Kupokea mahari ni sawa na kumuuza binti yako (tunauza mabinti kwa wanaume)

Kupokea mahari ni sawa na kumuuza binti yako (tunauza mabinti kwa wanaume)

K 4 LIFE

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2015
Posts
2,567
Reaction score
416
Tunaelewa kuwa kijana akitaka kuoa lazima apeleke mahari aliyopangiwa upande wa msichana, suala la kupokea mahari PESA , ni sawa na kumuuza binti yako kwa mwanaume. Hapa mnabadilishana kibiashara zaidi, unatoa PESA unapata MKE.

Kwa kifupi hapa tunaendeleza biashara ya kuuzana kama enzi za utumwa tu, kama watu wamependana wao, wewe mzazi kwa nini udai PESA/ mahari? Kama sio biashara ni nini hiyo? Na ndio maana wanawake wanapigwa na kuteswa na waume zao, si wamewanunua kwa pesa bwana?
 
NI MILA NA DESTURI ZA WATU

=> MWANAMKE utakae mchukua BURE BURE huwezi kuwa na thamani nae, MAANA UTAMWACHA KESHO NA UMCHUKUE MWINGNE WA BURE BURE mfano maisha ya baadhi ya watu DAR ES SALAAM, unaoa mchana usiku unafukuza ili aingie mwingne "KAMA UNABADILI NGUO VILE"
 
mkuu kama hujaoa hautakiwi kutoa mahari utakua unanunua binadam mwenzako

hamna kitu kibaya kama mwanaume kukosa chochote, anyway jitumeni muwe hata na laki mbili ukifika unawapa unaahidi utaleta unapewa mke maisha yanaendelea hawawezi kukunyang'anya
 
Mbona wanatolewa mahari.kibao na wanaachwa vilevile KAMA nguo
 
NI MILA NA DESTURI ZA WATU

=> MWANAMKE utakae mchukua BURE BURE huwezi kuwa na thamani nae, MAANA UTAMWACHA KESHO NA UMCHUKUE MWINGNE WA BURE BURE mfano maisha ya baadhi ya watu DAR ES SALAAM, unaoa mchana usiku unafukuza ili aingie mwingne "KAMA UNABADILI NGUO VILE"

kwa hiyo tuna wanunua hili tuwe dhamana nao au?
 
Mahali ni value ya mke inabidi utoe jasho kumpata mke nje ya hapo mke wa bure nikama umeokota kona baa!
 
hamna kitu kibaya kama mwanaume kukosa chochote, anyway jitumeni muwe hata na laki mbili ukifika unawapa unaahidi utaleta unapewa mke maisha yanaendelea hawawezi kukunyang'anya

kwa hiyo unatanguliza advance kwanza
 
sawa ni value lakini kwa upande wa pili tunawageuza bidhaa
Hiyo ni akili ya mhusika haiusiani na kutoa mahali!maana hata ukumfunga jembe la kukokota na ng'ombe huwezi singizia ni mahali!!kwanza ngoja nimpigie mpenzi wangu kwanza!
 
Mahali ni value ya mke inabidi utoe jasho kumpata mke nje ya hapo mke wa bure nikama umeokota kona baa!

Safi sana mkuu tusijifanye sisi tuna akili kuliko mitume na manabii mahali ipo hata ktk maandiko
 
Mwanamke kutolewa mahari ni sawa na kumuuza kwa mwanamme tu.kilichobadilika badala ya kuitwa pesa ikaitwa mahari.
 
Hiyo ni akili ya mhusika haiusiani na kutoa mahali!maana hata ukumfunga jembe la kukokota na ng'ombe huwezi singizia ni mahali!!kwanza ngoja nimpigie mpenzi wangu kwanza!

msalimie sana shemeji
 
Back
Top Bottom