa??? Au Umedanganyika na PADEPU ile miladi inasimamiwa na UN mkuu na ndio maaana inakwenda sisi tu wenyewe mbinde.

Bana ye mnyonge mnyogeni haki yake mpeni...mlitaka awafanyeje? wana JF mbona hamna shukrani hasa wewe mwanakijiji.


MKJJJ anakuhusu nini wewe umetumwa nini????? defend ur point dnt point fingers tu others Jiulize wewe umeifanyia nini serikali yako mkulu. Nanni mnyonge sasa hapa??????

Pole mpwa
 
Na kweli hivi kwa nini Makao makuu hadi leo hayajahamia Dodoma?
 
Na kweli hivi kwa nini Makao makuu hadi leo hayajahamia Dodoma?

Mpwa upooooo teh teh,

Yani serikali ikulizwa nini kimewafanya mpaka sasa wasi hamie Dodoma hawna jibu hata kidogo mie sioni shida pale. 90's wakati wa Malecela as MP alikuwa anakaaa japo hata kidogo pale Dom sasa sijui yale majengo ni masafi mpaka sasa??

Dom kuna ikulu ya Rais na PM sasa siju wao wanataka nini majumba yapo ya kumwaga viwanja vipo wazi vingi tuuuu.

Tatizo la maji waitafutie sababu hapo kama Pius Mwandu aliweza divert mradi wa maji Shinyanga mjini na akaupeleka Maswa na mpaka leo maswa wanamaji mazuri zaidi ya Dodoma, iweje serikali ishindwe kuweka mitambo ya maji Dodoma?????

Jamani Ivi MUSTAKABALI WA NCHI YETU KTK SEKTA ZOTE ZA SERIKALI NI UPI???

maaana kila kiongozi ajae huja na mustakabali wake sijui huwa wanaufichaga wapi, maaana akija tu ana plan zake amezitoa huko siju hewani mtajionea vituko yaaani umejaaa siasa na si utekelezaji.

Yani
MUSTAKABALI WA NCHI YETU ulitakiwa kuwepo iwe ameingia kiongozi wa CUF,CHADEMA,TLP,CCM etc watakachotakiwa ni kufanya maboresho tuuu ya kiuchumi na kimaendeleo, kielimu na etc ili inchi iende faster wazidiane mbinu za kifikla na sio siasa zisizo na kichwa wala miguuu

hebooooooo

 

Mkuu mambo ya kuangalia na kuona hayapo tena mkuu. Kiongozi yoyote mafanikio yake hupiwa na facts siyo kwa kuangalia tu. Hao wanao tuhumiwa kwenda mahakamani kesi zote ni kiini macho tu. Wangapi umeona wame hukumiwa kwa makosa yao? Ditopile kaua wakaifanya manslaughter. Zombe yuko wapi?

Hizo barabara mkuu pia lete data. Kama kweli zime fanyika haku kosekani data. kajenga barabara ngapi? Ngapi zilikua initiatives zake? Haya mambo ya kuona tu yana danganya sana. barabara zinaweza hata kujengwa bila initiative ya raisi.

Mkuu UDom siyo Kikwete kabisa. That was all Mkapa. Ime kuja kumalizika tu wakati Kikwete ni raisi. Na kuhusu hizo enrollment mtu utaonaje kwa kuangalia tu mkuu? kama kweli zimeongezeka una shindwake kuweka data kwamba kabla ya Kikwete ilikua hivi na baada ya Kikwete imekua hivi? Unataka kuniambia enrollment unaweza kuona imeongezeka kwa kuangalia tu bila data?
 

Umeshasahau kwamba Wanazuoni wa TZ bado wanatumia vigezo hivyo hivyo (bila ya facts) kumsifia Nyerere? Let's look the "history from below" and see who was a better leader between Kikwete, Mkapa, Mwinyi and Nyerere.
 
....... Let's look the "history from below" and see who was a better leader between Kikwete, Mkapa, Mwinyi and Nyerere.

