SoC03 Kupitia wasanii wa sasa, je tunaenda kutengeneza kizazi cha aina gani hapo baadae na nani awajibike?

SoC03 Kupitia wasanii wa sasa, je tunaenda kutengeneza kizazi cha aina gani hapo baadae na nani awajibike?

Stories of Change - 2023 Competition

Ali Nassor Px

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2022
Posts
2,384
Reaction score
3,926
UTANGULIZI

Msanii ni mtu anayetumia lugha kufikisha ujumbe( kazi zake za sanaa) kwa jamii. kwa lengo la kuburudisha na elimisha.

Katika kutoa maana halisi ya fasihi simulizi kwenye kipengele cha msanii (mwanafasihi) kuna mtazamo unasema 'Msanii ni kioo cha jamii'. Kioo kazi yake kubwa ni kutuonesha kasoro zilizopo mwili huenda tunaziona tukapuuzia au hatukuziona kabisa hivyo kupitia kioo tutaziona hizo kasoro.

Msanii ni kioo cha jamii kupitia maudhui (contents )ya kazi zake kama nyimbo, maigizo, uchoraji, uchongaji nk.

Tunaweza kujiangalia kupitia hizo kazi na kujirekebisha ili kuendana na utaratibu rasmi wa jamii yetu.

Lakini pia kioo kinaweza kuvunjika hivyo kushindwa kutoa taarifa kamili au kwa usahihi kwa mtazamaji husika hivyohivyo msanii anaweza kuwa na tabia mbovu ambazo zinaweza kutoa taarifa chafu na zisizofaa kabisa kwa jamii yake.

Ni vema wasanii wakatambua kuwa wana jukumu kubwa katika jamii kuelimisha na si kupotosha.

Sanaa katika jamii zetu imeendelea kutumika kama dhana ya kusaidia jamii kujikosoa na kupata burudani.

Ajabu siku hizi wasanii badala ya kuwa kioo cha jamii wamegeuka kuwa giza, ambalo halionyeshi na hugubikwa na mambo ya ajabu.

CHANGAMOTO
Sanaa katika Jamii au taifa lolote lile ni sawa na kiumbe hai, ambacho kinaendelea kukua na kujifunza kulingana na wakati na kufanyia mabadiliko sanaa yake ambayo ni kielelezo cha utamaduni wa taifa hilo. Sanaa pamoja na wasanii ni nguzo muhimu katika kuelimisha jamii hasa pale jamii inapojitahidi kunakiri mambo bila kujua uzuri au ubaya wa jambo husika, hivyo sanaa ikitumika vizuri inaweza kusaidia kuondoa tatizo hili kwa jamii ambayo pengine imekosa elimu, au teknolojia mpya, na hata kushindwa kujifunza kwa sababu ya utofauti mkubwa wa mazingira na maendeleo.

Mmoja; Katika kufaninikisha malengo ya kuelimisha jamii, serikali huunda chombo cha kusimamia, kukuza na kuongeza maendeleo ya utengenezaji wa kazi za sanaa kulingana na maadili ya taifa.

Ndani ya Tanzania tunachombo ambacho kinaitwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Chombo hiki kinatakiwa kiwe ndio kiranja mkuu kwa kusimamia kazi za wasanii ili ziweze kuchezwa au kuonyeshwa kulingana na maadili ya taifa letu.

ukweli ni kuwa chombo hiki kinayumba na katika kujiendesha chenyewe na pia kwenye kusimamia maadili ya kazi za wasanii kwani wasanii sasa wamekuwa na nguvu ya kuleta mmomonyoko wa maadili katika ndani ya taifa letu.

Siku hizi kuna kazi za sanaa zenye maudhui machafu zinapigwa redioni na katika runinga. na mamlaka inashindwa kuzizuia mapema, huku BASATA inaonesha wameshindwa kuwawajibisha wale wasanii wachache wanaoharibu sifa nzuri ya kazi ya sanaa.

