Mzee Mwanakijiji,
Mkuu huwezi kutenganisha haki ya mtu mmoja mmoja toka haki wa jamii ni kwa sababu haki nzima inahusu jamii hiyo na kwamba matendo hufanywa na mtu mmoja mmoja lakini hiyo right huandikwa kwa ajili ya jamii nzima..
sawa...lakini haki kabla ya kuandikwa kwa ajili ya jamii nzima hutambuliwa kama haki ya kila mwana jamii.
Mfano chukulia haki ya kuishi, inahusu jamii yote lakini wapo baadhi ya watu ambao hukutana na matatizo (individuals) na ndipo tunapotumia kifungu cha sheria hiyo inayohusu jamii..
Hapa unathibitisha ninachosema kuwa kulinda haki ya jamii yote ni lazima ulinde haki ya mtu mmoja mmoja kwenye jamii hiyo. Kwani kuvunja haki ya mtu mmoja ni kuvunja haki ya jamii nzima. NI kwa sababu hiyo hatuwezi kukaa kimya mtu mmoja akiamua kwenda kumtia kisa mtu mwingine kwa kusema ni haki ya mtu mmoja tu imevunjwa hivyo tusubiri hadi jamii nzima ivunjiwe haki hiyo. Jamii isiyoweza kulinda na kutetea haki ya mtu mmoja itaweza vipi kutetea na kulinda haki ya jamii hiyo nzima?
Tukikubali kuwa serikali inaweza kufuta haki ya mtu mmoja kuchaguliwa tutaweza vipi kuhakikisha haki ya watu wengi kuchaguliwa inalindwa?
Nachosema mimi hakuna haki inayoandikwa kwa ajili ya mtu mmoja hivyo jamii nzima waikubali haki ya mtu huyo..Utaratibu huu ndio uliopigwa vita na ujio wa Demokrasia kwa sababu zamani Masultan ndio walikuwa na haki ya kutawala kisheria na kati yao waligombea vile vile within royal family hizo lakini wananchi hawakupewa nafasi ya kumchagua kiongozi. Wakafuatia Madikteta ambao kwa kutumia nguvu ya chama au Jeshi waliteua ama kuchagua kiongozi bila wananchi kuhusishwa pia..
Mzee tunapozungumzia hapa ni kuwa haki inapotambuliwa inatambuliwa kama haki ya mtu mmoja kwanza. Ndiyo maana tunasema "kila mtu ana haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake" na hatusemi "kila jamii au watanzania wote wana haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake". Maana yake, mmachinga na tajiri wote wana haki sawa na usawa huo unatokana wote kuwa moja, binadambu; na mbili raia.
Wafalmee na masultani hawakutambua haki sawa kwa wote; ni wao walijipa haki zaidi kwa minajili ya nasaba zao au "matakwa ya Mungu". Ndio maana Mapinduzi ya Ufaransa yalitokea kudai haki za kila mtu na uwezo wa wao kujichagulia wanayemtaka; ni kwa sababu hiyo mapinduzi ya Marekani yalitokea kupinga "haki ya mfalme" kutawala na kurudisha haki ya watawaliwa kuchagua wanayemtaka; na ni kwa sababu hiyo Mapinduzi ya Zanzibar yalitokea kupinga utawala wa Sultani kwa sababu ulitambua haki ya watu wachache badala ya kila mtu.
Hat ukitazama huko kwenye utawala uliokuja pingwa na Demokrasia utakuta kilichotangulia ni ile executive power kuwa chini ya royal prerogative au tuseme Jeshi na sio individual ambao hawana nguvu ya kutawala kama hawana executive power vested in.
Power zote zinakuwa possessed by the Title na sio individuals pamoja na kwamba ni individuals watakao tawala. Bila shaka kwa mtazamo finyu unaweza kushindwa kuona nachojaribu kusema hapa, lakini mkuu ni rahisi kabisa..
Hapa unachanganya "mtu kuwa na madaraka" na mtu kuwa na haki ya kuweza kupata nafasi ya madaraka hayo. Ni kweli kuwa madaraka (power) yako kwenye cheo na si mtu. Na kwahili unathibitisha jambo lile lile. Mbunge anayetoka kwenye Chama na Mbunge anayechaguliwa kama mgombea huru wote watakuwa na madaraka sawa. Mbunge anayeingia Bungeni kama mgombea huru ataapa kuilinda Katiba ile ile na kule Bungeni ataingia na kuzungumza na kupata kinda na madaraka yote kama Mbunge wa Kuchaguliwa.
Mfano mzuri ni "wabunge wa kuteuliwa" na wa "viti maalumu" Hawa hawakuchaguliwa na wananchi lakini kwanini tunawakubali kama viongozi wakati wananchi hawakuwachagua? Yaani tunakubali Rais atuchagulie kiongozi kuwa mwakilishi lakini tunawanyima watu wa Chunya nafasi ya kumchagua kiongozi wanayemtaka kwa vile chama chake hakikumkubali?
Wabunge huru hawatishii madaraka ya mtu yeyote isipokuwa wanatishia uhuru wa watu wengine kufikiri wao ndio "watawala halali" kwa vile wamependekezwa na chama fulani.
ndio maana nikasema ni haki ya kila mtu kuabudu dini unayotaka ndiyo sheria imetungwa kwa kuitazama jamii nzima ya binadamu lakini individuals ndio wanakutwa na majanga haya kila siku sheria ipo kuwa protect.
