Uchaguzi 2020 Kupitia miundo mbinu iliyojengwa na Serikali ya Magufuli, CHADEMA wanafanyia kampeni

Hapo kwenye serikali ya Magufuli edit isomeke serikali ya Tanzania, ahsante
 
Acha ujinga,karibu kutumia akili hata za Darasa la nne. Miundombinu inajengwa kwa Kodi za watanzania,million 55,hazijengwi kwa michango ya Wana ccm.

Ccm inawanachama 15M,Wananchi tupo million 55!...

Mkuu bila kupinga maelezo yako mazuri, naona umesema ccm ina wanachama 15m. Ccm itoe wapi wanachama 15m? Kama ina wengi sana hawafiki 5m.
 
Kuna mambo huwa yananichanga sana yaani sanaa

Kila uchaguzi kuna chama cha Kijani kinadai kinatuletea Tanzania Mpya.

Nafikiri huwa wanamaanisha upya wa matatizo, ujinga na umaskini.

Fikiria kwa miaka 55+ sasa - wanasema tusichague wengine kwa kuwa wataondoa amani lakini wakati chini ya utawala wao wa kiimla tuna WASIOJULIKANA,VIROBA FUKWENI, Disapperance of Azory , kutapeliwa korosho zetu, Kuvunjwa haki za binadamu na sheria mbaya za ovyo ovyo
 
👊👊
 
..unajua haya maneno muanzilishi wake ni Magufuli mwenyewe.

..fuatilieni hotuba zake tangu akiwa waziri ktk serikali ya awamu ya 4.

Kabisa, hayo maneno kuwa wapinzani wanaandamana kwenye barabara zilizojengwa na ccm, yalikuwa ni maneno ya mara kwa mara ya Magufuli. Hata hili neno kupinga kila kitu ni maneno ya Magufuli, na kwakuwa kawashikia akili wanaccm wote, wanajikuta wanayarudiarudia hayo maneno.
 
Kwani anakusanya kodi kwa wanaCCM peke yao?, kama wanachadema nao wanalipa kodi, basi nao wanahaki ya kutumia miundombinu hiyo. Kwanini uteseke mkuu?.
 

..inawezekana huo ndio uelewa wa Magufuli kuhusu katiba yetu na demokrasia ya vyama vingi.

..inawezekana kwa dhati ya moyo wake anaamini kwamba hiyo miundombinu ni ya kwake yeye, na wana ccm wenzake.

..na zaidi anaamini kuwa wapinzani wataivunja na kuuza screpa.
 
Ungepewa wewe ungekataaa Acheni Unafki kawapa watanzania wenzenu hajawapa wazungu
Sipokeagi pesa nisiyofanyia kazi. Cha bure ghali sana mkuu. Hasa inapotoka kwa mwanaume mwenzangu
 
Na inaonekana kuna kina magufuli wengi tu
 
Comments zinaonesha elimu ya uraia iko mahali pake, uzi umefungwa.
 
Ujenzi wa miundo mbinu Ni wajibu serikali zote duniani, ukiona serikali inayo jisifia ujenzi wa miundo mbinu Ni serikali mufilisi.
 
Mkuu Jitahidi uwe unapata milo yote mitatu na kunywa maji mengi hadi moyo uelee..

May be akili yako itakaa sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…