Taifa letu lina wananchi wa rika mbali mbali lazima kuwe na utaratibu kama ilivyo katika nchi za wenzetu onesho lolote lilizozalishwa ndani au nje ya nchi linaonyeshwa katika vyombo vyetu vya habari linatakiwa lioneshe ni rika gani wanatakiwa kulitazama.

Kwa mfano; ikionyesha kuwa Onesho hili ni “ Parental Guidance (PG) 13” hii inamaanisha kuwa wenye ruksa ya kutazama onesho hilo ni wale wote wenye rika ya miaka 13 na kwenda kuendelea ,wale ambao hawajafika umri huu sio busara kuona onesho hilo.

hivyo sheria au utaratibu ukieleweka, jamii nayo sasa inaanza kuwajibika kwa kuwaelimisha na kuwakemea kwamba hawastahili kuangalia onesho hilo.

Pili; kuwa tatizo la mmomonyoko wa maadili ni la muda mrefu. Mmomonyoko huu umekuwa ukiendelea na kukua labda kutokana na ukimya wa mamlaka husika (BASATA), kwa kuwa upande wa msanii au kumuonea muhali msanii fulani.

imefikia hatua hivi karibuni baadhi ya kazi za sanaa zisizo na maadili zinaifikia jamii. na jamii hususani watoto wanaipokea hiyo kazi na kuiona kama kazi ya kawaida tu kumbe ndo maadili yanamong'onyoka.

Kazi inaingia kwa jamii (wasikilizaji/ watazamaji) na haina maadili. inaenda kuathiri jamii. baada ya athari BASATA ndo inatoa tamko la kukemea. mda wote huu BASATA ilikuwa wapi mpaka kazi inawafikia jamii kazi ya kuratibu kazi za sanaa inafanywa na nani sasa.

20230603_194249.jpg

aiishi hapo BASATA wanakemea kuwa kazi ya sanaa hiyo haina maadili lakini kwenye tuzo kazi hiyo hiyo wanaiteua tena ishindanie na inashinda na kupewa tuzo juu.

BASATA linakemea jamii lakini inatakiwa kujua makosa ni yule aliye upitisha huo wimbo ufike Kwa walaji wa mwisho (jamii).

SULUHISHO

Baraza letu la sanaa (BASATA) linatakiwa kuanza kuchukua hatua kwa ajili ya kudhibiti mmomonyoko wa maadili kupitia sanaa.

i. Baraza linatakiwa kuendelea kuwaelimisha wasanii; kufanya kazi za sanaa na kuishi ndani ya maadili wakiwa nje na ndani ya kazi zao na sio kusingizia Pombe kuwa ndio iliyofanya mambo haya yote. kumekuwa na video nyingi chafu za wasanii zikisambaa mitandao kila siku.

ii. Udhibiti wa mamlaka na usimamizi wa wazazi ; Uwepo utaratibu wa kudhibiti kazi za sanaa ambazo husababisha mmommonyoko wa maadili kwa kwa vijana wetu. kazi za wasanii wetu kwa ujumla hazioneshi umri wa kuzitazama Parental Guidance (PG) na baadhi ya nyimbo zinatumia maneno mazito ambayo yamekuwa yakiimbwa na watoto.

mamlaka ipambanie kutimiza jukumu lake lakini pia jamii itimize jukumu lake la kusimamia maadili yake.

iii. Utekelezaji wa sheria bila kuoneana muhari;

sheria zitekelezwe pale msanii anapovunja sheria za baraza bila kutazama ukubwa wake.

Utekelezaji wa sheria utapendeza kama pia kutakuwa na ushirikishwaji wa wasanii kabla ya kutunga sheria na kanuni zitakazotoa muongozo wa maadili wa kazi zao za sanaa kiujumla.

Hii itasaidia kupunguza lawama na uvunjwaji wa sheria na kanuni baina ya wasanii na baraza lakini pia kwa jamii kiujumla.

iv. Elimu kwa wasanii; wasanii wetu wanahitaji elimu ya kuijua sanaa kuundani na busara ya kumchanganua nini waonyeshe, nini wavae, nini waimbena namna gani wacheze na pombe kama ni lazima itumike, itumike wapi na kwa kiasi gani.

kwani jukumu la wasanii ni kuelimisha na kuburudisha na sio kuburudisha tu. burudani bila mipaka inapeleka kupotosha jamii.

