Kupinga serikali tatu kwa kisingizio cha gharama ni upuuzi

Kupinga serikali tatu kwa kisingizio cha gharama ni upuuzi

Bramo

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2009
Posts
13,176
Reaction score
10,068
Wakuu JF, Amani iwe Nanyi
Kuna watu wameshaanza tayari ,nina uhakika watu hawa wanatumiwa.
Wanapinga Rasimu ya Serikali tatu kwa kigezo cha Gharama.
Eti Nchi itakuwa na Gharama Kubwa ku Run na Marais wa Tatu.
Watu kama hawa wanastahili Kukumbushwa kuwa kwa Sasa Nchi ina Ma Rais wa Tano na Wa Tatu wanatokea zanzibar.
Watu hawa wamekuwa wapofu kuona kuwa Tume ya Warioba imependekeza Baraza lenye Ma Waziri wasiozid 15.
Kwa Sasa Baraza lina Zaid ya Mawaziri 45, Mbona hawasemiGharama kubwa za ku Run the Current Baraza la Mawaziri?????
Hawaoni kuwa kwa Kupunguza Baraza la Mawaziri Mpaka 15 tUtakuwa tumeokoa Kiasi kikubwa sana Cha Fedha.
Watu wanaopinga Serikali 3 Hawastahili kuishi Tanzania,
TUSIMAME KUWAPINGA HAWA WACHUMIA TUMBO
 
Naunga mkono. Ni upuuzi kwa kudhani kuwa mfumo wa uendeshaji wa nchi utakuwa huu uliopo, hivyo kuwa mzigo. Hautakuwa huu kabisa. Taasisi ya Uraisi wa Muungano itakuwa ndogo kwani mambo ya utawala yatakuwa yanafanywa na serikali za washirika ambazo pia zinaweza kubanwa kuondoa mambo mengi yasiyo ya lazima katika mfumo wa utawala uliopo sasa. Fikiria kuwa Tanzania bara nayo iwe na serikali yenye wizara zisizozidi 15. Fikiria kuwa labda ngazi ya ukuu wa wilaya iondolewe na majukumu yake yafanywe na Kurugenzi ya halmashauri za Wilaya. Nina maana kuwa kutakuwa na mabadiliko makubwa na wala haitakuwa mzigo. Ikumbukwe kuwa hata rasimu ya Katiba ya Tanzania bara haipo. Tusiogope mabadiliko kwani hayana budi kutokea kwa sasa. Tukikataa mabadiliko tunayoyaratibu wenyewe, yatakuja kwa njia ambayo hatutairatibu na ita kuwa mbaya yenye gharama ya kutisha. Kumbukeni mabadiko yaliyotokea katika nchi za Afrika ya Kaskazini. Waliogopa mabadiliko wakati upepo wa demokrasia ya vyama vingi ulipokuwa unavuma lakini kwa kuwa mabadiliko hayanabudi kutokea yakatokea kwa njia ambayo iligharimu umwagikaji wa damu na uharibifu mkubwa wa nchi. Cha kuangalia kwa sasa ni juu ya Katiba mpya, ya kidemokrasia, nzuri, makini, ya Tanzania bara.
 
Mkuu mshunami umenigusa sana. Any way. Katika Bible Mshunami alikuwa mke wa Mfalme Sulemani aliyekuwa na hekima nyingi sana.. Wewe ni nani? (jinsia) Samahani kwa kukuuliza hivyo. Ni kwa sababu kuna hekima sana katika hayo uliyosema.
 
serikali ya zanzibar
serikali ya Tanganyika
serikali ya Shirikisho
Hata kwa hoja ya gharama huoni kuwa ni ukweli wa wazi.
Kila serikali itakuwa na baraza la mawaziri, rais, na bunge lake.
Ukizingatia iyo katiba yenu mnayoishadadia inatupa wabunge wawili kila jimbo... mtu na demu wake!
Hivi tuna majimbo mangapi?
Na mangapi yataongezwa kwa kuvunja majimbo yanayoongozwa na Chadema?
Ila hii naipendea kitu kimoja... ambacho watanganyika tunakitamani na wazenji wanajidanganya eti wanaitaka...
...uyo kiongozi wa shirikisho ataachwa solemba akiwa yuko hewani... rejea USSR
 
