Kupisha machungu ya ndugu kupotezwa au kuuawa kwa sababu za kisiasa kwanini tusikubaliane walioko madarakani wadumu milele?

Kupisha machungu ya ndugu kupotezwa au kuuawa kwa sababu za kisiasa kwanini tusikubaliane walioko madarakani wadumu milele?

Ni kweli, kwa nini tusiamue kwa umoja wetu tufute vyama.vya siasa ili tubaki na CCM moja.
Maana hakuna haya ya vyama vingi vinavyozalisha vilema, yatima, wajane.

Mkuu hata kwa umoja wao inatosha tu.

Tlaatlaah fikisheni maombi haya kwa mama mpendwa.

Atuache salama na familia zetu kwani nia njema ya ushindani wa haki haipo!
 
kama Taifa tunapitia changamoto za kibaradhuli kama ilivyo mataifa maengine ulimwenguni,

na hiyo haiwezi kusababisha hata kidogo, eti taifa libabaike au kuzubaa, lisisonge mbele na kupiga hatua za kimaendeleo..

makasiriko na mihemko libaki ni kua ni suala binafsi.

2025 Taifa litafanya uchaguzi mkuu kwa amani, bila mbambamba ya mtu au watu wa aina yoyote ile,

mpaka sasa,
kama taifa tupo pazuri sana na tunaendelea vizuri pia:pulpTRAVOLTA:

Changamoto za wizi wa chaguzi. Kukosekana nia njema. Uuwaji, utekaji na vya namna hiyo siyo changamoto za kibinadamu.

Hizo ni dalili za kutostaarabika, kukosa ubinadamu na uhayawani uliopitiliza.

Tuwaachie binadamu demokrasia na ujumuishi. Labda unyani ndiyo silika zetu. Tuukumbatie unyani wetu, maisha yaendelee
 
Ni machungu kiasi gani kwa familia za waliopotea au kuuwawa kwenye kadhia hizi za kisiasa?

Ni familia ipi inaweza kuhalalisha unyama huu kutokea katika familia yao?

Imekuwa ni kawaida watu kupotea au kuuwawa kwa sababu za kisiasa, huku kukiahidiwa chunguzi zisizokuwa na majibu.

Kwamba haya yanatokea na tatizo ni dhana ya demokrasia na utawala jumuishi tu, kutokuwa zimeridhiwa vilivyo?

Kwamba kama waliopo madarakani wakiachwa watawale milele ndiyo suluhisho la haya?

Kwa hakika kupisha machungu ya namna hii ipendekezwe walioko madarakani waendelee kutawala hadi watakapojichokea!

Naomba kutoa hoja.
Tatizo ni wajinga na wapumbavu

Upumbavu kwasasa ni kipaji hadi umepewa cheo cha uchawa Yaani yule mtu unaye mfahamu kwamba fuvu lake liko vizuri, (mbobezi), lakini anajizima data, yaani anaahirisha kufikiri kizalendo, (unyumbu wa kisiasa)

Kuchelewa kujua siyo ujinga, ujinga nikuto taka kujifunza, (lack of adaptability skills), yaani hawa wakipewa dhamana, (washika matonge), wanataka ufikiri wanavyotaka wao, yaani na wewe uwe mjinga

Je uko tayari kuwa mjinga na mpumbavu, yaani sifuri ukiambiwa ni 10 unakubali, mkojo uwe inye unakubali, mazingira ya biashara ni mabovu sema ni mazuri tena kwasababu ya.............
 
Kama taifa tuko pabaya kuliko wakati wowote katika historia.

Lucas Mwashambwa na Tlaatlaah watapinga, kichawa chawa.
 
Kama taifa tuko pabaya kuliko wakati wowote katika historia.

Lucas Mwashambwa na Tlaatlaah watapinga, kichawa chawa.
katika africa,
Tanzania ndilo pekee,
taifa lenye utulivu na linalopiga hatua za maendeleo kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa kasi zaidi,

huku chimbuko la yote hayo likiwa ni amani, utulivu na umoja wa waTanzania katika yote :pulpTRAVOLTA:
 
Changamoto za wizi wa chaguzi. Kukosekana nia njema. Uuwaji, utekaji na vya namna hiyo siyo changamoto za kibinadamu.