JK Nyerere was the best pamoja na mapungufu yake yaliyokuwepo enzi zake still uchumi ulikuwa pazuri tu pamoja alikwenda vitani. serikali ilikuwa inamiliki sekta au nyanja nyingi za uchumi na kilimo. duh baaada ya kuachiwa mzeee wa ruksa na akafuatia Ben na b ro JK nae mmmhh yetu macho

Thnxk mpwa


 
Crystal and clear good one
 

..acha kupotosha ukweli wewe! barabara gn zilishatafutiwa fedha na kupangwa kutengenezwa,wakati nchi ilikuwa muflisi hoi bin taaban! inflation apprx.49% nchi ina madeni imeshindwa kulipa na hivyo kutokuaminiwa tena na wabia wa maendeleo!!

wewe unaona upangaji wa kujenga highway chalinze-segera badala ya kimara - chalinze ni wa watu wenye akili timamu???

..He s absolutely a failed leader!! labda tuhoji tu na uwezo wake wa kufikiri na kuamua kama kiongozi kwa ngazi ya rais kama bado anao!!
 

hivi unajua maana ya shule wewe?
shule inaweza kuwa hata chini ya mti wa mwembe na wanafunzi wakapatikana na kufaulu vile vile!
 


kamanda unapoteza sana maana ya program kwa ujumla, kujenga barabara ni mipango ambayo huwa ya muda mrefu sana, somtimes huchukua hata miaka mitano kuanza ujenzi, so ukiona sasa kuna barabara za kwenda Dodoma-singida, Arusha-Dodoma na nyinginezo, watu walikaamuda mrefu na kuweka hiyo mipango, so akifanyacho Raisi wetu ni ile implementation ya hizo program, so far mimi naweza kusema kafanya jambo kubwa la freedom of speech, make wakati wa mzee Kipara kulikuwa hakuna kitu hicho, ilikuwa ni mabavu tu, na by this time Tanzania tunahitaji sana freedom of expression ili watu wote waliokuwa wakila bila kufanya kazi basi ukomo ufikie, watambae zao turudi vijana wachapa kazi, wenye vision ya kuindeleza nchi yetu iwe better place for all and not for few kama ilivo kwa sasa.
 
Tumaini, Institution zote hizo PCB (now PCCB), CAG office, Banking systems, investment climate, Macro ecomomic stability etc za utawala wa Ben, to this he deserve his credit. The incurmbent kakuta structures na istutirions ziko in place so much was expected.
 

Prior Master, umezungumzia point muhimu sana... rais wa sasa amekuta everything on track including structures, institutions with surplus.. hivi leo nchi tena ina madeni na haina surplus... huyu hafai kusifiwa .... mi nasema both in macro and micro economics JK has failed, ila his loyal followers wako busy doctoring the figures lakini sasa imefika mahali ukweli haufichiki tena.
 
Ndio maana ya vijiti kupokezana ndugu..Mkapa kakuta mambo kibao kwa mwinyi..na yeye JK ataacha vitu kibao ...kwa rais wa awamu ya tano...ndio tunaijenga nchi hivyo..
 
Tumain,

..JK ameikuta serikali ikiwa na hali nzuri kifedha kuliko mwaka 1995 wakati Mkapa anaingia madarakani.

..kwa kweli mimi nilitegemea JK atafanya mambo makubwa sana kuliko Mwinyi na Mkapa kwa kuzingatia kwamba alichukua nchi ikiwa na afueni ya kiuchumi/kifedha kuliko Maraisi hao wawili waliomtangulia.
 
Julius Nyerere will be remembered as a maverick who stood to the west. Shujaa wa mwisho Tanzania baada ya historia ndefu ya kina mkwawa

Ali Mwinyi will be remembered as a man who endorsed embezzlement within the government.

Benjamin Mkapa will be remembered as a man who welcomed foreign investement to make his quick buck.

And Jakaya Kwikwete will be remembered has a man who sold us back to colonial masters, rob us our land, destroyed future prospects by endorsing land reform (EAC) due to his naivity.

The man should step down quickly for the sake of our Tanznania. A coward can never take us anywhere. May be he should have been a foreign affairs minister for the passion he has on flying, but not our president.

The next one should be a well schooled patriot for the sake of our land and freedom.
 

Wewe ulimpigia (kama ulipiga kura) nani kura mwaka 2005?
 
Umeshasahau kwamba Wanazuoni wa TZ bado wanatumia vigezo hivyo hivyo (bila ya facts) kumsifia Nyerere? Let's look the "history from below" and see who was a better leader between Kikwete, Mkapa, Mwinyi and Nyerere.

So according to the facts you have who was the better leader? Nyerere, mwinyi, Mkapa or Kikwete? Just curious.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…