Kwa maoni yangu Kikwete uongozi umemshinda na mimi sioni chochote cha kumpongeza. Alipata ushindi wa kishindo kwa kuahidi kuipitia mikataba upya ya uchimbaji madini yetu ambayo ilisainiwa na Mkapa hadi hii leo pamoja na kuunda kamati ya madini bado mapendekezo yaliyotolewa na kamati hiyo hadi hii leo bado tunaendelea kupata 3% ya mapato yote ya dhahabu na kuwaachia wageni 97% ya mapato. Pamoja na bei ya dhahabu kuongezeka kwa kiasi kikubwa sana (Wakati Mkapa anasaini Bei ya dhahabu ilikuwa ni dola 233 na sasa ni zaidi ya dola 1,100. Kwa kifupi bado tunaliwa kwenye rasilimali zetu.
Aliahidi Maisha bora kwa kila Mtanzania, sijui kama alikuwa na mikakati ya kuhakikisha hili analifanikisha vipi kama kiongozi au ilikuwa na kauli tu ambayo haikuwa na mikakati yoyote bali ni katika kupata kura nyingi toka kwa Watanzania.
Kwenye swaala la ufisadi mpaka sasa hivi ameshindwa katika kila ufisadi uliofanywa dhidi ya nchi yetu. Tukianzia Kiwira ambayo Mkapa alijiuzia kiwiziwizi mgodi ule wenye thamani ya shilingi bilioni 7 kwa shilingi milioni 700 tu na kulipa shilingi 70 millioni. Hadi leo Mkapa hajachunguzwa iliWatanzania tufahamu ni nani aliyeidhinisha uuzwaji wa mgodi ule. Mkapa pia alichukua mkopo wa shilingi bilioni 7 toka NSSF na hadi hii leo hakuna anayefuatilia mkopo huo ili Mkapa na Yona waanze kuurudisha. Pia si ajabu Mkapa na Yona wanaweza kulipwa mabilioni ya shilingi na Serikali eti kuwafidia katika gharama walizoingia kuhusiana na Kiwira.
Tukija EPA kitendo cha kutwambia kwamba wahusika wa EPA wamerudisha shilingi bilioni 70 na wakati huo huo kushindwa kuyaweka majina ya watuhumiwa hao hadharani na kiasi kilichorudishwa na kila mmoja kwa maoni yangu ni usanii wa hali ya juu. Na mimi siamini kama watuhumiwa wa EPA wamerudisha hata senti tano vinginevyo sioni ugumu wowote wa majina yao na kiasi walichorudisha kuwekwa hadharani. Kesi za EPA nazo zimejaa usanii mtupu hili siyo siri kabisa wote tunalijua. Balozi wa Marekani nchini wakati ule aliahidi nchi yake kuisaidia Tanzania kumrudisha nchini mhusika mkuu Balalli kama Serikali ingewaomba msaada huo, lakini Kikwete akaamua kukaa kimya bila ya kuchangamkia msaada ule mpaka Balalli akafa
Tukija kwenye ufisadi wa Kagoda wa $40 millioni tunajua fika kwamba muhusika na ufisadi wa Kagoda papa fisadi Rostam hawezi kabisa kuguswa hivyo hadi hii leo hakuna uchunguzi wowote unaofanywa ili Watanzania tuweze kufahamu nini kilichojiri katika ufisadi wa Kagoda ambapo zilichotwa
Tukija kwenye Rada yule mtuhumiwa Vithlani alikuwa nchini anahojiwa na vyombo vya dola, lakini kwa kuwa ufisadi ule unawagusa vingune wengi katika awamu ya tatu na ya nne basi wakampa upenyo akimbie nchi ili kuwasitiri wahusika wa ufisadi ule wa $12 millioni
Kwenye Richmond/Dowans nako mapendekezo ya kamati iliyoundwa na Bunge mpaka leo Kikwete na Serikali yake imeshindwa kuyafanyia kazi bila kuwa na sababu zozote zile za msingi na wahusika waliochota $172 millioni bila kuzifanyia kazi bado wanapeta mtaani na huku mjadala wake ukiendelea kwa mwaka wanne sasa
Meremeta ambapo $155 millioni zilichotwa, hii tumeambiwa kwamba inahusiana na usalama wa Taifa na wizi wowote unaohusiana na usalama wa taifa haustahili kujadiliwa popote pale!!! Mhhh!
Rukia Mipasho Simba anasema hawezi kujiuzulu hadharani. Mzee wa Vijisenti Chenge Mnyunyizaji anatamka hadharani kwamba hakuna anayemchunguza kama yupo amfuate jimboni kwake. Papa fisadi Rostam kwa mara ya pili anaomba uchunguzi wa Richmond ufanyike tena kwa sababu hakubaliani na ripoti ya kamati ya Bunge mara ya kwanza alitaka uchunguzi mpya ufanywe na majaji. Haya yote yanaonyesha kwamba hawa wameshafahamu fika kiongozi wa nchi ambaye ana madaraka makubwa aliyokabidhiwa na Watanzania baada ya kumchagua kwa kishindo hana kabisa ubavu wa kuyatumia madaraka aliyokabidhiwa. Hawa kila mtu anaropoka kivyake vyake tu maana wanajua hakuna athari yoyote itakayowapata kutokana na kuropoka huko.
Mashule yetu bado mengi majengo yake hayana hata hadhi ya kuitwa ****** wachilia mbali madarasa, asilimia kubwa ya Wanafunzi bado wanakaa chini walimu ndiyo wa kubahatisha na wakti mwingine hawako kabisa, huko CCM kutokana na uongozi wake dhaifu migongano chungu nzima isiyokwisha na kuonyeshana ubabe hadharani, na mipasho ya hali ya juu na wengine hata kutishiwa maisha yao!!
Mimi kwa maoni yangu ukitilia maanani ufisadi wa Richmond, $172, EPA $133 millioni, Rada $12 millioni, Meremeta $155 millioni Kagoda millioni $40 basi ni haki kabisa kutumia ufisadi kama kigezo cha kumpima Kikwete na hata tukitumia vigezo vingine vyovyote vile hakuna hata kigezo kimoja ambacho anastahili kupewa pongezi.
Sasa tukitilia maanani hayo yote niliyoyaandika hapo juu tutaona kwamba Kikwete siyo tu hastahili pongezi zozote bali pia hastahili kugombea tena 2010. . Tumeshaona Kikwete kama kiongozi alivyo dhaifu katika mambo mbali mbali na hii kwa maoni yangu ni sababu tosha kabisa ya kuhakikisha tunapata kiongozi mpya 2010 ambaye atakuwa tayari kuyatumia madaraka aliyonayo bila kumuogopa yeyote yule.
Kama kiongozi mwenye mediocre perfomance kiasi hiki anashindwa kuambiwa kwamba kazi tuliyokupa imekushinda hivyo kaa pembeni ili tumtafute kiongozi mpya basi Tanzania tuna matatizo makubwa sana
Mchango wangu wa thumni huo