Kupinga wagombea huru, ni uamuzi wa "Kipumbavu"

Kupinga wagombea huru, ni uamuzi wa "Kipumbavu"

mwanakijiji.....au marmo hajaamka maana ni saa 0830am
 
unaona usivyo makini alisema 70% , wewe umo humo!
Waw, naona unazidi kudhihirisha kuwa wewe ni walewale . 70 or 75 % is philosophical figure, maana hakukaa mahali kuwahesabu hao wafuata upepo,( i bet wewe ni kamishna wa hao wafuata upepo). Labda ulimsaidia ku-derive hiyo figure.
 
wacha nimalize ku - download nisikilize wakuu.
 
mzee umeua, Mfano wa Kiula na Nguva umemuua, hakuweza kujibu swali.
 
Currently Active Users Viewing This Thread: 50 (21 members and 29 guests)
Bila shaka naye Waziri ni miongoni mwa hao guests!
 
mahojiano mazuri sana, mwanakijiji umejaribu kumbana waziri - lakini naona waziri alikuwa anakwepa kwepa viunzi - bado una dukuduku hata mimi sijaridhika sana na majibu ya mheshimiwa Marmo

Nafurahia wimbo baada ya mahojiano unanifariji na shida zangu nilizonazo kwani unanikumbusha mbali sana......
 
Hawa jamaa wanataka kutufanyia usanii tena..i fear kama hawatanunua hii kesi ili washinde wao ..but let see
 
I wonder kwanini anasema lipelekwe kwa wananchi, wakati wawakilishi wa wananchi tayari wametunga sheria (Katiba) inayomruhusu mgombea binafsi, na chombo kinachotafsiri sheria (katiba) kimesema kuwa kikatiba inaruhisu. Kwanini kigugumizi? Kwanini serikali inapinga?

Mwanakijiji ingekuwa ni vizuri pia ungepata insight ya Mh Sitta kuhusu suala hili.
 
Kuna vocha moja mtu amelipia kwa matumizi ya internet in bracket access JF website.

Idumu JF, wadumu waliojitolea kuiweka hewani. Inashika.
 
good interview na pia umejitahidi kumueweka Mh.Marmo ndani ya interview kwa muda wote japo mwanzo alikuwa akisound not eager to talk.....hili suala wanalichukulia very political...
 
Jamaa kajitahidi kujihami. Lakini kama Serikali inatishika na suala dogo kama mgombea binafsi, itaweza mambo makubwa kama kubadili tume ya uchaguzi kuwa huru. Manake tume ni yao, hivyo wanapata kila msaada toka kwa hiyo tume. Pia ni pale watumishi wa Serikali (kama wakurugenzi) wanapotumika katika chaguzi, haiwezekani kupatikana haki.

Lakini taratibu tutafanikiwa, CCM hawawezi kutufanya watu wote majuha kwa nyakati zote.
 
Kwanza nikupongeze M.Mwanakijiji.

Pili nikiri kuwa nimeyasikiliza vizuri kabisa hayo mahojiano

Tatu nikubali kuwa hili ni moja ya mambo ya maana ambayo huwa yanafanyika hapa jamvini.

Nne, Mimi nimegundua nini.


Wakati mahakama ilipotoa hukumu ya kwanza, hao hao walikimbilia bungeni na kubadilisha katiba ili kumzuia mgombea binafsi BILA KURA YA MAONI. Leo mahakama inakomaa wanakuja na ujanja wa kutuambia kuwa kubadilisha katiba kuna mchakato. MBONA WAKATI ULE MCHAKATO HAUKUFUATWA?

Hii ni karata nzuri sana ya kisiasa kwa wapinzani, Je waniona? Mh Waziri hata anaona aibu kwa kuwafanya Watanzania wajinga mchana kweupe, mfano: Anaulizwa Kwanini tangu hukumu ya kwanza serikali haijafanya maandalizi yoyote, jibu lake ni utumbo mtupu. MM anamwambia hekima iko wapi kuja kukata rufaa leo baada ya karibu miaka mitano, masikini mzee wa watu hana majibu.

Kwenye bunge la kubadilisha katiba kumzuia mgomba binafsi Marmo alikuwamo ndani na alikubali hilo lifanyike, sasa atasema nini tofauti?

Huu ni mtihani mkubwa kwa MHIMILI WA TATU WA NCHI YAANI MAHAKAMA. Hukumu yao inaweza kuwa kitanzi chao ama uhuru wao. Naamini hawatakubali kusukumwa kutoa maamuzi ya kuipendele serikali.
 
Bila ya shaka; huwa inachosha kusoma quotes tu toka kwenye magazeti..
Kazi nzuri kwa mahojiano na ubunifu wa kaka yetu M. Mwanakijiji. Hata hivyo, hata siku moja sijaridhisha na juhuzi za serikali kujaribu kubana hadi hukumu iliyotolewa isitekelezwe. Kwa mfano, serikali ilikuwa wapi kuandaa rufaa yake mapema tu baada ya hukumu? Mbona wamesubiri mwaka wa uchaguzi mkuu uliolengwa na hukumu iliyotolewa mwaka 2006, ndiyo kasi ya rufaa yao ikawa kubwa? Kwa nini isingefanyika 2006, 2007, 2008 ama mapema 2009?
 
Asante Mkuu! mahojiano haya yanaonyesha jinsi huu muungano una migongano! Ni jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini kuna upande mmoja unaweza kutoa maelekezo ya nini kifanyike upande wa pili but not the same to the other side. Na pia sheria zinaweza kugeuzwa geuzwa kukidhi mahitaji ya kundi fulani.

Bado tuna imani na mahakama kwenye hili....hata wakilikwamisha sasa linakuja...kivuli hakikimbiwi. Kelele kila siku ndani ya hili jumba kubwa! Tunazozana mno! Ha ha ha! Pwagu na Pwaguzi
 
Wajameni me mbona nasikia ala za muziki na maneno machache inakuwaje? Au ni changa la macho?

Big up Mwanakijiji, mimi naipata yote hapa, cjui wengine kwanini hawaipati yote, guys mimi naipata , nipo hapa nasikiliza mahojiano, lakini naona marmo is incompetent, majibu yake hayaridhishi kabisa, mimi naona sheria haijui kabisa, toka lini hukumu ikikatiwa rufani basi ile hukumu ya mwanzo haitekelezeki, anakuja na habari kuwa hiyo rufani iko mahakama ya juu na kesi kama za akina Nguza zilikuwa mahakama ya hakimu mkazi-----------cmuelewi kabisa
 
I wonder kwanini anasema lipelekwe kwa wananchi, wakati wawakilishi wa wananchi tayari wametunga sheria (Katiba) inayomruhusu mgombea binafsi, na chombo kinachotafsiri sheria (katiba) kimesema kuwa kikatiba inaruhisu. Kwanini kigugumizi? Kwanini serikali inapinga?

Mwanakijiji ingekuwa ni vizuri pia ungepata insight ya Mh Sitta kuhusu suala hili.

Natarajia mwaka huu tutashuhudia mvutano mkubwa wa mahakama na serikali, ambao haujapata kutoea.Kauli za marmo na membe ni dhahiri kuwa wameshakubaliana hivyo serikalini, hawahitaji kuruhusu mgombea binafsi.

Yaani uamuzi wa mahakama unapelekwa kwanza kwa wananchi kabla ya utekelezaji?hii serikali ya JK kiboko!!

Lakini binafsi bado nina imani kubwa sana na Jaji Mkuu Samatta, hawezi kuuma uma maneno wala kuogopa wanasiasa katika hili, ndio maana naamini kwa dhati kwamba hapo april mahakama ya rufaa itakapoketi kusikiliza na kutoa uamuzi juu ya kesi hii, kuna watu hawataamini macho yao.

Bado nina imani na Jaji samata, naisubiri april ifike tujue mbivu na mbichi.
 
Back
Top Bottom