Itabidi BASATA wakae pamoja na wasanii kuwapa elimu kuhusu swala la maadili kiundani zaidi.

USHAURI KWA BASATA

Iwapo BASATA wameshindwa Kuwajibika ipasavyo kwa kusimamia na kutekeleza majukumu yao. kazi zisizo na maadili zitaendelea kuzalishwa kila siku.

Tunahitaji sanaa ambazo zitatuburudisha na kutuelimisha pia.

kinyume na hapo dhana ya sanaa na msanii ni kioo cha jamii itakuwa haina maana ya kuendelea kutumika tena.

Ukienda kuoga, kisha ukamaliza kuoga na ukatoka bafuni, ghafla ukagundua kuna povu halijatoka unaweza akaamua mmoja katika mawili.

ama UKAJISUUZE au UJIFUTE na taulo. Ingawa maamuzi yote yanaweza kuwa sawa lakini moja litakugharimu bila wewe kujua.

Nawasilisha.
 
Upvote 11
Kwa mashoga kama akina Diamond Harmfulnize na wenzake, ni balaa. Magufuli aliwabana baada ya habithi Kikwete kuwapa mwanya. Sasa huyu mtu wa Kikwekwe naye hao hao cha wote. Tunatengeneza kizazi cha mazezeta. Hebu fikria, mwandishi wa vitabu vya kufundishia vyenye wingi wa maarifa anakufa maskini wakati mashoga kama hao wanakufa mamilionea. Tatizo? Jamii yetu ni ya kipumbavu inayoogopa kuumiza bongo kufikiri na kupenda ubwete. Anaona fahari kukaribisha wakimbiza boli lakini siyo thinkers kwa sababu watamkosoa.
acha kuwazushia watu tuhuma ambazo hutaweza kuthibitisha ,kumwita mwanaume mwenzio shoga na unajua ana familia tena baba wa watoto na watoto zake watakuja kuona ulichoandika si busara hata kidogo hata kama ni kweli kuna namna nzuri ya kuwasilisha '
ukifanya hivyo huondoi tatizo unaongeza
na hicho ndicho kinawafanya wasanii warefrect jamii za hovyo wanazotoka maana kama mtu
mzima kama wewe unaropokwa maneno machafu namna hii vijana kina konde boy na Rayvann unategemea waimbe nini?

change mindsets nisamehe nikikukwaza!
 
Serikali na Jamii kwa ujumla imeshindwa lea watoto.

Ukienda uswahilini watoto wanaanza tombana wakiwa na miaka 8
 
Mkuu ingawa nitakuja kuandika tena maana hapa nipo bize kufanya jambo fulani la sanaa. Napenda kukufafanulia kuwa, majukumu waliyopewa BASATA kupitia marekebisho ya sheria na 5 yaliyorekebisha vipengele vya sheria ya National Arts Act no 23 of 1984. Yameipa mamlaka BASATA kukamata, kuzuia, kuharibu kazi za sanaa. Sanaa siyo jinai, hivyo marekebisho hayo Yanapingana na mkataba wa Kimataifa wa International Convenant of Economics, Social and Cultural Rights (ICESCR) ambayo

My word to you ni kwamba, BASATA kuhusika na maudhui ya sanaa ili kuyadhibiti ni ukiukwaji mkubwa wa Uhuru wa Sanaa ambao ni msingi muhimu wa Haki za Binadamu.

Nitarejea lakini unaweza kunikosoa kwa nilichoandika

I think kuna kitu imekisahau chief

Kwenye mkataba wa Kimataifa wa International Convenant on Economics, Social and Cultural Rights (ICESCR).