Mheshimiwa, hivi Mtanzania akiamua kutengeneza ugiimbi wake, na sadaka yake ya kuku akaenda kwenye mti wa mkwaju kutoa sadaka kwa mababu zake serikali inaweza kumkataza kufanya hivyo kwa sababu hajajiunga na dini fulani iliyoandikishwa vitabuni? Je Mtanzania anayo haki ya kwenda kuabudu ng'ombe wake bila kulazimishwa kumsalia au kumswalia kikristu au Kiislamu? Je serikali inaweza kwenda mahakamani na kusema "tumeona ili kulinda amani na utulivu kila mtu anayetaka kuabudu lazima ajiunge na dhehebu fulani au aanzishe dhehebu lake rasmi?"
Tukirudi ktk uchaguzi nitarudia kusema kwamba haki ya mtu binafsi bado kabisa wakati wake Kantazania kwa sababu hadi sasa hivi siasa zetu zinatupotosha zaidi. Siku tutakapo weza kusimamisha Demokrasia na vyama vikawa vinatazamwa kwa mrengo na sera zake na akachaguliwa kiongozi anayeonekana kuwa mbora ktk kuwasilisha sera hizo kwa wananchi hapo naweza kukubali watu binafsi wanaokuja na hoja tofauti kabisa na vyama hivi..Not now hasa nikiwaona wagombea wenyewe wanaotafuta ULAJI na hawana mpya kisiasa zaidi ya ahadi za kutupa Utajiri!
sasa tumekuwa na wagombea kutoka kwenye vyama hivi miaka karibu hamsini sasa, wametufikisha wapi? Hivi wale waliozembea maofisini, kuiba mali zetu na kuharibu utawala wa sheria si wanatoka kwenye vyama hivyo? Je kwa wao kuwa wanachama wa chama cha kisiasa vimetusaidia vipi sisi? Sera si wanazo, namba si wanazo? Imelisaidiaje Taifa.?
Hakuna haja ya kusubiri kwa muda mrefu kwani kama kimeharibika ni bora tukitengeneze. Wagombea wa vyama vya siasa ambao tunaosasa wanafungia milango walio nje ya vyama hivyo kwa sababu yawezekana wao ndio wanatishiwa zaidi na wagombea huru.
Lakini tunapozungumzia wagombea huru, hatuzungumzii wale wasio na vyama tu na hii ni point naona unairuka. Tunazungumzia hata wale wenye vyama lakini kwa sababu ya ufinyu wa nafasi au uhuru wa aina fulani wanashindwa kugombea kupitia vyama vyao lakini wananchi wanawakubali na wao hawataki ikuvikana vyama vyao.
Hebu fikiria kama Dr. Salim, Dr. Kigoda au Mzee Malecela angeweza kusimama kama mgombea huru kutoka CCM badala ya kulazimika kwenda Chadema au TLP na wananchi wakamkubali na akarudi kutekeleza sera za CCM kuna ubaya gani hapo.
Mfano mzuri ni Seneta Joe Lieberman wa CT ambaye chama chake kilimkana na kumtupa nje kwa sababu anamuunga mkono Rais Bush. Baada ya kutupwa na chama chake akajisimamisha kama mgombea huru (independent candidate) na kushinda kiti cha Useneta. Chama chake kikamuomba radhi na kumhakikishia kuwa wataendelea kumpa seniority yake kama atapiga kura na demokrats. Akakubali na sasa ingawa ni seneta huru lakini yuko aligned na Demokrats.
Kama Njelu Kasaka angeweza kugombea kule Chunya na kurudi Bungeni au Hassy Kitine au wnegin wengi walioenguliwa na vyama vyao si Bunge letu lingekuwa moto moto? Wangeweza kuchagua wapi wanataka kupiga kura chama tawala au upinzani na wangekuwa ndio wale wanaoweza kubadilisha mwelekeo wa upigaji kura Bungeni.
Kugombea huru ni jambo zuri, la Kikatiba na uamuzi wa serikali kuifuta haki hiyo ni uamuzi wa "kipumbavu" kama alivyosema Nyerere. (I know some people flinch when they see that name.. you know I had to do that..)
Mkuu bila kubisha sana ebu turudi nyuma kwenye shina la hii issue.. Nini maana ya KIONGOZI?..
Nauliza hivyo kwa sababu huwezi kujijengea jina la Mheshimiwa (Hon) kuongoza wananchi kwa utaratibu unaoutaka wewe..sheria na utaratibu hutazama the mass population ama title kisha huijengea sheria kuipa kinga ya kutoingia wasiokuwa na haki. Kwa maana hii Diwani , Mbunge na rais hawa wote ni
Wa - Heshimiwa, hivyo utaratibu unatakiwa kulinda heshima hii kutolewa ovyo kwa mafisadi...
Kisha bado hujanijibu swali langu mkuu hawa wanaotafuta haki ya individuals kugombea Uheshimiwa wanashindwa kitu gani kujiunga na Upinzani ikiwa matokeo ya matunda ya kujiandikisha kwao hakutakuwa na tofauti kama wakiwa individuals.. Kama hawakubaliani na vyama vilivyopo then kwa nini wasituambie kwanza kile wanacho amini wao tofauti na vyama hivi..
Imean hii ndiyo inayomkuta Field Marshall Es na hata wewe wakati fulani yaani watu wanakupinga kitu lakini wao hawana jibu wala solution isipokuwa wanapinga tu ulichoamdika. Why? ati haikukaa sawa!
Sema basi usawa ni Upi? watu wanazunguka tuuuu, kumbe hata ukweli wa issue nzima hawana isipokuwa wanajaribu kudadisi zaidi upate kuingiwa hasira zaidi..[/QUOTE]