Tofauti na Nchi nyingine Duniani zenye siasa ya Vyama vingi, Tanzania ndo Nchi pekee ambayo Vyama vikuu vya Upinzani havijui dhana halisi ya Upinzani. Vyama hivi Vikuu Kama CHADEMA, CUF, ACT, na NCCR Mageuzi vimekuwa Vyama vya *"UPINGAJI"* kuliko kuwa Vyama vya Upinzani....
Rekebisha kichwa cha habari yako,andika serikali ya Tanzania na siyo ya Magufuli.Pili,hatupingi kila kitu kama unavyoamini, kinachopingwa ni mbinu mnayotumia kuanzisha na kutekeleza huyo miradi mnayojisifia. Miradi huyo inafanywa kwa kodi za Watanzania wote bila kujalisha vyama vyao.Pia hatujawahi kupinga Ujenzi wa vituo vya afya Bali ni vichache mno kulinganisha na mahitaji,hivyo vituo vina uhaba mkubwa wa watoa huduma pamoja na dawa na vifaa tiba.
Kuhusu elimu,Sera ya elimu bure nilikuwa ya vyama mbadala ila jinsi mnavyoitoa kiholela bila kuzingatia uhitaji,haina ubora na waalimu hawatoshelezi kutokana na kukosekana kwa ajira na waalimu waliopo hawana motisha,miundo mbinu mibovu napungufu mno.
Kwenye miundo mbinu,tunakubali kuwa tunahitaji reli.Tulitakiwa kuifanyia maboresho TAZARA ambayo kimsingi ni sgr,kuweka miundo mbinu ya umeme,kuipa mabehewa ya kisasa ya abiria&mizigo ili kuiongzea ufanisi.Reli ya TRC ingekarabatiwa,kuipa vichwa vya kutosha na mabehewa ya aina zote halafu mapato yake yajenge sgr.
Suala LA umeme lilishatatuliwa kwa kujenga bombs LA gas toka Msimbati hadi Kinyerezi lakini mkarukia Nyerere Hydo Electronic Dam kabla ya kuitumia gas kuzalishia umeme rahisi.Tuna Coal,Geothermal na Wind or Sea Current Electronic generators. Tuna ng'ombe wa kuweza kutuzalishia Bio Gas ya kumwaga.
Watanzania siyo wajinga,tulitaka sana kuwa na ndege zetu ila jinsi mlivyozinunua ni kama mnakimbilia 10% ya manunuzi ya Cash Money. Mnavunja sheria za manunuzi mlizotunga wenyewe kwa ajili ya kujimwambafy kuwa nchi ni tajiri!Duniani kote ndege zinanunuliwa kwa mikataba na biashara huyo hufanywa na sekta binafsi kwa ubia na serikali.
Hii serikali mnayoiita ya CCM au Magufuli ni yetu sote,tufuate taratibu na kutendeana Hali ili tuendelee.Ubaguzi mnaoufanya hautupeleki kokote.
Sisi mnaotuita wapinzani na Mh.Lissu tuna haki zetu na ni Watanzania wenzenu hivyo tunatakiwa kufaidi matunda na mema ya nchi hii.
Tunamwaga Pombe na machicha yake yote.Mnabisha?