Uchaguzi 2020 Kupitia miundo mbinu iliyojengwa na Serikali ya Magufuli, CHADEMA wanafanyia kampeni

Uchaguzi 2020 Kupitia miundo mbinu iliyojengwa na Serikali ya Magufuli, CHADEMA wanafanyia kampeni

zagamba deo

Member
Joined
Oct 27, 2014
Posts
52
Reaction score
28
Tofauti na Nchi nyingine Duniani zenye siasa ya Vyama vingi, Tanzania ndo Nchi pekee ambayo Vyama vikuu vya Upinzani havijui dhana halisi ya Upinzani. Vyama hivi Vikuu Kama CHADEMA, CUF, ACT, na NCCR Mageuzi vimekuwa Vyama vya *"UPINGAJI"* kuliko kuwa Vyama vya Upinzani.

Katika Nchi nyingine Vyama vya Upinzani huja na Sera mbadala kwa lengo la kuongeza ufanisi wa pale Utendaji wa Serikali inayomaliza muda wake ulipofikia. Jambo hili Kwa Tanzania ni tofauti.... Vyama vya Upinzani vimekuwa na tabia ya Kubeza kila Jambo linalofanywa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi bila kuangalia linawanufaisha Watanzania wengi kiasi gani.

Hivi kweli Sera za CHADEMA kuwa Serikali imewekeza kwenye Vitu na sio watu zinatija kwa sisi wananchi wa Hali ya Chini?
Vitu Kama Umeme, Madaraja, Vivuko, Meli, Ndege, Barabara, Treni/Reli, Hospital, Shule, Maji havina uhusiano na Maendeleo ya watu?

Chadema kubeza uwepo wa Miundombinu hii ambayo kwa miaka mitano Dr. John Pombe Magufuli ameweza kufanya vizur katika Ujenzi wake ni kuonyesha Ni kwa namna gani hawana Nia njema na sisi wananchi wanyonge tunaonufaika na Fursa za ajira zinazotokana na Ujenzi wa Miradi hii na hata kuajiriwa kuendesha Miradi hii.

Ni kupitia Miundombinu hiyo hiyo CHADEMA wanaitumia kufanya Kampen zao kwa Uhuru na amani na hakuna anayewabugudhi, Hii ndo CCM, Chama kinachofundisha siasa kwa Vitendo.

Ni muda sasa muafaka kwetu sisi Kama wananchi kuamua kwa kauli moja kuwapuuza wagombea wote wanaotaka kutumia Propaganda kutuaminisha Mambo ya uzushi. Tujipange kuichagua CCM maana ndicho Chama haswa chenye ilani inayotekelezeka kwa manufaa ya Watanzania wote.

CHAGUA JOHN POMBE MAGUFULI KAZI IENDELEE.
 
Tatizo la Magufuli ni kuamini kwamba miundombinu ni mali yake yeye na chama chake, na hiyo hupelekea kuchukia anapoona wasiomuunga mkono wanaitumia.

Pia hakuna serikali yoyote ile katika dunia hii ambayo haijengi miundombinu. labda tatizo la kutokusafiri na kutokujifunza toka kwa viongozi wenzake ktk nchi nyingine ndiyo kumepelekea Magufuli kuamini kuwa miundombinu ni mali yake yeye na chama chake.
 
Rais wa JMT 2020-2025
1599744080302.png
 
Acha ujinga, karibu kutumia akili hata za Darasa la nne. Miundombinu inajengwa kwa Kodi za watanzania,million 55,hazijengwi kwa michango ya Wana CCM.

Ccm inawanachama 15M,Wananchi tupo million 55!!

Hii nchi sio mali ya ccm,Tanganyika ilikuwepo tangu 1880,ccm imeundwa 1977!

Wala ccm haijengi Miundombinu, Miundombinu inajengwa na watumishi wa umma,ambao hawapati kazi kwa vile Wana kadi za CCM.

CCM wanatumia pesa yetu kujenga,vile vile ndio mafisadi wakubwa,EPA,escrow,Kiwira,meremeta,Richmond,maskandali yote hayo yanafanywa na ccm.
 
kamilisha equation yako kama ifuatavyo:

kupitia kodi na tozo za Wanachadema, Magufuli akalazimika kujenga miundombinu ambayo leo Wanachadema wanastahili kuitumia.
sema Wanachadema wameamua tu kupotezea kufuatilia ufujaji wa kodi zao zilizotumika isivyo kujenga airport ya mtu binafsi kule kijijini Chato!
 
Kwa namna ulivyoijenga hoja yako, wewe huenda ni mnyonge zaidi wa kichwani kuliko unyonge wa mwili.

Hivi ni miundombinu gani ya pekee iliyohengwa awamu kuzidi awamu zilizopita?

Miundombinu ya barabara iliyojengwa awamu hii haifikii hata 25% ya awamu iliyopita.

Shule zilizojengwa awamu hii hazifikii hata 5% ya zile zilizohengwa awamu iliyopita.

Bwawa la umeme lipo kwenye hatua za mwanzo kabisa, na sidhani kama litaisha hata ndani ya miaka 5 ijayo.

SGR - ilitarajiwa ifikapo Nov 2018, ianze kufanya kazi kwa kipande kati ya Dar na Morogoro, mpaka leo hoi. Hata ndani ya miaka 5 ijayo haiwezi kufika hata Singida.

Ndege yangu zinunuliwe hazijaingiza faida hata mwaka mmoja. Na wala haitegemewi ATCL watakuja kuingiza faida.

Ukuaji wa uwekezaji umeshuka toka 28% mpaka 4%. Ukuaji wa utalii umeshuka toka 15% mpaka 3.6%.

Hivi kuna nini la pekee la kujivunia katika awamu hii zaid8 ya propaganda nyingi, hasa zinazowalenga wajinga?
 
Mkuu hivyo ulivyovitaja vinapaswa kuwa matokeo ya maendeleo.ila chenyewe Kama vilivyo si marndeleo
 
Hata kinyume chake ni sawa; yaani Chadema wangekuwa madarakani, CCM wangetumia hiyo miundo mbinu. Vipi kuhusu maendeleo ya kwenye halmashauri zilizoongozwa na vyama vingine vya siasa, CCM hawatumii?
 
Back
Top Bottom