Naunga mkono. Ni upuuzi kwa kudhani kuwa mfumo wa uendeshaji wa nchi utakuwa huu uliopo, hivyo kuwa mzigo. Hautakuwa huu kabisa. Taasisi ya Uraisi wa Muungano itakuwa ndogo kwani mambo ya utawala yatakuwa yanafanywa na serikali za washirika ambazo pia zinaweza kubanwa kuondoa mambo mengi yasiyo ya lazima katika mfumo wa utawala uliopo sasa. Fikiria kuwa Tanzania bara nayo iwe na serikali yenye wizara zisizozidi 15. Fikiria kuwa labda ngazi ya ukuu wa wilaya iondolewe na majukumu yake yafanywe na Kurugenzi ya halmashauri za Wilaya. Nina maana kuwa kutakuwa na mabadiliko makubwa na wala haitakuwa mzigo. Ikumbukwe kuwa hata rasimu ya Katiba ya Tanzania bara haipo. Tusiogope mabadiliko kwani hayana budi kutokea kwa sasa. Tukikataa mabadiliko tunayoyaratibu wenyewe, yatakuja kwa njia ambayo hatutairatibu na ita kuwa mbaya yenye gharama ya kutisha. Kumbukeni mabadiko yaliyotokea katika nchi za Afrika ya Kaskazini. Waliogopa mabadiliko wakati upepo wa demokrasia ya vyama vingi ulipokuwa unavuma lakini kwa kuwa mabadiliko hayanabudi kutokea yakatokea kwa njia ambayo iligharimu umwagikaji wa damu na uharibifu mkubwa wa nchi. Cha kuangalia kwa sasa ni juu ya Katiba mpya, ya kidemokrasia, nzuri, makini, ya Tanzania bara.
serikali ya zanzibar
serikali ya Tanganyika
serikali ya Shirikisho
Hata kwa hoja ya gharama huoni kuwa ni ukweli wa wazi.
Kila serikali itakuwa na baraza la mawaziri, rais, na bunge lake.
Ukizingatia iyo katiba yenu mnayoishadadia inatupa wabunge wawili kila jimbo... mtu na demu wake!
Hivi tuna majimbo mangapi?
Na mangapi yataongezwa kwa kuvunja majimbo yanayoongozwa na Chadema?
Ila hii naipendea kitu kimoja... ambacho watanganyika tunakitamani na wazenji wanajidanganya eti wanaitaka...
...uyo kiongozi wa shirikisho ataachwa solemba akiwa yuko hewani... rejea USSR
Wakuu JF, Amani iwe Nanyi
Kuna watu wameshaanza tayari ,nina uhakika watu hawa wanatumiwa.
Wanapinga Rasimu ya Serikali tatu kwa kigezo cha Gharama.
Eti Nchi itakuwa na Gharama Kubwa ku Run na Marais wa Tatu.
Watu kama hawa wanastahili Kukumbushwa kuwa kwa Sasa Nchi ina Ma Rais wa Tano na Wa Tatu wanatokea zanzibar.
Watu hawa wamekuwa wapofu kuona kuwa Tume ya Warioba imependekeza Baraza lenye Ma Waziri wasiozid 15.
Kwa Sasa Baraza lina Zaid ya Mawaziri 45, Mbona hawasemiGharama kubwa za ku Run the Current Baraza la Mawaziri?????
Hawaoni kuwa kwa Kupunguza Baraza la Mawaziri Mpaka 15 tUtakuwa tumeokoa Kiasi kikubwa sana Cha Fedha.
Watu wanaopinga Serikali 3 Hawastahili kuishi Tanzania,
TUSIMAME KUWAPINGA HAWA WACHUMIA TUMBO
Mambo ya serikali tatu hayana maana,maana ni kama vile hakuna muungano.Tumeungana basi tunataka serikali moja.
Tatizo ni kwamba
watz wengi hawjaisoma rasimu hii na kuielewa, badalayake
wadandia uchambuzi wa baadhi ya watu wengi wenye hiden agenda..!
hebu angalia huyu mpuuzi
mwengine,https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...yo-serikali-moja.html?highlight=serikali+tatu
hawa ni watu wenye mawazo mgand wanao fanya kitu bila kufikiri.
mleta thread naona hata
hajitambui.wizara hazijapunguzwa,hizo zilizosemwa ni za muungano tu.hapo
bado za tanganyika,hao wazenji wakafie mbali na wizara zao
hazituhusu.huku bara utakutana na mafisadi watataka kula so
watajitengenezea nafasi nyingi tu.bado mabunge matatu,wabunge watatu
kila jimbo,wakuu wa mikoa/wilaya,makatibu,manaibu waziri na wapambe
wao.ukisikiliza madai ya wazenji ndio utachoka so kwa nini tusivunje tu
muungano kama watu wanataka mamlaka kamili?