Ref; sehemu ya pili, Kifungu cha 4 inasema hivi:

The States Parties to the present Covenant recognize that, in the enjoyment of those rights provided by the State in conformity with the present Covenant, the State may subject such rights only to such limitations as are determined by law only in so far as this may be compatible with the nature of these rights and solely for the purpose of promoting the general welfare in a democratic society.


Hapa ni wazi mkataba unatambua mipaka na tofauti za tamaduni katika jamii za watu mbalimbali.

Lakini pia, Sheria Namba 1-6ya mwaka 2018 ; imeweka bayana nini msanii anapaswa kufanya katika kazi yake kabla hajaiwasilisha kwa walaji na wanachofanya kama Basata.

kwenye swala la kuhariri sio kwa ajili ya kuingilia sanaa au kumpangia msanii ila tu ni njia ya kulinda maadili na kuhakikisha kazi hizo zinaangaliwa au kusikilizwa kutegemeana na rika la watu na kuhakikisha zinazingatia maadili, mila na desturi.


Mimi bado nipo na wewe kuwa Sanaa siyo jinai ila lazima tuheshimu mipaka.

Sanaa ni ajira lengo la andiko hili sio kumkandamiza msanii lengo la andiko hili ni kumlinda msanii na jamii pia.

Hivi wewe kama mzazi kweli unaweza kufurahia kuona mtoto wako anaimba au anafanya matendo ya ovyo ambayo kayaona kwenye kazi ya sanaa ?
 
Tatizo sio wasanii ,tatizo lipo kwa jamii nzima kupenda mambo ya kiwaki kuliko
mambo ya maana na kwa sababu wasanii ni kioo cha jamii wanarefrect vile
jamii ilivyo pia mabadiliko ya sayansi na teknologia yanachangia kufanya hili suala kua
pana kimataifa ,utawabana kina Harmonize na Zuchu wakati kuna Naira Marley wa Nigeria na
Pabi Cooper wa South Afrika tunaona kazi zao?

teknolojia haipigwi ngumi na culture inachange now we are the World tusiwaangushie
Wasanii jumba bovu
utake usitake kula chuma hichoooooooo-!

Naheshimu mawazo yako mkuu lakini acha nikueleweshe kidogo.

Tatizo la mmomonyoko wa maadili kosa sio lao wasanii ila tu unatakiwa kujua swala la mmomonyoko wa maadili wasanii nao wana percentage zao na ubaya wa mambo wao ndo wanafatiliwa zaidi na jamii.

Japo kuwa swala la mmomonyoko wa maadili lina sababishwa na wengi ikwemo jamii pia.

Lakini wasanii wana nguvu kubwa sana.

Ubaya wa mambo wasanii wengi hawajui swala la kuelimisha kupitia sanaa zao bali wanachojua wao ni kuburudisha tu.

Sasa burudani inavuka mipaka yanaibwa matusi siku hizi.
 
Serikali na Jamii kwa ujumla imeshindwa lea watoto.

Ukienda uswahilini watoto wanaanza tombana wakiwa na miaka 8
Me nina imani bado haijashindwa kulea watoto ila imejisahau tu.

Kila mmoja akitambua wajibu wake watoto watakaa kwenye mstari
 
Me nina imani bado haijashindwa kulea watoto ila imejisahau tu.

Kila mmoja akitambua wajibu wake watoto watakaa kwenye mstari
Tushachelewa
Kila mtu alee mtoto wake vyema, asomeshe shule nzuri

Nursery schools nyingi hufundisha watoto kukatika
 
Tushachelewa
Kila mtu alee mtoto wake vyema, asomeshe shule nzuri

Nursery schools nyingi hufundisha watoto kukatika
Tukisema kila mtu alee mtoto wake bado tutakuwa hatujatoa tatizo kwa tafsiri itabaki kuwa mtoto wa mwenzako mkubwa mwenzako.

Ni ngumu sna kumlea mtoto peke yako maana ni ngumu kumchunga kila mda.

Kwako ataonesha heshima wewe kama haupo atafanya maovu.