Hizo ni dalili za kutostaarabika, kukosa ubinadamu na uhayawani uliopitiliza.

Tuwaachie binadamu demokrasia na ujumuishi. Labda unyani ndiyo silika zetu. Tuukumbatie unyani wetu, maisha yaendelee
hayo yote unayolalamikia ni matatizo na changamoto binafsi, ambazo inafaa kutafutiwa ufumbuzi wa kibinafsi.

lakini kama taifa kwa kusema ukweli, mambo ya kisiasa, kijamii na kiuchumi yanafanyika kwa weledi na utulivu wa kiwango cha juu zaidi, ukilinganisha na nyakati zilizopita :pulpTRAVOLTA:
 
Mkuu hata kwa umoja wao inatosha tu.

Tlaatlaah fikisheni maombi haya kwa mama mpendwa.

Atuache salama na familia zetu kwani nia njema ya ushindani wa haki haipo!
Tanzania itaendelea kuzingatia misingi ya kidemokrasia ya vyama vingi ili kutoa fursa ya kutosha kwa wananchi kutoa maoni na mitazamo yao juu ya mambo mbalimbali nchini.

hata hivyo,
waliopoteza uelekeao, waliokosa sera, mipango au hoja ni vizuri kuchukua likizo au mapumziko, na wale wenye mipango na maono ya mbali, waendelee kutekeleza wajibu huo kwa uhuru na uwazi.

aidha,
ccm bado ndicho chama pekee Tanzania kinachoaminika na kukubalika kwa wananch kuongoza dola na serikali kwa niaba ya waTanzania wote :pulpTRAVOLTA:
 
Ni machungu kiasi gani kwa familia za waliopotea au kuuwawa kwenye kadhia hizi za kisiasa?

Ni familia ipi inaweza kuhalalisha unyama huu kutokea katika familia yao?

Imekuwa ni kawaida watu kupotea au kuuwawa kwa sababu za kisiasa, huku kukiahidiwa chunguzi zisizokuwa na majibu.

Kwamba haya yanatokea na tatizo ni dhana ya demokrasia na utawala jumuishi tu, kutokuwa zimeridhiwa vilivyo?

Kwamba kama waliopo madarakani wakiachwa watawale milele ndiyo suluhisho la haya?

Kwa hakika kupisha machungu ya namna hii ipendekezwe walioko madarakani waendelee kutawala hadi watakapojichokea!

Naomba kutoa hoja.
Tatizo ni wajinga na wapumbavu

Upumbavu kwasasa ni kipaji hadi umepewa cheo cha uchawa Yaani yule mtu unaye mfahamu kwamba fuvu lake liko vizuri lakini anajizima data, yaani anaahirisha kufikiri kizalendo, (unyumbu wa kisiasa)

Kuchelewa kujia siyo ujinga, ujinga nikuto taka kujifunza, (lack of adaptability skills), yaani hawa wakipewa matonge, (dhamana) wanataka ufikiri wanavyotaka wao
Kama taifa tuko pabaya kuliko wakati wowote katika historia.

Lucas Mwashambwa na Tlaatlaah watapinga, kichawa chawa.
Nani sala bongo
 
Hapana mkuu, wanaotekwa ni wanaotaka kuwatoa madarakani siyo sisi tunaowambea fisi kususiwa bucha.
hahaha CCM hawataki hivyo, wanataka muwasusie bucha halafu muwasifie, kuna mchungaji mmoja aliwahi kusema"Wanataka wakupige halafu usionyeshe hisia za maumivu au usilie kabisa" yani wana control maisha yako na utu wako.
Halafu wanapotumia nguvu kuendelea kutawala, pia muwasifu, wao ni malaika hawakosei.
 
Back
Top Bottom