Naunga mkono. Ni upuuzi kwa kudhani kuwa mfumo wa uendeshaji wa nchi utakuwa huu uliopo, hivyo kuwa mzigo. Hautakuwa huu kabisa. Taasisi ya Uraisi wa Muungano itakuwa ndogo kwani mambo ya utawala yatakuwa yanafanywa na serikali za washirika ambazo pia zinaweza kubanwa kuondoa mambo mengi yasiyo ya lazima katika mfumo wa utawala uliopo sasa. Fikiria kuwa Tanzania bara nayo iwe na serikali yenye wizara zisizozidi 15. Fikiria kuwa labda ngazi ya ukuu wa wilaya iondolewe na majukumu yake yafanywe na Kurugenzi ya halmashauri za Wilaya. Nina maana kuwa kutakuwa na mabadiliko makubwa na wala haitakuwa mzigo. Ikumbukwe kuwa hata rasimu ya Katiba ya Tanzania bara haipo. Tusiogope mabadiliko kwani hayana budi kutokea kwa sasa. Tukikataa mabadiliko tunayoyaratibu wenyewe, yatakuja kwa njia ambayo hatutairatibu na ita kuwa mbaya yenye gharama ya kutisha. Kumbukeni mabadiko yaliyotokea katika nchi za Afrika ya Kaskazini. Waliogopa mabadiliko wakati upepo wa demokrasia ya vyama vingi ulipokuwa unavuma lakini kwa kuwa mabadiliko hayanabudi kutokea yakatokea kwa njia ambayo iligharimu umwagikaji wa damu na uharibifu mkubwa wa nchi. Cha kuangalia kwa sasa ni juu ya Katiba mpya, ya kidemokrasia, nzuri, makini, ya Tanzania bara.

Mimi kwangu wafaanye yoooote, wabadilishe kila kitu, lakini Mtu asicheze ma Madaraka ya Raisi hapo ndipo nilipochora Mstari!
Hayo mengine ni wabadilishe wanavyotaka lkn Mtu asiguse Madaraka ya Raisi eti kupunguzwa, hilo nitalipinga mpaka siku ya Mwisho!

Asietaka kubadilika wakati utam-badilisha,jamhuri ya watu wa z'br kwanza,shengesha baadae.
 
Hawa wajumbe wa tume inafaa waongezewe panadol kwa kweli, wembe tumeulilia wenyewe jamani mbona twatoka na povu?
 
mambo ya serikali tatu hayana maana,maana ni kama vile hakuna muungano.tumeungana basi tunataka serikali moja.

hapo ndipo penye muhogo mchungu kumeza kwa wazanzibari
 
Naunga mkono. Ni upuuzi kwa kudhani kuwa mfumo wa uendeshaji wa nchi utakuwa huu uliopo, hivyo kuwa mzigo. Hautakuwa huu kabisa. Taasisi ya Uraisi wa Muungano itakuwa ndogo kwani mambo ya utawala yatakuwa yanafanywa na serikali za washirika ambazo pia zinaweza kubanwa kuondoa mambo mengi yasiyo ya lazima katika mfumo wa utawala uliopo sasa. Fikiria kuwa Tanzania bara nayo iwe na serikali yenye wizara zisizozidi 15. Fikiria kuwa labda ngazi ya ukuu wa wilaya iondolewe na majukumu yake yafanywe na Kurugenzi ya halmashauri za Wilaya. Nina maana kuwa kutakuwa na mabadiliko makubwa na wala haitakuwa mzigo. Ikumbukwe kuwa hata rasimu ya Katiba ya Tanzania bara haipo. Tusiogope mabadiliko kwani hayana budi kutokea kwa sasa. Tukikataa mabadiliko tunayoyaratibu wenyewe, yatakuja kwa njia ambayo hatutairatibu na ita kuwa mbaya yenye gharama ya kutisha. Kumbukeni mabadiko yaliyotokea katika nchi za Afrika ya Kaskazini. Waliogopa mabadiliko wakati upepo wa demokrasia ya vyama vingi ulipokuwa unavuma lakini kwa kuwa mabadiliko hayanabudi kutokea yakatokea kwa njia ambayo iligharimu umwagikaji wa damu na uharibifu mkubwa wa nchi. Cha kuangalia kwa sasa ni juu ya Katiba mpya, ya kidemokrasia, nzuri, makini, ya Tanzania bara.

Tatizo ni kwamba watz wengi hawjaisoma rasimu hii na kuielewa, badalayake wadandia uchambuzi wa baadhi ya watu wengi wenye hiden agenda..!
hebu angalia huyu mpuuzi mwengine,https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...yo-serikali-moja.html?highlight=serikali+tatu hawa ni watu wenye mawazo mgand wanao fanya kitu bila kufikiri.

Kwanini unaita wenzako wneye mawazo tofauti wapuuzi?