Jamii inapaswa kelea watoto na sio kila mtu alee mtoto wake tutakuwa hatufiki ng'oooo
 
For an innocent mind, wasanii wetu hawaimbi matusi. Ila kutokana na kilichojaa katika jamii na vichwa vyao, they are seems to be. So kabla hujafika kwa wasanii , jamii inatakiwa iguswe kwanza. Tatizo liko kwa jamii yenyewe.
 
For an innocent mind, wasanii wetu hawaimbi matusi. Ila kutokana na kilichojaa katika jamii na vichwa vyao, they are seems to be. So kabla hujafika kwa wasanii , jamii inatakiwa iguswe kwanza. Tatizo liko kwa jamii yenyewe.

Wasanii wanaimba matusi , basata inasahau jukumu lake lakini pia jamii inashindwa kuchagua kipi cha kuchukua na kipi cha kuacha kutokana na ukosefu wa elimu au kuwachukulia vitu vya kawaida na wanavikumbatia wakidhani ni maua kumbe bomu linalusubiri mda wake lilipuke.

Swali langu je unaweza kusikiliza nyimbo ya K2GA inaitwa GOMA au SANDAKALAWE ya HARMONIZE ukiwa na mzazi wako yani baba yako au mama yako ?

Nasubiri jibu lako Samahani lakini.
 
Wasanii wanaimba matusi , basata inasahau jukumu lake lakini pia jamii inashindwa kuchagua kipi cha kuchukua na kipi cha kuacha kutokana na ukosefu wa elimu au kuwachukulia vitu vya kawaida na wanavikumbatia wakidhani ni maua kumbe bomu linalusubiri mda wake lilipuke.

Swali langu je unaweza kusikiliza nyimbo ya K2GA inaitwa GOMA au SANDAKALAWE ya HARMONIZE ukiwa na mzazi wako yani baba yako au mama yako ?

Nasubiri jibu lako Samahani lakini.

unafurahisha sana we jamaa. kwa hiyo wewe kila kitu huwa unafanya na baba yako na mama yako?
 
unafurahisha sana we jamaa. kwa hiyo wewe kila kitu huwa unafanya na baba yako na mama yako?
Haujanijibu swali langu mkuu na swali lako linataka jibu mmoja kati ya aya mawili


1. naweza

2. Siwezi

Lakini lengo la kukupa mfano wa wazazi lilikuwa ni


• Baba au mama ni watu wa kwanza kabisa ambao mtoto anawaheshimu inawezekana hasimuheshimu mtu baki lakini anapokuwepo mzazi heshima inakuwepo na mara nyingi analo ambiwa anatii
 
For an innocent mind, wasanii wetu hawaimbi matusi. Ila kutokana na kilichojaa katika jamii na vichwa vyao, they are seems to be. So kabla hujafika kwa wasanii , jamii inatakiwa iguswe kwanza. Tatizo liko kwa jamii yenyewe.
Lakini la nyongeza pia ilikujua wasanii wanaimba matusi au hawaimbi matusi.

Unatakiw kujua nini maana ya msanii

Ukipata jibu la nini maana ya msanii basi utakuwa teyal ushapata jibu nani wenye tatizo kati ya msanii na shabiki/ msikilizaji
 
Mamlaka zikifanya kazi yake ipasavyo
Familia zilitimiza jukumu lake katika malezi ya watoto
Tutakuwa na jamii bora

Ukiacha basata kuzifungia nyimbo mbovu wanaweza kuwatunza wasanii waliotoa kazi bora hii itaamsha wasanii waone chakufanya
Kwenye familia pia tuangalie nyimbo ambazo watoto wanaishi wakizisikiliza
 
Mamlaka zikifanya kazi yake ipasavyo
Familia zilitimiza jukumu lake katika malezi ya watoto
Tutakuwa na jamii bora

Ukiacha basata kuzifungia nyimbo mbovu wanaweza kuwatunza wasanii waliotoa kazi bora hii itaamsha wasanii waone chakufanya
Kwenye familia pia tuangalie nyimbo ambazo watoto wanaishi wakizisikiliza

Facts tupu kiongoz
 
Back
Top Bottom