- Thread starter
- #41
wakoloni waliacha tawala za mitaa kwa machifu na watwale, watwale walichaguliwa na DC na kuidhinishwa na machifu, huu utaratibu wa watu kugombea ilikuja baada ya mwalimu kufuta uchifu. sasa hili la kampeni za uongozi wa mtaa kufanywa kichama sijui hili jambo la hovyo nani alilileta.
mimsingi uongozi wa kijiji ungefaa ufanywe kwa kugombea pasi kufuata ushawishi wa kichama, jamii ndogo ya mtaa kusema huu nibuongozi wa ccm na ule wa cdm na ule wa chauma tunapanda mbegu ya kishenzi sana.
fikiria kimara iwe ya ccm mbezi iwe ya chadema goba iwe ya act wazalendo tunatengeneza mfumo ambao mbeleni nchi haitatawalika. leo cdm inalalamika ccm kuua watu wao hiyo mitaa iliyoko chini ya cdm wana ccm watakaa kwa utulivu kweli?
napendekeza uongozi wa mtaa upatikane pasipo kufuata itikadi za vyama mtu agombee yeye kama yeye. hii itaondoa mgawanyiko wa kisiasa ngazi ya mtaa
hili la mtu kutoka ubelgiji anaenda kupiga kampeni ikungi na wala sio mpiga kura kwenda kuleta fujo tu, mwingine anatoka dar anaenda kazuramimba, mwingine anatoka dar anaenda shinyanga mbaya zaidi wengine ni mawaziri. huku ni kuleta taharuki tu zisizokuwa na maana yeyote.
Tungekubaliana kuachana na harakati za chaguzi kama hatuko tayari kwa zilizohuru na za haki.