Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Kwa wakongwe kama mimi, wanajiuliza, nini tutaona mageuzi ya maana na ya kweli. Walipofanya kweli Kenya, Malawi, na Zambia tulidhani ni wimbi na wingu vya kupita. Juzi tu, tuliona moto wa mageuzi na mapinduzi ukiwashwa kule Afrika Kusini ambapo ANC iliponea chupuchupu kujikuta pakanga. Kalba joto kupoa Botswana walifanya kweli. Msumbiji hawakubaki nyuma. Tunapoandika Frelimo haijui kama itaendelea kuula au kuliwa. Hakika, katika uhai wangu, naona ndoto ya Tanzania mpya kutoka mikononi na midomoni mwa machwa na kunguni. A Luta Continua. Mapambano Yaendelee na Kazi ya kufutulia na kuvunjilia chawa mbali iendelee. Je wewe unasemaje dugu yangu?