Kupimana imani

Kupimana imani

Rich Pol

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2013
Posts
7,874
Reaction score
5,685
Hii ni true story alinihadithia rafiki yangu

Mm na mpenz wangu Tupo kwenye love kwa miaka 4 sasa na nimeamua kumuoa,kitu ambacho kinanisumbua ni huyu mdogo wake wa kike, shemeji yangu huyu hupenda kuvaa vinguo vifupi na vinavyobana,hupenda kuinama kila anapokuwa karibu nami na kunifanya mm nione mapaja yake mazuri na mistari ya....

Siku moja niliitwa na huyu shemeji yangu kwenda kuangalia kadi za mualiko wa harusi,nilipofika nilistuka kumkuta peke yake akiwa kavaa kanga moja tu, hizi kanga za india, kanga ilikuwa nyepesi kiasi cha kufanya macho yangu yaweze ona rangi ya kilichovaliwA ndani, kabla sijasema lolote shemeji yangu aliamua kuvunja ukimya kwa kufunguka juu ya hisia zake kwangu, aliomba nimpe raha angalau Mara moja kabla sijafunga ndoa na dada yake. Moyo ulianza kwenda mbio huku mwili ukitetemeka, nikashindwa kujibu kitu.

Aliniambia kama nataka mautamu basi nimfate chumbani kwake ambapo alikuwa akilala ghorofani, akanza panda ngazi kuelekea kwake kwa mwendo wa madaha na kuniacho nimekodoa mimacho kama mjusi aliyebanwa na mlango��, nikitizama kanga iliyokuwa inasogea kutokana na hatua zake.

Mwili ulinisimka,nikahisi baridi hivi oooh,nilisimama kwa mda kisha nikageuka na kuutazama mlango wa kitokea nje. Nikosogea mlangoni na kutoka nje kwa haraka mno nikielekea nilikopaki gari yangu, ghafla nikaona kundi la familia ya wakwe zangu wakinipigia makofi.

Huku machozi yakimtoka,baba mkwe alinifuata na kunikumbatia. Akasema "familia imefurahi kwa kufahulu hili jaribio, karibu sana ktk familia yetu''
Nilivuta pumzi kwa nguvu kisha nikatabasamu kwa furaha oooohm asante Mungu maana nilikuwa naenda kwenye gari kuchukua condom zangu.
 
Mambo mengine si kupimana imani ila nikuhamasisha ngono.Maana baada ya hapo watakua wanaangalianaje mtu na shemeji yake?Ndio hapo baadae wanaanza kuambizana wafanye kweli
 
Mambo mengine si kupimana imani ila nikuhamasisha ngono.Maana baada ya hapo watakua wanaangalianaje mtu na shemeji yake?Ndio hapo baadae wanaanza kuambizana wafanye kweli

Naona kabla hawajafanya ndugu wangefumania na kusitisha shughuri nzima ya harusi
 
Am confused
Baba mkwe kujihusisha kwenye huo upuuzi
It means huyo mdogo wake mkewe mtarajiwa akija kuolewa mtihani atakaopewa utakuwa kutoka kwa mkeo au nani
Familia zenye watu wenye ethics hawawezi kukufanyia trial kama hiyo
 
Hahahahhahahaaaaa mwanzoni nilitaka nikoment kitu kingine lakini baada ya kusoma hadi mwisho nimeishia kucheka tu aiseee, ok mstari wa mwisho nadhani ndio umebeba story nzima. Imani yako nikiipima inafika qramu hamsini tu maana kama ungekuwa nazo (condom) mfukoni kama mimi I am sure ungekua ushakula nyama halafu bint angetoka na kukusifia kuwa umeshinda mtihani, kwani nani asiyependa utamu??

Lunch time hii
 
Hapana chezea binamu Elli.Kwa hiyo huwa unatembea nazo kabisa?Kweli umetisha
 
Last edited by a moderator:
Duuh, Huo siyo kwa utamaduni wa hapa kwetu....... ni mila za wenzetu wenye misimamo !! Lakini story hii educative !! suregirl Rich Pol Honey Faith

Sio educative wala nini mie naona inahamasisha ngono tena ile ngono zembe maana akikutwa si mvumilivu na asiyejali kinga angemrarua huyo shemeji mtu mpaka washangae wenyewe
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom