Kwanza nikupongeze M.Mwanakijiji.
Pili nikiri kuwa nimeyasikiliza vizuri kabisa hayo mahojiano
Tatu nikubali kuwa hili ni moja ya mambo ya maana ambayo huwa yanafanyika hapa jamvini.
Nne, Mimi nimegundua nini.
Wakati mahakama ilipotoa hukumu ya kwanza, hao hao walikimbilia bungeni na kubadilisha katiba ili kumzuia mgombea binafsi BILA KURA YA MAONI. Leo mahakama inakomaa wanakuja na ujanja wa kutuambia kuwa kubadilisha katiba kuna mchakato. MBONA WAKATI ULE MCHAKATO HAUKUFUATWA?
Hii ni karata nzuri sana ya kisiasa kwa wapinzani, Je waniona? Mh Waziri hata anaona aibu kwa kuwafanya Watanzania wajinga mchana kweupe, mfano: Anaulizwa Kwanini tangu hukumu ya kwanza serikali haijafanya maandalizi yoyote, jibu lake ni utumbo mtupu. MM anamwambia hekima iko wapi kuja kukata rufaa leo baada ya karibu miaka mitano, masikini mzee wa watu hana majibu.
Kwenye bunge la kubadilisha katiba kumzuia mgomba binafsi Marmo alikuwamo ndani na alikubali hilo lifanyike, sasa atasema nini tofauti?
Huu ni mtihani mkubwa kwa MHIMILI WA TATU WA NCHI YAANI MAHAKAMA. Hukumu yao inaweza kuwa kitanzi chao ama uhuru wao. Naamini hawatakubali kusukumwa kutoa maamuzi ya kuipendele serikali.