Kwa kawaida huwa hakuna malipo yoyote kwa personal belongings (kuna jina lake kitaalamu kwenye lugha za kodi ila nimelisahau). Zamani kidgo maafisa wa forodha walikuwa wanapiga mkwara kusudi uwape kitu kidogo. Kuna wakati nilirudi na nguo nyingi sana masanduku manne ya kilo 40 kila moja; nguo zile kulikuwa na za kwangu na nyingine ambazo nilikuwa nimepata donation kupeleka kwa ndugu na marafiki huko kijijini kwetu. Maafisa wa forodha walitaka kunipiga mkwara sana na kuna jamaa mmoja alikuwa anasema hiyo ni biashara ya mitumba. Hata hivyo baadaye walinielewa wakaniacha, ingawa walifanya hivyo baada ya kunicheleshewa ndege ya precisionair niliyokuwa naenda nayo Shinyanga. Kwa hiyo nikalala dar es Salaam hadi kesho yake. Gharama ya Kulala na usafiri dar es Salaam ilikuwa ni kubwa kuliko hongo ambayo ningeweza kuwapa. Wakati huo nyumba yangu ilikuwa kule changanyikeni haijaisha, na sikuwa nategemea kusumbumbua ndugu na marafiki hapo jijini.
Mizigo yangu haikuwa Cargo, bali ilikuwa unacompanied luggage ambayo ilikuwa kwenye ndege ile ile niliyoruka nayo; kwa hiyo tulifika pamoja.