Kupitia Macho Yangu with passion for Love

Kupitia Macho Yangu with passion for Love

Axel Norid

Member
Joined
May 21, 2022
Posts
46
Reaction score
92
Uzi huu ni wa mapenzi wenye mfululizo wa picha za kustaajabisha zinazoakisi upendo kwa njia tofauti tofauti. Pia kutakua na nukuu zinazohusu mapenzi yan maneno matamu yenye upendo wa dhati na yanayogusa moyo na kuvunja moyo. Karibuni
 
"Furaha hii yote maishani mwangu, fahari yote na uaminifu katika penzi letu, hisia hii nzuri niliyokua nayo. Kwa kweli nina deni kwako!, Hivi ni vipi umeweza kuongeza furaha yangu na kuweka nuru inayo ng'aa katika maisha yangu, kuniongezea hisia za kuishi hadi sijui kama haya ni maumivu au raha, kwa kweli hizi hisia siwezi kuzielezea kuweza kueleweka. Yapaswa mimi kufikiria kuwa nina deni kwako la upendo wa dhati. Najua, lazima, utasikia wakisema " hakuna mwanaume anayempenda mwanamke mmoja au hakuna mwanaume mwenye mwanamke mmoja." Najua watasema kwa dhamira kali, lakini ukiwasikia wakisema yapaswa wewe kujua kwamba "mapenzi yetu Mimi na wewe ndo tunajua", na wala tusiwalaumu kwasababu hawayaoni tunayofanyiana. Lakin pia mimi siamini kuwa hakuna mwanaume aliwahi kumpenda mwanamke hapo awali kwa dhati kiasi cha kumuona yeye tu na wengine asiwaone, naamini walikuepo na watakuepo hata kwa uchache na Mimi nitakua miongoni mwao."
IMG_20220608_223738_088.jpg
 
ngoja nisome koment nimtumie kibajaji wangu
 
Back
Top Bottom