Hivi ndivyo jinsi ma great thinkers wanavyopingana kwa hoja?
 
Mambo ya serikali tatu hayana maana,maana ni kama vile hakuna muungano.Tumeungana basi tunataka serikali moja.

Kwanza kabisa naipongeza tume kwa kazi nzuri na kwakufanyia kazi kwa umahiri mkubwa maoni ya wananchi "Wananchi have spoken, we are duty bound to respect their voices".

Muundo wa serikali tatu ni mzuri kisheria. Kila nchi itakuwa huru kujifanyia mambo yake bila kuathiri muungano/shirikisho.
Hoja ya gharama kubwa na kuvunjika muungano, hizo ni hoja ambazo wanasiasa (baadthi ya wanasiasa wa CCM wanaoutaka uraisi 2015 na makundi yao), ambao masilahi yako yameathirika kwa muundo wa serikali tatu wanahaha kujificha katika hoja hizo. Kimsingi hizi hoja ni za kupikwa na wanasiasa ili kujustfy interests zao kisiasa.
Gharama: Hii siyo hoja, kwani serikali za Tanzania bara na Zanzibar watatakiwa kuunda mabaraza ya mawaziri pasipo kuweka mbele urafiki na vyama vyao.Watatakiwa kuzingatia ufanisi zaidi.Hivyo hawatahitaji kuwa na baraza kubwa la mawaziri, wasiozidi 10. Wabunge nao,tume za uchaguzi za nchi hizo 2 zitalazimika kupunguza majimbo yasiyo ya lazima. Mishahara ya wabunge hao kupunguzwa.

Kuvunjika kwa Muungano: Atavunja nini? Hizi ni hofu za bure. Kwani maraisi wote wa nchi 2 watakuwa ni wajumbe wa baraza la usalama la taifa.

NOTE: -Wanasiasa waache mchezo huo mchafu wa kuingilia "sauti za wananchi", kwa masilahi yao kisiasa.
- Watanzania tuwe makini na propaganda hizi za wanasiasa wanaotaka kupindisha ukweli kwa masilahi yao kisiasa.
 
Tatizo Watanzania wengi ni makupe,tunaishi kwa mawazo ya wengine. Serikali tatu ni uchu wa kutaka kuongoza, it's better to 've two independent country rather than three government within same republic. If you cannot remove a stone on your way,go around it. Vijana wengi wamekuwa makupe,rasimu hii haifai kwa mtu ambaye ni mzalendo wa Afrika. 99.99% rasimu imeongelea suala zima la muundo wa uongozi na kusahau mambo nuhimu. I believe most of Tanzanian lack political awareness,thus why the government use this opportunity to humiliate them. Serikali tatu ni mwanzo wa kuigawa nchi. Hii rasimu ikipita, I MUST ORGANISE REVOLUTION.
 
Kwanza nianze kwa kumwambia mleta thread kuwa hakuna mtu yeyote ambae ni mpuuzi ila yeye anaemdhani mwenzie ni mpuuzi! Kila mtu ana haki ya kutoa maoni na msimamo wake kulingana na fikra zake!

Sidhani kama ni jambo la kueleweka kwamba kuna watu wanataka muungano alafu wanataka serikali tatu , kinacho shangaza nipale wanapo taka kutoka kwenye Muungano wa serikali mbili kwenda serikali tatu badala ya moja, yaani nikama unakimbia kurudi ulipotoka, nadhani kuna kitu kimefichika hapa,kuna watu wana agenda ya sili ya kujitafutia wao na familia zao madaraka na malupupu. Sioni umuhimu wa serikali tatu, ni bora tuendelee na serikali mbili kama tunataka kuungana zaidi iwe moja au Tuvunje tu Muungano ili tujue moja. Ni mawazo yangu and I stand to be challenged!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hii rasimu ni kwa ajili ya watu wachache,lakini kwa kuwa Watanzania wengi ni makupe,hawalioni hili. A great thinker has to think about 50 y's to come and not today &tomorrow. Nawapinga kwa nguvu zote.
 
Kila mwananch achague serikar yake hapo chacha

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Mimi naona tuuvunje huu Muungano tuwe na Tanganyika yetu.
 
Ungefanya la maana kuchambua faida na hasara za serikali 1, serikali 2, na serikali 3.
 
Hivi ni lazima awepo raisi wa Muungano? Kwani EAC kuna Rais. Mm napinga serikali tatu. Serikali mbili zatosha, na kama ni ushirikiano uwepo kati ya Zanzibar na Tanganyika chini ya wirzara fulani.
 
Back
Top Bottom