Naunga mkono. Ni upuuzi kwa kudhani kuwa mfumo wa uendeshaji wa nchi utakuwa huu uliopo, hivyo kuwa mzigo. Hautakuwa huu kabisa. Taasisi ya Uraisi wa Muungano itakuwa ndogo kwani mambo ya utawala yatakuwa yanafanywa na serikali za washirika ambazo pia zinaweza kubanwa kuondoa mambo mengi yasiyo ya lazima katika mfumo wa utawala uliopo sasa. Fikiria kuwa Tanzania bara nayo iwe na serikali yenye wizara zisizozidi 15. Fikiria kuwa labda ngazi ya ukuu wa wilaya iondolewe na majukumu yake yafanywe na Kurugenzi ya halmashauri za Wilaya. Nina maana kuwa kutakuwa na mabadiliko makubwa na wala haitakuwa mzigo. Ikumbukwe kuwa hata rasimu ya Katiba ya Tanzania bara haipo. Tusiogope mabadiliko kwani hayana budi kutokea kwa sasa. Tukikataa mabadiliko tunayoyaratibu wenyewe, yatakuja kwa njia ambayo hatutairatibu na ita kuwa mbaya yenye gharama ya kutisha. Kumbukeni mabadiko yaliyotokea katika nchi za Afrika ya Kaskazini. Waliogopa mabadiliko wakati upepo wa demokrasia ya vyama vingi ulipokuwa unavuma lakini kwa kuwa mabadiliko hayanabudi kutokea yakatokea kwa njia ambayo iligharimu umwagikaji wa damu na uharibifu mkubwa wa nchi. Cha kuangalia kwa sasa ni juu ya Katiba mpya, ya kidemokrasia, nzuri, makini, ya Tanzania bara.